Its Pancho
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 14,138
- 22,507
Muda mwingine unajiuliza waafrika tumemkosea nini Mungu.?
Lakini ukichimba unakuja kugundua adui yetu wa maendeleo yupo kati kati yetu. Hayuko mbali..!
Mwalimu aliwahi kusema maadui wakuu watatu hapa Tanzania ni.
Umaskini
Ujinga
Maradhi/magonjwa
Nafkiri mwalimu huenda aliangusha miwani yake kidogo wakati anaendelea kutafuta maadui hao watatu.
Alisahau adui mmoja mkubwa na ngumu kumtokomeza
UBINAFSI..
Ndio ni ubinafsi. Adui huyu alianza kuwepo toka enzi za utawala wa machifu.
Mkwawa kwenye historia ni shujaa.
Lakini aliuza wenzake..!
Ndio aliuza wenzake kwa wahindi ili tu apewe kioo,shanga,bunduki..!
Mpka kufikia kwa kina mobutu sese seko..
Namna alivyochukulia madaraka kama silaha kuu ya kulisha tumbo lake kuliko kipimo alichowekewa..!
Ubinafsi...!
Hapa afrika viongozi wanapoomba kura , watashinda na sisi hohe hahe mitaani, watakula na sisi,watalima na sisi..lakini baada ya matokeo na kupata ushindi wanaouita wa kishindo.
Utawaona tu kwenye V8 zao huku tukiamriwa kuwapisha njiani wakubwa wana haraka kuliko sisi kajamba nani..!
Tuna haraka kwani mambo yetu hayana umuhimu kuliko yao ya kuwahi viti virefu baada ya kutoka kula posho za siku kikaoni..!
Tusiwaseme vibosile hata wewe ukipata shavu hilo najua utawaza moyoni wanao wakasome ulaya.mkeo umfungulie biashara..ujenge hekalu kama la mfalme sulemani..!
Huku ukinadi Sera kuwa utawaletea watoto wetu hohehahe madawati na kuwatoa chini ya mwembe wakae darasani..!
Lakini ubinafsi huwa unakuja pale unapopata kitu.
Ukiwa huna unakuwa mmoja wetu. Ukipata sisi sio class yako..!
Dunia hii iko sawa ila watu ndo hatujawahi kuwa sawa.
Kuhubiri na kutenda ni vitu viwli tofauti..!
Tuwe na kiasi.
Pancho boy