Nini hatma ya CCM baada ya Rostam...


Kiswahili hiki cha kujiuzuru na many topographycal errors ni mambo mawili ambayo yamekosesha sana thread yako mvuto.Mara nyingine ukiandika hakikisha kwamba unapunguza makosa yasiyo ya lazima as much as possible.Kiswahili cha Nyelele,kufulu,kujiuzuru achana nacho.
 
Najifunza kiswahili mkuu wangu, Mkerewe wapi na kiswahili fasaha!
 
naukiangalia kwa undani nadhani ccm kama chama cha mapnduzi chama chetu chama tawala
ambacho kinaelekea mwisho hakuna daraja lisilo na mwisho , Libya wananchi wake wanavyoishi
maisha mazuri wanalipwa mashahara na kujengewa nyumba bure lakini wamechoka je tujiulize
hiki chama narudia hiki chama cha ccm kimetufanyia kuwa maskini kuliko wate ukanda wa afrika mashariki
kila kitu kimepanda bei ,matibabu ,nyakula,umeme ,maji ,mafuta kwa Binadamu wa kawaida mwenye
Akili sawa sawa hataweza kukisaport adha wawe tu ni wale wateule wachache wanaofaidi keki ya taifa
hivi wewe unaye post vitu vya ajabu na kukusifia chama hicho kilichoshindwa bara bara ya kule kijijini
kwako na nahayo maandaki wanaotuachia wanaochimba dhahabu .najiuluza hivi wanazo akili au ni
Machizi nenda kwenye mahospital kaangalie watu wanavyolala chini kwenye sakafu nenda hapo
hospital kubwa ya mjini muhimbili je kama muhimbili watu wanalala chini je na huku vijijini itakuwa je

KIKUPACHO RAHA NA UCHUNGU KITAKUPA
 
Mkandara nakubaliana na analysis yako.Pia nakubaliana na ile notion kwamba siasa zetu ni kama upepo unapovuma.Nina amini kuwa RA atatumia nguvu nyingi sana kujaribu kuisambaratisha CDM.

Tukirudi kwenye hoja ya kwamba hatma ya CCM itakuwaje,basi ukweli ni kwamba hivyo vyeo alivyojivua havitaamisha kwamba sasa hatakuwa na influence kwenye maamuzi kama ilivyokuwa hapo awali.Kama ni uweka hazina wa CCM,basi hakuwa nao tena.Level aliyokuwa nayo ni higher one,na ni behind the scenes kama wanavyodai kuwa ni King maker.Sasa sidhani kama uking maker wake ulitokana na hivyo vyeo vya magamba aliyojivua.Kwasababu kama ni vyeo,basi EL ndo angekuwa King Maker since alishawahi kuwa Waziri mkuu.

Hatma ya CCM kwene hili inategemeana na the rest of the twins na maamuzi yao,Kwasababu walijumuishwa kama "mapacha watatu" Basi hili linanikumbushia ile kauli ya "the axis of evil."Na hivyo basi wakakti tunajadili hatma ya CCM,tusisahau kuwajumuisha hao mapacha waili waiiobakia.Kwamba itakuwaje kama;

a)Wote wakifuatia na kujivua gamba.

b)Mmoja pekee yake akijivua;ie ikiwa ni EL peke yake ama AC peke yake.

Mwishowe umegusia kuhusu nguvu za JK zitatokea wapi.Mkuu nikueleze kitu kimoja siasa za TZ ni za ajabu sana,yani ni shida kuzitabiri.Hata hivyo kuna yale ambayo tunaweza kuyatabiri kutokana na matukio halisi yanayooneakana na wananchi mara baada ya hayo mambo ya behind the scenes.Kwa mfano;ni wazi kabisa kuwa mikataba mara nyingi ni rahisi sana kuingia lakini kutoka ni mara nyingi almost impossible.Mkataba kama unalinufaisha Taifa utajulikana tu na kama n wa kifisadi pia itajulikana kwasababu ya matokeo ya mikataba hiyo mara ikishatake place.Tunashuhudia mambo ya umeme sasa tunaamibwa ni mvua.Tunajuwa ni waongo kwasababu walituambia wanalishughulikia ie Dowans.

Kwa hiyo kuwavua magamba watu walioingia mikataba mibovu haina maana kuwa mikataba hiyo sasa ni batili.Hapo tuwe makini sana.Kwa hiyo hao watu wanaweza bado kuwa na influence kama bado wanaendelea kunufaika na mikataba hiyo na pia kama bado iko valid.Kama wanajivua magamba halafu wananchi bado wanaendeleA kula hasara kutokana na mamuzi yao, hayo,basi haijalishi kama wamejivua magamba ama la,bado watakuwa na influence,na hivyo shida ya ufisadi kuendelea kuwepo.Kama JK angelikuwa anasimamia maslalhi ya Taifa kiukweli,basi tungeweza kuwa na matumaini,na story zingekuwa tofauti na si hizi innuendos.
Kama nilivyosema,lets wait and see.
 
wakale walisema ukimbana sana paka kwenye ukuta atatokea kwenye mbavu zako
sasa jamaa wamechoka watasema ukweli muda si merfu

kikupacho raha na uchungu kitakupa
 
Nachofikiria mimi kwa vile huyu jamaa aliitwa KING MAKER na sishangai kwamba RA kuwa anajulikana nje zaidi ya anavyojulikana ndani kwa watanzania nahisi bado kazi ipo tena si ya kitoto,kwa maana anao uwezo wa kuoganaizi mambo huko nje na hata akaleta makampuni hapa Tz na akaiingiza serikali yote chaka kwa mtindo uleule wa mikataba ya hovyo,anao uwezo mkubwa sana na ameweza kupata siri nyingi sana kujua ujinga wa watanzania kwahiyo endapo akiamua kufanya itakuwa ni gharika

Anyway hatma ya CCM kwangu doesn't matter kwa maana tayari inaonekana ipo pabaya na itaiacha nchi yetu mortuary,the only that aches my head ni kwa jinsi gani CDM itaendelea kukua na kusimama ili kutake over the dying CCM kwa sababu CCM itake isitake kama hawa mapacha wanakwenda kustep down wote CCM can't stand as one anymore,ni lazima itafall apart into pieces i.e ya EL,Chenge na ya JK,S6
 
Mkuu haya yote ndio yalipelekea mimi kuanza kujiuliza hatma ya CCM... yaani nchi yetu kweli ni kama jahazi linalofuata upepo, pengine wapo wanajimu wanaoweza kutupa warning mapema...
 

Vipi, hukuelewa lililoandikwa? Mbona inaonekana kuwa thread ina mvuto wa kutosha kiasi kuwa imepata wachanagiaji wengi tu. Ningekubaliana nawe kama makosa hayo uliyoandika yangefanya mada isieleweke kabisa. Watu wengine wanaandika kwa kutumia pda's zenye keyboard ndogo sana kiasi cha kufanya iwe ngumu kufanya masahihisho baada ya kuandika lakini, bado mada zao zinaeleweka pamoja na makosa hayo.
 

Mzee Mwanakijiji,

Nimefurahishwa sana na mfano wako wa kumfananisha RA na ile habari ya Samson na Delila na Wafilisti kwenye Biblia.
Mfano huu unaweza kuwa katika sura 2 tofauti, sura ya ku-match au ya kuto-match. Iwapo uta-match ina maana CCM inaenda KUFA. Maana Biblia inasema Samson baada ya kukamatwa na Wafilisti wakamtoboa Macho akawa kipofu na baada ya SIKU KADHAA ZILE NYWELE ZILIOTA na hapo Samson akapata akili ya KULIPIZA KISASI. Alitafuta nguzo ya mhimili wa Jengo kubwa walilokuwa wakifanyia sherehe na SAMSON aliikamata ile nguzo akaivunjilia mbali na WATU WOTE WALIOKUWEPO KWENYE HILO JENGO WAKAFILIA MBALI. Kwamba baada ya RA kujivua gamba atawasubiri CCM kwa wakti mwafaka(nywele ziote) halafu ATAWALIPUA KWA PIGO AMBALO KAMWE HAWATALISAHAU. Kumbuka huyu jamaa ilikuwa kwenye the inner circle of the Gutter politics kama alivyoziita mwenyewe. Kwa hiyo he knows much about CCM,uchafu wote wa kina Kikwete,Lowasa,Chenge,Mramba,Yona,EPA issues k.m. Deep Green,KAGODA n.k. Anaweza akavuta subira halafu ata-strike back au ku-revenge. CCM patakuwa hapatoshi. Walioanzisha siasa UCHWARA YA KUJIVUA GAMBA WATAJUTA kwanini walianzisha upuuzi huo.

Iwapo mfano huu hauta-match basi ndiyo kusema UTAKUWA MWISHO WA RA KISIASA NA KIBIASHARA. Kama kweli siasa alikuwa akiitumia kama mlango au mtaji wa kufanikisha biashara zake.
 
they did not
 
Maneno mengi lakini hakuna hata moja lenye maana..CCM ni kubwa kuliko kina Rostam au umesahau kuwa wametajirikia kupitia CCM.

Wamekutajirisha na wewe? Lakini hujajibu hoja ya mstakabali wa CCM Bw. Zuzu
 
Mi wasi wangu ni hii kadi ya CCM anayoing'ang'ania!! Kulikoni? Inawezekana vp analalama siasa uchwara na za hovyo ziszo na tija ndani ya CCM yeye haziwezi na bado kadi ya chama ipo mkononi maana yake ni nini?

Hii kadi anaing'ang'ania kwa sababu sidhani kama kaondoka jumla jumla huyu, ni lazima atarudi tu katika kinyang'anyiro cha 2015 kuja kumpigia debe la nguvu EL au mgombea mwingine ambaye mafisadi wataamua ndiye anastahili kuingia Ikulu dhidi ya wale wanaopigiwa debe na Kikwete akina Asha Migiro, Karume na Hussein Mwinyi.
 
Ni kweli kufikiria mstakabali wa CCM ni jambo jema.

Mimi namuona RA kwa upande tofauti.

1. Ni wakala aliyefanikiwa kuingamiza CCM kwa kuitengenezea viongozi na uongozi usiofaa.

2. Ameingiza mbinu na mikakati michafu ya kibiashara katika siasa ambazo zimeathiri CCM na nchi eg EPA, RICHMOND

3. Hotuba yake ya kujivua gamba ni vijembe kuwa bila yeye CCM haipo.

Hayo yote yanakamilisha usemi au methali ya "Ukimchekea nyani utavuna mabua".

Tatizo

CCM bado hawawezi kusimama in time na kukiri kwa furaha kuwa RA kujiuzuru ni kutimiza azma ya kujivua gamba. Walivyo wapuuzi sasa hivi wanawasiliana kwa ukaribu na RA ili kuwepo na muafaka na msimamo wa pamoja. Hapo RA lazima atawaingiza mkenge MWINGINE maana ndiyo taaluma yake.

Fursa ya CCM kurejea uhalisia wake haipo. IT IS DAMAGED BEYOND REPAIR. Hakuna cha kuwasaidia wachache waliobakia ni lazima wawepo siyo kwa sababu wanaipenda bali hawajui na wala hawana choice kwa jinsi ambavyo walipoteza fursa nyingi walizozipata. Moja wapo ni kuwabagua na kuwanyanyasa wanaowaita wapinzani.

MUSTAKABALI WA CCM NI MAJUTO NA HASA KWA JK
 
Reactions: Ame
It's still a drama. Its my hope that only time will tell the real truth and everything will be out. Therefore every move should be careful watched.


You should not worry yourself for nothing....Kushinda vita usiyejua mwanzilishi wake na ninani unayepigana naye ni ngumu sana; unabaki kuhisi pengine ni huyu ukimgeukia unagundua siye mwingine ukienda unakuta hola.... Hii vita hakuna atakayeweza kuipangua maana ni circumstancial; kila wahusika wanapojaribu kufanya move wakidhani labda itakuwa afadhali ndo kwanza mambo yanaharibika zaidi. Acha niwape ushauri tu kwamba hakuna dhalimu yeyote anayejulikana ama asiyejulikana atabaki salama. Nimekuwa nikilisema hili nakulirudia lakini ni kama vile watu hawaoni; hawasikii wala hawaelelwi.

Ninapowacheki watu nikiwa pembeni wakidhani pengine ni CHADEMA; labda wana CCM (Maarufu kama wapinga ufisadi); labda wafadhili wa vyma et etc huwaninaona jinsi mwanadamu alivyodhaifu akizitegemea akili zake za damu na nyama....Lakini ukweli ni kuwa hivi vita ni vya watanzania wanyonge walioonewa kwa muda mrefu nakuonekana kuwa hawawezi kujisaidia maana wamechukuliwa kuwa kama wajinga wasiojua kitu wala kujitambua huku hao "wajanja" wakisahau kuwa hata kuta za yeriko zilibomoka bila physical force yeyote zaidi ya nyimbo za kusifu na zumari za wana israel....

Ninayasema haya kwa uhakika bila kigugumizi; hakuna fisadi atakayesalimika this time nawala asijisifu mtu yeyote kuwa ni sababu ya anguka la udhalimu maana wasiopenda na wanaopenda kupinga ufisadi kwakujua ama kutokujua watashika sila kuuangamiza ufisadi. Wengine watajikuta wanalazimika hata kama wao wenyewe ni washirika huku wakijua kuwa watakuwa victim lakini kwakua mbingu na vyote viijazavyo dunia vitakuwa vina act in favour of this decree watajikuta nao pia wakisaidia kuuangamiza kwa mikono yao wenyewe; kwani wanalazimika kufanya hivyo maana hawana pa kukimbilia wala pakujificha ili wasitekeleze agizo hili la kuuangamiza huu ufisadi.

Mwenye sikio na asikie neno hili!


Hii nikwaajili ya kuweka record sawa ili wakati wa bwana ukifika na mimi nisimame kuliinua jina Mungu wetu aishie asiye na upendeleo wala ubaguzi!
 
