Nini hasa siri ya kuachwa kwa ole medeye.?

Nini hasa siri ya kuachwa kwa ole medeye.?

Kanuniya68

Senior Member
Joined
May 26, 2013
Posts
157
Reaction score
44
Mabadiliko ya baraza la mawaziri yameleta sura mpya lakini pia yamewaondoa baadhi ya waliokuwepo. Mmoja kati ya walioondolewa bila kutarajiwa ni mh.ole medeye aliyekuwa naibu waziri wa wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi. Je ni nini kilichomfanya naibu waziri huyu kuachwa. Je ni zile tuhuma kuwa anafanya siasa za ukabila arusha? Au ni 'kuonekana ikiwa bega kwa bega' na 'kujionyesha waziwazi' akimuunga mkono mh.lowasa?...lakini pia pengine ni 'kuperfom' chini ya kiwango?..(ingawa mimi binafsi siamini kama hiyo inaweza kuwa ni sababu,kwani kuna wale 'mizigo' wamepeta)...ni nini siri hasa ndugu zangu?
 
Nadhani hilo la Lowassa linahusika na yawezekana pia hakuwa na mahusiano mazuri na mkuu wake na hivyo kuonekana mzigo.
 
Kwa mambo yalivyo sasaivi? unawezakuta jamaa alikuwa na mkono wa birika.:hand:
 
Nadhani hilo la Lowassa linahusika na yawezekana pia hakuwa na mahusiano mazuri na mkuu wake na hivyo kuonekana mzigo.

watasubiri sana...
mwenzao huku anaendelea na strategies za kutwaa ikulu,
Lowassa hoyeeeeeeeeeeeeee
Pasco itikia!
 
Last edited by a moderator:
Amevuliwa wadhifa ili uchunguzi ufanyike pasipo pingamizi au maslai ya nafasi ya uongozi juu ya tuhuma zake za kuchochea wamasai kuwaua wengine wanao ingia ktk ardhi ya ki masai, kama ilivyotokea ktk nauaji yakutisha hivi majuzi.
 
Huyu jamaa ndo alitakia kuwa mzigo namba moja! Na sababu ulizozitaja hapo juu zinahusika sana!
 
huyu ni kipindupindu arusha ukabila ndo umetoa
 
mabadiliko ya baraza la mawaziri yameleta sura mpya lakini pia yamewaondoa baadhi ya waliokuwepo. Mmoja kati ya walioondolewa bila kutarajiwa ni mh.ole medeye aliyekuwa naibu waziri wa wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi. Je ni nini kilichomfanya naibu waziri huyu kuachwa. Je ni zile tuhuma kuwa anafanya siasa za ukabila arusha? Au ni 'kuonekana ikiwa bega kwa bega' na 'kujionyesha waziwazi' akimuunga mkono mh.lowasa?...lakini pia pengine ni 'kuperfom' chini ya kiwango?..(ingawa mimi binafsi siamini kama hiyo inaweza kuwa ni sababu,kwani kuna wale 'mizigo' wamepeta)...ni nini siri hasa ndugu zangu?

badala ya kuuliza kwanini ameachwa , hebu jiulize kwanini aliteuliwa ?
 
Kumbe definition ya mzigo kwa JK ni tofauti na ile ya kina Nape na Kinana.

Hawa ndugu sijui wataficha wapi nyuso zao...Walijiaminisha kwa asilimia mia kwamba mizigo itatuliwa..kumbe mkuu ndio kwanza kaongeza mbeleko
 
Mkabila ambaye hadi karne hii hajastaarabika kabisa..ila pia NDOTO ZA EL..ukanda wa CCM, na mengine ni mojawapo ya mambo yanayompa JK shida sana.JK hakuweza taja majina hadharani kwa vile anajua kuna watu hawezi watazama machoni...au hata kujibu maswali ya waandishi.
 
Kuna watu wamemlaumu na
kumbeza Rais katika uteuzi wake
wa Baraza la mawaziri.
Wakuu, baraza la mawaziri ni hitaji
la kikatiba. Wawe mizigo au
wasiwe mizigo lakini sio utashi wa
Rais. Ni ngumu sana kufanya kazi
bila kuwa na mawaziri. Kwaiyo kwa
kukidhi hitaji la katiba ambalo Rais
hana option anajaza cabinet
miongoni mwa wale
tuliomchagulia. Sasa wengine
tulimpeleka Ole Sendeka, wengine
Lusinde, Wengine tulimpeleka Maji
Marefu, wengine tulimchagua Idd
Zungu, sasa rais anachagua humo
humo,
Na uteuzi wa Baraza la mawaziri
pamoja na factors zingine
hupaswa kuwa la Kitaifa. Kwaiyo
uiano wa mawaziri kimikoa
wanayotoka ni muhimu sana.
Otherwise utajikuta huna cabinet
ya kitaifa. Kaondoka Nchimbi wa
Ruvuma kaingia Jenista wa
Ruvuma. Amefariki Mzee wetu
Mgimwa wa Iringa amekuja
Mgimwa mwingine wa Iringa. Yule
mkabila wa Ngorongoro katoka
amekuja Tetele sijui Telele nae ni
wa jamii ya wafugaji. Rais hachagui
hovyo jamani...Na ninaamini ni
moja kati ya kazi ngumu sana rais
aliyonayo kupanga safu ya
Mawaziri. Kwa kuzingatia uwiano
huo kawapata hao. Otherwise kwa
dodoma Nkamia angeachwa
angeteuliwa Lusinde na kadhalika
na kadhalika. Mnyonge
mnyongeni....
 
Una hoja ila ni nyepesi. nasema hivi kwa sababu katika uteuzi tukiangalia atokako mtu basi itabidi tuangalie pia kabila lake,dini hata rangi pia twaweza kufikia huko. Waziri haendi kufanya kazi kwa ukanda wake tu bali kwa taifa zima. Hivyo cha kuangalia ni uwezo na uadilifu. Na kama J.K ametumia kigezo hicho cha atokako mtubasi atakuwa kakosea na kupotoka pakubwa.
 
Una hoja ila ni nyepesi. nasema hivi kwa sababu katika uteuzi tukiangalia atokako mtu basi itabidi tuangalie pia kabila lake,dini hata rangi pia twaweza kufikia huko. Waziri haendi kufanya kazi kwa ukanda wake tu bali kwa taifa zima. Hivyo cha kuangalia ni uwezo na uadilifu. Na kama J.K ametumia kigezo hicho cha atokako mtubasi atakuwa kakosea na kupotoka pakubwa.

Mkuu, fanya utafiti usikurupuke. Uwiano wa maeneo ni fakta moja kubwa sanw
 
Hapo JK amecheza, ile clip ilitosha kabisa kumtema kwani alionyesha ukabila uliokithiri... Hata hivyo sidhani kama kutakuwa na jipya kwani Jenister na Zambi ni watu wenye kuendekeza UDINI na ukabila uliopitiliza ...
 
Back
Top Bottom