Nini faida ya matamko?

Dijovisonjn

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
466
125
Kila likitokea jambo lenye hasara kwa jamii furahi, wanaibuka watu, taasisi, vyama n.k kutoa matamko!
Baada ya kifo cha mwandishi wa habari nahisi yameishatolewa matamko zaidi ya mia moja!
Kwa anayefahamu faida za haya matamko, tafadhali naomba anisaidie kunielimisha!
 
Hayana faida. Ni njia tu ya kujulisha jamii kuwa mtoa tamko naye amepata taarifa wa kuwepo kwa hilo tatizo.
 
Matamko yana 'influence' public opinion
na public opinion ina influence utendaji wa serikali....
 
ni kuijulisha jamii kuwa watu wa hiyo kada mfano mwalimu,mwanahabari,doctor n.k, ni jinsi gani walivyokuwa hawana misimamo kwenye maswala yao. hii ni kwasababu matamko yote yanayotolewa na hawa jamaa huwa yanakuwa tofauti na kwenye kuyatekeleza kwake.
 
Matamko yanaonyesha misimamo.

Ukweli kwamba tunahitaji zaidi ya matamko hauondoi umuhimu wa matamko.

Tanzania ishatoa matamko mengi sana kulaani utawala dhalili wa makaburu wa Afrika kusini, lakini hili halikumaanisha kwamba iliishia kwenye matamko.Iliwapa wapiganaji hifadhi na mafunzo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom