Nini kifanyike ili Mashabiki wa Simba wasije kung'oa tena viti wakifungwa?

Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
5,358
9,232
Habari wadau, niende kwenye mada moja kwa moja...

Tunajua Simba wana matarajio makubwa msimu huu baada ya kuongoza ligi ya NBC Premier league huku wakijiandaa na michuano ya African Football league maarufu kama super League, lakini ukitazama kwa jicho la mwewe Simba ametangulia na baskeli ya miti huku bingwa halisi akija na kwa mwendo wa Ferrari.

Hofu yangu siku Simba akifungwa na Yanga asije kung'oa tena viti pale uwanja wa Taifa na kulitia Taifa hasara maana ni mabilioni mengi tu nasikia yametumika kuukarabati uwanja.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2016 Simba walishang'oa baada ya kushindwa kuvumilia kichapo kutoka kwa wababe wa Jangwani Dar Young Africans .

Pamoja na kupigwa faini ya Milioni 25 bado hawakukoma kwani mwaka uliofuatia yaani 2017 mashabiki hao lia lia wa Simba maarufu kama Kolo FC walichapana makonde na kung'oa tena viti baada ya wataalamu wa soka Tanzania Dar Young Africans kuichapa Al Ahly Bao moja bila kwenye mechi za kufuzu kuingia Makundi ya Klabu Bingwa.

Mashabiki hao waliokuwa wakiishabikia Al Ahly walichukizwa na ushindi wa Yanga hadi wakaanza kung'oa na kutwangana viti vya utosi huku wakisonya .

Lakini kwa kuhofia kupigwa tena faini aliyekua msemaji wa simba Kwa wakati huo Bi. Asha Muhaji alikanusha kuwa waliohusika na fujo hizo sio mashabiki wa Simba, lakini ili kuienzi kauli ya Mwenyekiti wao wa zamani Bwana Eden Ismail Rage akaonesha Umbumbumbu kwa kudai kuwa waliofanya hizo fujo ni mashabiki wa Al Ahly waishio Tanzania namnukuu hapa.

“Sisi tunaamini waliofanya vile ni mashabiki wa Al Ahly kwani ndio waliokuwa wapinzani wa Yanga siku hiyo, kwanza inashangaza Simba tunahusikaje katika mechi tusiyokuwa na maslahi nayo. Pia ikumbukwe uongozi wa Simba siku zote umekuwa ukipinga vitendo vya uvunjifu wa amani zikiwemo vurugu, sasa mtu anaposema Simba imehusika mimi nadhani wana agenda ya siri kutaka kuichafua klabu yetu,” alisema.

Akizungumzia kigezo cha wahusika kuvaa jezi zenye rangi nyekundu inayotumiwa na klabu yake alisema, si kweli Simba ndiyo inayotumia jezi zenye rangi nyekundu pekee.

“Ukiachilia mbali Al Ahly wenyewe, zipo pia timu nyingine hapa nyumbani zinazotumia rangi kama hiyo kama vile Coastal Union, Small Simba nk. ingawa simaanishi kama ndizo zilizohusika na tukio hilo hapana, nachotaka kusisitiza kuwa rangi si kigezo cha kumtuhumu mtu, ningependa Simba isihukumiwe kwa hilo”.

Sasa wadau kwa jinsi navoona inabidi hatua za mapema zifanyike ili kuwadhibiti hawa wakora wasijefanya tena Umbumbumbu wao maana hawana uvumilivu .

Leta maoni yako, je, hatua zipi zifanyike ili kuwadhibiti?

images.jpg
images%20(1).jpg
 
Habari wadau ..?

Niende kwenye mada moja Kwa moja... Tunajua Simba Wana matarajio makubwa msimu huu baada ya kuongoza ligi ya NBC Premier league huku wakijiandaa na michuano ya African Football league maarufu kama super League.
Nje kidogo ya mada. Hivi timu gani kutoka hapa Tanzania zinazoshiriki mashindano ya African Football League?
 
