Nini Faida ya u fake katika maisha?

Nini Faida ya u fake katika maisha?

timetoloveyourself

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2015
Posts
206
Reaction score
206
Wakuu habarini za jumapili.
Leo napenda kuzungumzia suala la mtu ku pretend na kutaka kuonekana katika jamii kwamba ni mtu fulani smart lakini anachokionyesha yeye hayuko hivo hata kidogo .
Suala hili lipo sana hapa jf na mtaani yamkini. Na huu ufake unapelekwa hadi kwenye mahusiano. Kwanini usiwe wewe halisi? Wapungukiwa nini? Ya nini kujitia mzigo kwa sababu mwisho wa siku hutoweza ku maintain hizo dramas kwa muda mrefu wenye upeo watakuumbua tu.
Kisa kamili. .....
Niliwahi kutafuta rafiki hapa jf na kwa bahati nzuri niliwapata wengi kisha nikafanya uchambuzi yakinifu nikaibuka na mchumba hapa .
Ukaribu wangu na jf ingawa sichangii sana mada nimekuwa msomaji zaidi kutokana na ukulima wangu unaniweka busy sana lakini nimeweza kufahamiana na wadau wengi humu nje ya jukwaa lkn ni members wa jf.
Katika kuwafahamu na kuwasoma nimegundua ufake mwingi sana kwa wanajamii humu ndani. Anyway ni fantasy zao no objection.
Ila kinachonipelekea leo nilete mada ni juu ya wale ma fake kiasi cha kumshirikisha hata Mungu ku justify ubazazi wao. Hapo nawachoka kabisa yaani.
Yaani unamkuta mtu anajipambanua humu ndani kuwa ni bonge la mcha Mungu na anaandika vitu full contents unamwamini kumbe . ...ni chui katika ngozi ya kondoo.
Jamani badilikeni na mbebe uhalisia mnalinajisi jina la Mungu tafadhali. Bora ijulikane kuwa wewe si mlokole kuliko kujifanya mwema mbele za watu ilhali matendo yako hata shetani anakushangaa.
Hii imetokana na kisa halisi kilichonitokea. Kama nilivoanza mwanzo kuwa nilipata rafiki humu ndani ambaye tulianza mahusiano tukiwa na malengo ya kufika hatua ya ndoa. Kimsingi huyu kaka ni anajipambanua humu ndani kuwa mcha Mungu sana na maandiko yake yanajidhihirisha ivo na hata alipokuwa nami amekuwa akijionyesha mwema sana. Ajabu akawa ananambia yeye kukutana na mimi ni Kaonyeshwa na mungu ili nitende nae huduma hapo ndipo nilipoanza kumuundia tume though mwanzo nilimuamini kiaina. Akawa ni mtu mwenye kunishauri sana juu ya uchaji Mungu. Mie nikaanza kuona kweli huyu katumwa kuja kuniokoa coz kiukweli mimi nimekuwa sio msafi kiroho yaani ni mdhambi tu.
Nikaendelea nae ktk hali ya uchumba hivo but alipohitaji nimpeleke home kidogo nikawa mzito sijui sababu. Akanitambulisha kwa rafiki na baadhi ya ndugu zake. Baada ya kama 3months jamaa huyu akarudi US coz anaishi huko na huku alikuja likizo ingawa ana mpango wa kurudi bongo akimaliza masomo yake . Huku akaniachia rasilimali zake kadhaa nizimiliki nami kiroho safi nikachukua maana alizibadilisha hata majina akaweka yangu.
Alipofika Marekani akawa anafanya mchakato niende kule nimfuate nami nikataaa kwakuwa alisema anamalizia masomo atarudi bongo so hakuna haja mie niende badala yake niboreshe hapa home. Akaniambia baba yake ambae ni anafanyia kazi huko na maisha yake kiasi kikubwa amefanya huko amemshauri asiondoke upesi that's why anataka niende. Nikamwambia anipe muda nijipange.
Wakati huo mimi mbali na kumwamini nikawa namfutilia kimya kimya kuanzia kanisani anakoabudu nikawa nimepata contacts za baadhi ya waumini pale, ndugu zake wengine pia nikawa nimepata contacts zao ili niwafukunyue details kadhaa za Bwana kaka. Mimi nina tabia ya ufukunyuku sana
