Nini hatma yetu wanandoa watarajiwa?

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,323
3,353
HAPO ZAMANI

Muongo takribani mmoja na nusu uliopita hakukuwa na tukio la heri na lililoheshimika kama kuoa/kuolewa.

Nyakati hizo mke/mume aliheshimika ndani ya jamii yake.. Alihesabika kama mtu mzima aliyestaarabika.

Siku zote mke alikuwa chini ya mume kwa kila kitu, alimheshimu mume hata kama mume akikosea bado heshima kwa mumewe ilibaki kuwa juu... Juu mawinguni..

Mke alibaki kama kielelezo cha familia imara, yenye heshima, amani na furaha.. Alibaki kuwa mtatuzi wa migogoro kwa busara na hekima iliyotukuka.. Maa zote kilichochangia kumrekebisha mume ni hekima na busara za mke mwenyewe.. Ndoa zilikua imara kwelikweli..

Mume alibaki kama kichwa cha familia kwelikweli.. Mke alimtengenezea mumewe juice akamkabidhi kwa kuinama kwa heshima, akamnywesha kwa upendo.. Alimtengea maji angalabu akamuogesha kama sio kuoga wote.. Mke alibaki kama mtunza siri za mume na familia.. Kuna mengi ya kumwelezea mke huyu.

SIKU HIZI

Mke anaona aibu.. Kupiga goti kwa mumewe... Mume akikosea n gubu mwanzo mwisho.... Hela ikipotea tayari ushaachwa...

Elimu ya usawa imewaharibu kina dada wa kileo hadi wanaingiza elimu na vipato vyao katika ndoa.. Mke anataka usawa na mumewe anasahau kuwa mama zao walidumu katika ndoa zao kutokana na HESHIMA NA KUTAMBUA MAJUKUMU YAO

Mume akikosea na mke analipiza, ni mwendo wa ukimwaga mboga namwaga ugali.. Mtamwaga chakula wee mwisho wa siku ndoa chali... Watoto wanabaki kuishi maisha ya single parent na parent wa kambo...

Siku hizi ndoa ni fasheni tu... Ndoa imekua ya kishkaji tu.. Unaambiwa mke analiwa nje na mume anakula nje.. Fresh

Siku hizi mtu anaoa huku anajua kabisa atakula na wenzake....

Wakewa siku hizi hawatimizi majukumu kabisaa., wanakimbilia housegirl huyohuyo anafua nguo a mumewe na anamtengea maji ya kuoga ama chakula.. Kitandani nimechoka na sijisikii zimekuwa nyingiii...

Mume unachambwa hadi chakula kinagoma kupita kooni... Unaandaliwa chakula na mke kavimba sura kwa kisirani

Hata kama umemuoa jua kabisa yule jamaa mwenye kiswift pekee kitaa akiamua kummega anammega tu... Unaachwa na sanlg yako unajiita mume wa fulani.. Kina dada hawana msimamo kabisa..

Kinadada mnakwama wapi au ndo malezi ya siku hizi... TUTAOWA WAPI JAMANI...ina maana wake wema wameisha?

Ndoa zetu zitakuwaje..???

images-55.jpeg
 
Wanawake wamekuwa wataftaj sana wanaona nafasi yq mwanaume katika maisha yake ni ndogo sana.
Hata akikupoteza hana hasara.
Maana maisha anaendesha poa tuu
 
Wanawake wamekuwa wataftaj sana wanaona nafasi yq mwanaume katika maisha yake ni ndogo sana.
Hata akikupoteza hana hasara.
Maana maisha anaendesha poa tuu
Kwa maana hiyo mama zetu waliolewa ili wayaendeshe maisha yao kupitia baba zetu?

Wanawake wamekuwa wachaarikaji tangu enzi na enzi kinachotokea sasa ni kkosa heshima.... Ndoa imepoteza maana kabisa
 
Kwa asilimia kubwa ipo hivyo.
Mama zetu waliokomaa ndoa zao zisivunjike tofauti na wake zetu.
Pia mafunzo yao ya unyago na ukali wa wazazi wao ulisaidia. Lkn leo mzazi anachangia ndoa ya mwanae kuvunjika anamwambia njoo nyumbani kwenu hujaua.
Mtoto anapata kiburi

Kwa maana hiyo mama zetu waliolewa ili wayaendeshe maisha yao kupitia baba zetu?

Wanawake wamekuwa wachaarikaji tangu enzi na enzi kinachotokea sasa ni kkosa heshima.... Ndoa imepoteza maana kabisa
 
Nini suruhisho kwa vijana wanaotarajia kuoa/kuoiewa
Kwa asilimia kubwa ipo hivyo.
Mama zetu waliokomaa ndoa zao zisivunjike tofauti na wake zetu.
Pia mafunzo yao ya unyago na ukali wa wazazi wao ulisaidia. Lkn leo mzazi anachangia ndoa ya mwanae kuvunjika anamwambia njoo nyumbani kwenu hujaua.
Mtoto anapata kiburi
 
Wanawake wamekuwa wataftaj sana wanaona nafasi yq mwanaume katika maisha yake ni ndogo sana.
Hata akikupoteza hana hasara.
Maana maisha anaendesha poa tuu

Anakua single mamaa..
Malezi ya watoto hapa ndipo yanapopotea
 
Back
Top Bottom