Hizo zama zilipendwa...sasa timu kama Alhaily ikufunge ung'oe viti kweli? yani mbabe wa Africa....yani Simba pale tunaenda kuongeza umaarufu ikiwa bahati yetu tunawapiga kimoja tunapaki bus... Tungefungwa na IHEFU tungeng'oa mpaka meno....
 
Habari wadau?

Niende kwenye mada moja Kwa moja... Tunajua Simba Wana matarajio makubwa msimu huu baada ya kuongoza ligi ya NBC Premier league huku wakijiandaa na michuano ya African Football league maarufu kama super League.

Lakini ukitazama Kwa jicho la mwewe.. Simba ametangulia na baskeli ya miti huku bingwa halisi akija na Kwa mwendo wa Ferrari.

Hofu yangu siku Simba akifungwa na Yanga asije kung'oa tena viti pale uwanja wa Taifa na kulitia Taifa hasara maana ni mabilioni mengi tu nasikia yametumika kuukarabati uwanja.

Ikumbukwe kua mwaka 2016 Simba walishang'oa baada ya kushindwa kuvumilia kichapo kutoka Kwa wababe wa Jangwani Dar Young Africans

Pamoja na kupigwa faini ya Milioni 25 bado hawakukoma kwani mwaka uliofuatia yaani 2017 mashabiki hao lia lia wa Simba maarufu kama Kolo FC walichapana makonde na kung'oa tena viti baada ya wataalamu wa soka Tanzania Dar Young Africans kuichapa Al ahly Bao moja bila kwenye mechi za kufuzu kuingia makundi ya klabu bingwa.

Mashabiki hao waliokua wakiishabikia Al ahly walichukizwa na ushindi wa Yanga hadi wakaanza kung'oa na kutwangana viti vya utosi huku wakisonya

Lakini Kwa kuhofia kupigwa tena faini aliyekua msemaji wa simba Kwa wakati huo bi. Asha Muhaji alikanusha kua waliohusika na fujo hizo sio mashabiki wa Simba, lakini ili kuienzi kauli ya mwenyekiti wao wa zamani bwana Eden Ismail Rage akaonesha Umbumbumbu Kwa kudai kua waliofanya hizo fujo ni mashabiki wa Al ahly waishio Tanzania namnukuu hapa.

“Sisi tunaamini waliofanya vile ni mashabiki wa Al Ahly kwani ndio waliokuwa wapinzani wa Yanga siku hiyo, kwanza inashangaza Simba tunahusikaje katika mechi tusiyokuwa na maslahi nayo, pia ikumbukwe uongozi wa Simba siku zote umekuwa ukipinga vitendo vya uvunjifu wa amani zikiwemo vurugu, sasa mtu anaposema Simba imehusika mimi nadhani wana agenda ya siri kutaka kuichafua klabu yetu,” alisema.

Akizungumzia kigezo cha wahusika kuvaa jezi zenye rangi nyekundu inayotumiwa na klabu yake alisema, si kweli Simba ndiyo inayotumia jezi zenye rangi nyekundu pekee.

“Ukiachilia mbali Al Ahly wenyewe, zipo pia timu nyingine hapa nyumbani zinazotumia rangi kama hiyo kama vile Coastal Union, Small Simba nk. ingawa simaanishi kama ndizo zilizohusika na tukio hilo hapana, nachotaka kusisitiza kuwa rangi si kigezo cha kumtuhumu mtu, ningependa Simba isihukumiwe kwa hilo”.

Sasa wadau Kwa jinsi navoona inabidi hatua za mapema zifanyike ili kuwadhibiti hawa wakora wasijefanya tena Umbumbumbu wao maana hawana uvumilivu

Leta maoni Yao je hatua zipi zifanyike ili kuwadhibiti.
Mimi nadhani ni vizuri waelezwe mapema kua huko TATU MALOGO hatakuwepo wa kuwapa magoli ya offside na kukataa magoli halali ya wapinzani wao.
 