Basi kupitia hizo contacts si ndio nikagundua mkaka kaoa na anaishi na mkewe na ana watoto ingawa kuhusu watoto alishanitonya alidai mama yao alimkimbia. Kumbe mkewe wanaishi pamoja. Nilipogundua nikatafuta muda nikamweleza akakiri ni kweli lkn mke ana matatizo hataki kujirekebisha ivo ameamua kumwacha na ana process divorce. Nikaishiwa nguvu why aniongopee. Nikaanza kumshauri ili asimwache. Akawa haelewi anakomaa tu bwana kamwonyesha mimi. Nikaona huyu analeta drama kwangu. Nikapata namba ya mkewe nikampigia nikijifanya nimekosea namba basi hapo hapo urafiki ukaanza nikaanza kumdodosa uhusiano wake akawa ananieleza yuko poa na mumewe na anampenda sana. Tukaendelea kuwasiliana na mkewe sana hata akanieleza weakness kadhaa za mumewe nami nikawa namshauri sana.
Huku upande wa huyu bwana humu jf na Facebook haonyeshi kama ameoa na humu jf anajifanya anatafuta mke mwema kutoka kwa Bwana daily na anatoa ushauri humu utajua boongeeee la mlokole na mume mwema ukijaaliwa kumpata. Mwenyezi Mungu atuponye nafsi kwakeli tumekuwa wanafiki mbele za watu.
Yaani naandika natetemeka natamani kama nimtaje mumjue na wapo wengi tu humu wameharibu ndoa zao halafu wanajifanya washauri nasaha wakati wanayoongea hawayaishi.
Basi mawasiliano yangu na mkewe yakanifanya nimuonee imani mwanamke mwenzangu kwani hata zile properties alizonipa huyu kaka huku bongo ni efforts za mkewe. Nikajisikia vibaya sana jinsi huyu kaka anavyomlazimisha mkewe amuache kwa visingizio vya kijinga ili tu atimize adhma yake awe na mimi wakti mimi nimeshamjua. Nikawa natafuta namna ya kumpa ukweli. Baadae nikamweleza lakini hakujali ndio akazidisha dharau kwa mkewe. Ikabidi nimpe mkewe ukweli kuhusu mimi na uhusiano wangu na mumewe na niko tayari kutoa ushahidi amweleze tu na mimi siwezi kuwa nae kwakuwa hakunieleza ukweli na kimsingi yuko na mkewe na kwanini awe analitumia jina la Mungu kuniaminisha kuwa yeye ndie mtu sahihi kwangu maana naamini Mungu hawezi fanya double standard.
Basi nikaibua ugomvi mkubwa kwenye ile familia lkn niliahidi full support kwa mke. Mke akahama pale home kwa muda .huyu mume ndio kama karogwa akazidi kujileta kwangu. Nikamblock kwa simu akawa ananitumia pm tu humu jf simjibu niko karibu na mkewe tu.akaenda mahakamani kufungua kesi ya talaka ili amuache mkewe akisisitiza mungu wake kamwonyesha mimi ndie mkewe. Hali ikawa si shwari habari ikawafikia ndugu zao nami nikawa tayari kuwaeleza ukweli.
Talaka haikutolewa hadi sasa ingawa wawili hawa wanaishi nyumba tofauti lakini wewe jamaa naomba uniache na ukizidi kunifuatailia nakutaja humu humu jf na mengine mengi sijayasema unajua.
Halafu fanya toba ya kweli Acha kujionyesha kwa watu humu kuwa wewe unamjua sana Mungu na unawadanganya watu kuwa una mchumba utamuoa wakati huko unaishi na mkeo na hamjaachana sio vizuri unadhalilisha Ukristo aisee.
Jitafakari upya na ujitathmini.
Mkeo anakupenda sana kamuombe msamaha mlee watoto. Hakuna alie mkuu kuliko Mungu utambue. Jiulize tu mwanadamu ni nani hata ajikweze. Umeaibisha ingawa sio issue bali issue kuwa mkweli na mhalisia. Unawezaje kujiita mlokole halafu unafanya ubazazi mkeo yumo ndani eti unanipenda
Najua mihemko tu inakusukuma na ninakuombea pia utambue ulichofanya ili utubu.
Poleni wanajamii mimi si mwandishi mzuri so hata mpangilio sio mzuri ila ujumbe wangu mkuu ni kwa wale pretenders wabadilike jamani halafu tabia zenu za kudhania kwakuwa mko nje ya nchi basi tunawahusudu na viingereza vyenu muache. Sisi tupo hapa bongo na tunawapiga gap sana kimaendeleo. Kuwa nje kuwafanye mtumie fursa vizuri kukwamua familia na taifa sio kujionyesha.
Muwe na vision lol.
Jumapili njema.
 
Ubaya wa uongo haufiki mwisho kila siku unatakiwa upate mbinu mpya ya kuutetea uongo wako

anyway yamenijia majina mawili ya walokole wa humu mmoja lazima awe yeye au anatumia id zote yeye
 
Hukutumia busara kabisa kusambaratisha ndoa ya mwenzio
Mimi tena nimeisambaratisha? Ulitaka niendelee kudanganyika? Ni yeye mwenyewe ametaka kuvunja nami natumia jitihada kadhaa kurudisha. Yeye ndio anataka apewe talaka.
 
Nakuliza tu ushawahi kulala na huyo mume wa mtu?
Nimewahi lala nae na hicho ndicho kilinisukuma kutaka kumjua zaidi.
Halafu ujue haikuwa na haijawa rahisi kwangu coz kiukweli huyu jamaa ni miongoni mwa wanaume walionikaa kumoyo sana lakini kiungwana tu nimemuhurumia mkewe zaidi nahisi nami table inaweza ika turn.
 
ndefuuu kusoma,walio maliza waweke summary bas
 
Nimewahi lala nae na hicho ndicho kilinisukuma kutaka kumjua zaidi.
Halafu ujue haikuwa na haijawa rahisi kwangu coz kiukweli huyu jamaa ni miongoni mwa wanaume walionikaa kumoyo sana lakini kiungwana tu nimemuhurumia mkewe zaidi nahisi nami table inaweza ika turn.
Kosa ulilofanya ni kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzio... ungemuacha kimya kimya bila kuleta uharibifu... huruma yako imesababisha familia kuvurugika, na inawezekana watoto wakapata shida pia...
 
Dah huu uzi umenigusa balaa.inabidi nibadilike kwa kweli. Ngoja nimpende mke wangu hivyo hivyo pamoja na madhaifu yake. Kumbe umenishtakia humu.
 
Kosa ulilofanya ni kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzio... ungemuacha kimya kimya bila kuleta uharibifu... huruma yako imesababisha familia kuvurugika, na inawezekana watoto wakapata shida pia...
Niliamua kufanya kimya kiroho safi lakini jamaa alivozidi kunikomalia na ujue kuna vitu vingi katikati vilitokea. Alivozidi kunikomalia hata kuelekea kumtafutia mwenzie talaka nikaona isiwe shida Acha nidhihirishe ukweli huu. Maana wakati wa mawasiliano yangu na mkewe pia alikuwa akimention uhusiano wangu na mumewe kuwa ni kichochezi. Alikuwa anasema mumewe anwasiliana sana na mwanamke huko bongo na anaomba sana huyo mwanamke ajue ukweli pasipo yeye kujua kuwa huyo mwanamke ni mimi. Nikamjuza jamaa aachane nami ili a Lee family yake hakunielewa.
Better apate mwanamke mwingine na sio mimi.
Amevunja ndoa yake mwenyewe ingawa anaweza kuokoa coz mkewe bado anampenda sana na mimi nikizidi kumkataa jamaa ndipo nairudisha hiyo ndoa though mkaka mlokole anaweza kuwa ana jini mahaba coz si bure uwe tayari kumwacha mkeo just because of mimi Aaahhh
 
Dah huu uzi umenigusa balaa.inabidi nibadilike kwa kweli. Ngoja nimpende mke wangu hivyo hivyo pamoja na madhaifu yake. Kumbe umenishtakia humu.
Badilika kwakweli.
Niache mie nipate mtu fresh ikiwa nitajaaliwa nawe mpende mkeo kwa faida ya watoto wenu
 
Mtenda hutendwa subiria zamu yake ifike uone
Mkuu huyu jamaa king'ang'anizi unadhani ananiachaje sasa. Fikiria hadi nimemleta huku nae ananikomalia tu. Mimi nitawezaje kuwa mwema kuliko mkewe alotoka nae mbali
Pia why atumie jina la Mungu kuniaminisha kuwa yeye ndie mtu sahihi kwangu
 
Mkuu huyu jamaa king'ang'anizi unadhani ananiachaje sasa. Fikiria hadi nimemleta huku nae ananikomalia tu. Mimi nitawezaje kuwa mwema kuliko mkewe alotoka nae mbali
Pia why atumie jina la Mungu kuniaminisha kuwa yeye ndie mtu sahihi kwangu
Mmh haya mambo ni magumu mno kwakweli la msingi tu usije ukajisifu sana mpaka ukakufuru
 
Back
Top Bottom