Hapa ndipo nashindwa kuwaelewa Watanzania. Yaani pamoja na kelele zoote, kilichokuwa kinaliliwa ni Rostam Aziz kuachia Ubunge na Unec na mambo kwisha ! Mkuu Mkandara unaposema amefukuzwa na kujiuzuru ni kufunika kombe tu mwanaharamu apite unaniacha hoi maana kama ni kufukuzwa angefukuzwa chamani na vyeo vyote alivyo navyo vingeota mbawa - lakini thubutu !

Lakini yeye anadai atabaki mwanachama mwaminifu wa CCM sasa hapa ndipo swali linajitokeza, ni makosa ya namna gani yanaweza kufanywa na mwanachama hadi kusababisha afukuzwe ! Kama nakumbuka vizuri kilio cha wana CCM kabla ya hapo ilikuwa RACHEL wafukuzwe ila kwa sababu hawafukuziki kirahisi kuna usanii umeandaliwa hapa wa kufunika kombe mwanaharamu apite.

Katika hii sinema imekuwa rahisi kwa Rostam kushirikishwa kuliko hao wenzake wawili na kuna kila dalili kuwa Kikwete halali akiomba wana CCM watulie wasikurupuke wasijekitia kitumbua mchanga. Na kweli hakuna wa kuthubutu kukohoa, ni kama vile kilichotokea kimewapiga ganzi hata watayarishaji wenyewe huku watazamaji wakijiuliza kama mpira umetinga golini kwao au kwa wapinzani wao.

Labda mchezo ndio unaanza, yetu macho................! Ninavyowaelewa CCM hivi sasa wangekuwa mitaani wakimpongeza Kikwete, lakini mh !
 
Kuna kitu watanzania wengi tulikuwa hatukijui nacho ni 'chama kushika hatamu'. Tulidhani ni kelele tu, wenzetu walijua maana yake ni nini. Watu hawakushangaa wenye mabilioni kugombea NEC, CC n.k. Ukweli ni kuwa RACHEL wanajua jinsi ya kujipanga, kushambulia na kuzuia.
Si mnakumbuka walivyomkona Sitta wakati anachezea 'rasilimali' zao za Richmond!!

RA anaijua system vizuri sana, alichofanya ni kupunguza headlines. Amejijenga sana ndani a chama na ndiyo maana alikuwa anamwaga pesa ima mtu andoke au achaguliwe. Kamuulizeni Mangula. Ndivyo ilivyo kwa RACHEL yote.
Kuonyesha wana nguvu hakuna atakayeshitakiwa kwa lolote lile, nani atathubutu!

Kwasasa hali inaonekana kama ni shwari na kuondoka kwa RACHELkunaweza tafsiriwa kama kujisafisha. Not!
JK hana cha kupoteza zaidi ya kumpa nafasi ya kupumua kutokana na kubebeshwa mzigo wa marafiki, ana uhakika na 10 yrs.

Katika kipindi cha miaka 2 tutaona CCM kimya na tambarare, lakini mjue RACHEL wapo active wakijipanga kwa kuelewa kuwa safu imeingiliwa na mushkeli. Mwaka 2013-2014 Tutasikia mengi na mengine yanaweza kuleta mtikisiko mkubwa.
Wata hit back fiercely, kwanza kujipanga, pili kutengua mitego ya wapinzani wao ndani ya chama, tatu kumuumbua mshirika aliyewatosa na wale walioasi. Sasa hivi wapambe wa RACHEL wame- retreat but not surrender. Hali itakuwa mbaya sana, just matter of time.
 
Halafu Rostam katibua hali ya hewa CCM, mwenyewe kakimbilia Sweden anakula kuku huku CCJ jana wanajiosha kule Mbeya!
 
Maneno mengi lakini hakuna hata moja lenye maana..CCM ni kubwa kuliko kina Rostam au umesahau kuwa wametajirikia kupitia CCM.
Kumbe!! Kwa hiyo ccm has facilitated them kuiba na kuwa mafisadi. Kwa hiyo ukitaka utajiri na kuwa fisadi ujiunge na ccm. Nakumbuka na Makamba sr aliropoka hivyo.Mbona unaidhalilisha ccm.
 

Hiyo retreat ndo gud bye forever amen! Hata Pharao aliwaachia wanawaisrael waende na baadaye aliwakimbiza ili awateke tena na kuwarudisha utumwani Misri, yeye mwenyewe akiliongoza jeshi lake na kutumia sila na askari wake wote lakini wote wakaishia bahari ya Sham; ndivyo itakavyokuwa kwao! Wafikishie hizi salamu hakuna fisadi atakaye kanyaga Ikulu 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…