Nini kifanyike ili viongozi na wapiga kura tuheshimiane?

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Kuna tabia naona inaota mizizi sasa viongozi wa serikali wanajiona kama wao ndio wasemaji na waamuzi wa matakwa ya watanzania wote

Kama ambavyo tumesika matamko 'mbali mbali mara leo tena nasikia kuna mwehu na mwendawazimu mmoja eti anashauri msajili wa vyama afute vyama vya upinzani utadhani mahitaji ya vyama hivyo kayataka yeye

Mwingine anasema ndani ya mkoa wangu sitaki hiki wala kile bali nataka hiki na kile kienyeji tu kama wamewehuka na mamlaka waliyo pewa

Wametufanya watanzania mabubu hatuongei, viziwi hatusikii na vipofu hatuoni, wanatuona ni mataahira ambao hatujui kitu na wala hatujui tunataka nini na hatutaki nini.

Nauliza: nini kifanyike ili hawa wendawazimu na wehu walio wehuka na madaraka wajue kwamba wao ni viongozi wa wananchi na sio viongozi wa matakwa yao na matamanio yao?

Maaana wanaona wao wanaweza kuwaamlia watanzania over 50 milion nini cha kufanya kwa kauli zao tu ambazo hazina ushirikishwaji wa wanao waongoza.
 
Back
Top Bottom