Nini hasa tofauti ya Mbwana Samatta na wachezaji wengine?

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,044
3,963
Mbwana Samatta kijana mtanzania ambaye anaonekana kung'ara kila kukicha kwenye timu yake ya Genk huko Ubelgiji, amenifanya kujiuliza;

1. Je, nini hasa ambacho alifanya na anaendelea kufanya Mbwana Samatta kwenye maisha ya soka na maisha ya kawaida, ambavyo wachezaji kama Mrisho Khalfan Ngassa alishindwa kufanya na matokeo yake kutofanikiwa?

2. Wachezaji wanaoonekana kung'ara kwa sasa kwenye ligi ya Vodacom kama Shiza Kichuya na wengine, wanatakiwa wafanye nini hasa kwenye maisha yao ya kawaida na ya soka kwa ujumla ili kufikia na hata kuvuka level aliyopo Mbwana Samatta kwa sasa?
 
Tatizo la wachezaji wa bongo wepesi kuridhika,aking'aa msimu mmoja tu basi,anaongeza mke km mrisho ngasa!!ndo kinawaponza wachezaji wengi wa kibongo
 
Mimi sio mpnz wa mpira ila namuombea sana Mbwana Samatta afike mbali.
Very humble guy, n determined.
Na Mungu azidi kumtangulia.
Anaonekana ana njaa(hunger) na matamanio(desire) ya ku-make it to the big time.
Na ata-make it tu.
 
Kwani Ulimwengu mbona hazungumzwi sana?!! Au kwa kuwa hafungi kama Samata?!! Naona kwenda Mazembe pia kulisaidia kupata exposure zaid katika soka la ushindani na la kibiashara. Alipata advantage km ya Ulimwengu ukifananisha na hawa wengine.

Vilabu vyetu bado sana kwenye kukuza kipaji cha mchezaji nje ya juhudi,bidii au nidhamu ya mchezaji husika.
Wangapi tumewapeleka majaribio ya soka nje?! Idadi bado ndogo ikichangiwa na hao mawakala ambao kimsingi sio wengi TZ. Kiufupi bado kuna changamoto nyingi sana kwa hao wachezaji na vilabu vyetu. Km kikosi cha kwanza timu/klabu kubwa waTz wanahesabika,ni wazi hatuna hazina ya kutosha kwenye vilabu vyetu. Na hata hao wanao anza,ukiangalia uwezo wao kutoka timu husika bado kwa kweli.

Spain na brazil,una beki tatu na beki mbili wazur kibao wanagombea namba moja,leo tz hilo bado ndoto. Akitoka mhusika,anayeingia ni kawaida tu.
Naskia Maximo ndio alikuja na kutoa elimu kuhusu vyakula kwa wachezaji,sasa kama vitu vya msingi kwenye vilabu vyao hawapati unategemea nin!? Tuwe na academies za kutosha,vijana wapikwe tokea wadogo kiufundi,misosi husika,nidhamu,bila shaka matunda tutayaona tu. Hawa wazee wengi wao jua lishazama
 
Back
Top Bottom