Nini kifanyike ili tupige hatua zaidi kimaendeleo kama taifa?

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
757
842
Nimekuwa nikifilia kwanini tupo hapa tulipo kimaendeleo kama Taifa, je tunastahili kuwa hapa tulipofikia au tulitakiwa kuwa hatua zaidi ya hapa tulipofikia?.

Ukiangalia kwa undani vitu karibu vyote vinavyochangia kufanikisha maendeleo tunavyo kama Taifa, mfano; Raslima watu, Maliasili, n.k.

Sisi kama Taifa tunakwama wapi na nini kifanyike ili tupige hatua zaidi ya hapa tulipofikia?.

Mimi nashauri haya yazingatiwe pia ili tupige hatua zaidi;

1. Tuwe na mifumo isiyoweza kuingiliwa na mtu, kikundi, chama chochote cha siasa, n.k. kwa maslahi yao.

2.Tuwe na mhimili yenye uhuru kamili, ili checks and balances tuione haswaa!.

3.Tuwe na malengo ya Kitaifa na si malengo ya yatokanayo na makundi, yaani timu za wataalam wabobezi bila kuangalia mitazamo, itikadi za kisiasa, n.k. wawe wanakaa kwa pamoja kisekta kutuandalia malengo hayo ya Kitaifa.

4. Asiwepo mtu asiyeweza kuwajibishwa nahasa apokiuka maslahi ya Taifa.

Naomba na wewe uongezee, nini unaona kinaweza kufanyika ili hatua zaidi ipigwe kamaTaifa kimaendeleo?.
 
NI KWELI MKUU KWA LUGHA RAHISI TUFANYE FACTORY RESET KAMA TAIFA. MADUDU NI MENGI MNO KAMA TAIFA
Tuanze upya kila sekta kwa mipango madhubuti na yenye tija kwa kila sekta
 
Tangu uhuru tuko chini ya mfumo wa CCM wenye mapichapicha yaleyale, kama tulitakiwa tuwe tumefika kwenye hatua zaidi ya hii, kikwazo ni mfumo tuliona nao wa kiccm umezeeka umeishiwa fikra mbadala za kutusogeza hatua nyingine mbele, dawa ni kuufyekilea mbali mfumo wote wa kiccm na kuingiza mfumo mpya wenye fikra mpya.
 
Mchawi wa maendeleo ya kweli nchini mwetu ni CCM na vibaraka wake. Kivipi? Mjadala wake ni mpana sana. Ila ikatokea siku ccm ikaondolewa madarakani, hakika kama nchi tutapiga hatua kubwa sana kimaendeleo.

Unapoitaja CCM; unataja unafiki, wizi, ufisadi, umungu mtu, kikundi cha uhalifu, ubaguzi, majungu, kutukuzana, kuabudiana, kikundi cha familia/koo, mchwa, fisi, kikundi cha wachawi, majambazi, nk. Kwa hali hiyo maendeleo tutayapata wapi?
 
Mihimili mikuu ya nchi na matawi yake imefungamanishwa na chama tawala so tatizo ndo linapoanzia. Soln ni kuua ccm full stop
 
5. shughuli za kisiasa zisihisishwe na harakati za aina yoyote na vyama vyote vya siasa za harakati viondolewe na kufutiwa usajiri.

6.tuwekeze zaidi kwenye elimu ujuzi na maarifa ambayo itamfikia kila mtu na ikiwezekana ule mpango wa ELIMU KWA WOTE upitiwe upya kuendana na mazingira ya sasa ya kiuchumi, tiba, sayansi, teknolojia na sanaa.

7. iwepo dira ya taifa ya muda mrefu ambapo vyama vya siasa lazima vitengeneze ilani zao za uchaguzi kulingana na dira hiyo.

8. kuwepo kwa vipaumbele vya kitaifa vya maendeleo.

9. kuwepo kwa mikutano na mijadala ya wazi na Mara kwa mara ya wachumi na watafiti wengine wakijadili fursa na nini kifanyike kutumia fursa.
 
Hapo kwanza ni ELIMU.mfumo wa elimu ufumuliwe kabisa na tuanze na mfumo rafiki unaoendana na karne ya 21,kufuta A-level sekondari.na kubadili mifumo mingine ya kielimu.

Kujikita kwenye viwanda vya kati.kisha bidhaa zikizalishwa kwa wingi nchini zile bidhaa za kutoka nje tunazizuia zisiingie nchini.,lakin kwa viwanda vya juice na maji hatuwezi bado.

Idara ya usalama wa taifa(TISS)itafute vijana wenye akili nyingi na wazlendo kwa taifa lao.(sio chama na serikali).Kisha wawe na uchunguzi wa kina kila nyanja ya kiuchumi na kijamii ili kusukuma maendeleo ya wizara husika.

Ikibidi kama taifa (kwa pamoja)tuchague mambo kadhaa ya kudeal nayo mfano matatu tu kwa miaka 10 labda ni afya,elimu na ajira.Miaka 10 mingine ni miundombinu ,viwanda na biashara.
 
Kama taifa kwa pamoja tuungane na kuiunga mkono serikali hii ya awamu ya 5 ambayo imeonyesha nia dhabiti ya kuijenga Tanzania yenye uongozi ulio wazi, Lakini baadhi yetu wamekua wakijisahau na kusahau tulipotoka eti kisa tu Mbowe kasema watanzania hawana uhuru katika vyombo vya habari jamani tubadilike na ifike wakati tuijue siasa na sio kufata mkumbo wa kina Lissu...
 
Back
Top Bottom