Hizo zama zilipendwa...sasa timu kama Alhaily ikufunge ung'oe viti kweli? yani mbabe wa Africa....yani Simba pale tunaenda kuongeza umaarufu ikiwa bahati yetu tunawapiga kimoja tunapaki bus... Tungefungwa na IHEFU tungeng'oa mpaka meno....
Mbumbumbu wadhibitiwe gharama nikubwa imetumika halaf mwaka naiona dalil yawao kuvunja viti mana wanatimu mbovu ila inashinda kimagumashi pira nibebe sasa siku wakifungwa watachachaa sn mana msemaj wao amewahakikishia watulie hatakama pira bovu ila matokeo uhakika
 
Habari wadau, niende kwenye mada moja kwa moja...

Tunajua Simba wana matarajio makubwa msimu huu baada ya kuongoza ligi ya NBC Premier league huku wakijiandaa na michuano ya African Football league maarufu kama super League, lakini ukitazama kwa jicho la mwewe Simba ametangulia na baskeli ya miti huku bingwa halisi akija na kwa mwendo wa Ferrari.

Hofu yangu siku Simba akifungwa na Yanga asije kung'oa tena viti pale uwanja wa Taifa na kulitia Taifa hasara maana ni mabilioni mengi tu nasikia yametumika kuukarabati uwanja.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2016 Simba walishang'oa baada ya kushindwa kuvumilia kichapo kutoka kwa wababe wa Jangwani Dar Young Africans .

Pamoja na kupigwa faini ya Milioni 25 bado hawakukoma kwani mwaka uliofuatia yaani 2017 mashabiki hao lia lia wa Simba maarufu kama Kolo FC walichapana makonde na kung'oa tena viti baada ya wataalamu wa soka Tanzania Dar Young Africans kuichapa Al Ahly Bao moja bila kwenye mechi za kufuzu kuingia Makundi ya Klabu Bingwa.

Mashabiki hao waliokuwa wakiishabikia Al Ahly walichukizwa na ushindi wa Yanga hadi wakaanza kung'oa na kutwangana viti vya utosi huku wakisonya .

Lakini kwa kuhofia kupigwa tena faini aliyekua msemaji wa simba Kwa wakati huo Bi. Asha Muhaji alikanusha kuwa waliohusika na fujo hizo sio mashabiki wa Simba, lakini ili kuienzi kauli ya Mwenyekiti wao wa zamani Bwana Eden Ismail Rage akaonesha Umbumbumbu kwa kudai kuwa waliofanya hizo fujo ni mashabiki wa Al Ahly waishio Tanzania namnukuu hapa.

“Sisi tunaamini waliofanya vile ni mashabiki wa Al Ahly kwani ndio waliokuwa wapinzani wa Yanga siku hiyo, kwanza inashangaza Simba tunahusikaje katika mechi tusiyokuwa na maslahi nayo. Pia ikumbukwe uongozi wa Simba siku zote umekuwa ukipinga vitendo vya uvunjifu wa amani zikiwemo vurugu, sasa mtu anaposema Simba imehusika mimi nadhani wana agenda ya siri kutaka kuichafua klabu yetu,” alisema.

Akizungumzia kigezo cha wahusika kuvaa jezi zenye rangi nyekundu inayotumiwa na klabu yake alisema, si kweli Simba ndiyo inayotumia jezi zenye rangi nyekundu pekee.

“Ukiachilia mbali Al Ahly wenyewe, zipo pia timu nyingine hapa nyumbani zinazotumia rangi kama hiyo kama vile Coastal Union, Small Simba nk. ingawa simaanishi kama ndizo zilizohusika na tukio hilo hapana, nachotaka kusisitiza kuwa rangi si kigezo cha kumtuhumu mtu, ningependa Simba isihukumiwe kwa hilo”.

Sasa wadau kwa jinsi navoona inabidi hatua za mapema zifanyike ili kuwadhibiti hawa wakora wasijefanya tena Umbumbumbu wao maana hawana uvumilivu .

Leta maoni yako, je, hatua zipi zifanyike ili kuwadhibiti?
Kila anaeng'oa kiti na yeye ang'olewa kichwa.
 
Back
Top Bottom