Nini furaha ya mwanamke katika ndoa?

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Mwanamke ni mtu muhimu sana katika maisha ya mwanaume. Mwanamke hufanya kazi nyingi za nyumbani kama vile kufua, kuchota maji, kuosha vyombo, kupika na kazi zingine kadha wa kadha japo mwanaume huwa msaada wa baadhi za kazi hizo.

Mwanamke ni pambo la nyumba, uwepo wa mwanamke katika nyumba ni urembo tosha unaofanya nyumba ipendeze na kuvutia watu mbali mbali kuja katika nyumba hiyo namainisha ndugu, majirani na marafiki wa kila namna.

Mwanamke hapendi kudharauliwa, katika ndoa mwanamke anapenda heshima kubwa inayoambatana na kuthaminiwa kwa hali ya juu kama wewe ni mwanaume na unatabia ya kumdharau mke wako, au mpenzi wako ujue unamchukiza na kumkera kwa kiwango cha juu. Mwanamke anapenda heshima.

Furaha ya mwanamke katika ndoa ni Uaminifu. Mwanamke hufurahi zaidi anapoona kuwa mme au mpenzi wake ni mwaminifu, hamsaliti kwa namna yoyote. Niliwahi kushuhudia mwalimu mmoja akimhadithia mwenzake tabia mbaya za mme wake ila akasema anachonifurahisha jambo moja toka niwe naye katika uhusiano sijawahi hata pata shaka naye kama ananisaliti.

Mwanamke anafurahi kujituma kwa mtoto wa kiume, mwanaume usiwe mvivu kubuni mambo tofauti ya kumvutia na kumridhisha mpenzi wako, mwanamke anafurahi kupewa mambo yatakayo mfurahisha na kumfanya awe na hamu ya kuduu na mme wake mara kwa mara. Mapenzi hayana uchafu kwa walio kwenye ndoa.


Mwanke anafurahi kushirikishwa kwa kila jambo la kifamilia na kupewa kipaombele cha kushauri hata kama ushauri wake utakuwa haufai lakin ile kupewa kipaombele cha kushauri na kufanya baadhi ya mamuzi ya familia hujisikia burudni sana. Mke ni Tunu kwa mwanaume.
 
Mkuu mwanamke anapendwa kupendwa na mwanaume ndio anapenda heshima
Bibilia haikukosea juu ya maneno hayo fanya utafiti utagundua
Hata kama humpendi mwanamke ni bora u fake aone kuwa unampenda
 
Back
Top Bottom