Nini chanzo cha kuanzishwa chama cha CHADEMA?

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Wamajamvi Heshima kwenu.

Nina swali dogo tu au pengine linaweza likawa kubwa kulingana na wachangiaji watakavyo jitokeza kuchangia.

Na huenda si mimi peke yangu ninaetaka kufahamu nini chanzo cha kuanzishwa kwa chama cha demokrasia na maendeleo?

kwa nijuavyo mimi baadhi ya viongozi walionzisha chama hiki walitokea NCCR Mageuzi, lakini sina uelewa wa nini kilitokea mpaka wakajitoa NCCR Mageuzi Na kuanzisha Chama cha CHADEMA.

Naomba mtusaidie historia hii mzuri ya vyama hivi viwili.
 
Kilitokana na Wafanyabiashara wa Kichaga. Yaani Chagga Development Manifestor. Lengo lilikuwa kulinda Masilahi ya Wafanyabiashara. Baadaye Mtei na akina Ndesambulo wakaona kiwe chama cha Kisiasa na kubadili jina kuwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, ili kupanua Wigo wa Mapato zaidi.

Mwenye hoja nje na hizi aseme ukuntu wa hiyo hoja.
 
Lengo kuu la Chadema ni Kutetea Demokrasia na kuleta Maendeleo. Si kweli viongozi wote wa Chadema walitoka NCCR. Zitto, Dr Slaa etc hawajawahi kuwa wanachama wa NCCR
ila Slaa ni mwanachama hai wa vyama viwili vya siasa
 
Wamajamvi Heshima kwenu.

ninaswali dogo tu au pengine linaweza likawa kubwa kulingana na wachangiaji watakavyo jitokeza kuchangia.

Na huenda si mimi pekeyangu ninaetaka kufahamu nini chanzo cha kuanzishwa kwa chama cha demokrasia na maendeleo?

kwa nijuavyo mimi viongozi karibu wote wa chama hiki walitokea NCCR Magezi, lakini sina uelewa wa nini kilitokea mpaka waka jitoa NCCR Mageuzi Na kuanzisha Chama cha CHADEMA.

Naomba mtusaidia histiria hii mzuri ya vyama hivi viwili.

PISTO LERO,
Sio kweli kluwa viongozi wote wa Chadema wanatokea NCCR-Mageuzi. Kwa sababu hiyo mada yako haikufanyiwa utafiti wa kutosha na inaweza ikawa na upotoshaji wa makusudi!
 
Ni vichwa vigumu na butu tu ambavyo havina historia ya cdm. Nenda msajili wa vyama utapata maana na nani waanzilishi maana hata hoja haina sio tu kichwa hata mkia hivyo haiwezi jadiliwa na wenye uelewa.
 
Kilitokana na Wafanyabiashara wa Kichaga. Yaani Chagga Development Manifestor. Lengo lilikuwa kulinda Masilahi ya Wafanyabiashara. Baadaye Mtei na akina Ndesambulo wakaona kiwe chama cha Kisiasa na kubadili jina kuwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, ili kupanua Wigo wa Mapato zaidi.

Mwenye hoja nje na hizi aseme ukuntu wa hiyo hoja.
Waanzilishi wa CHADEMA ni hawa hapa nani chama cha kisiasa hakikuwahi kubadilishwa.
Edwin Mtei (Arusha),
Makani (Shinyanga),
Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
Edward Barongo (Kagera),
Mary Kabigi (Mbeya),
Menrad Mtungi (Kagera),
Costa Shinganya (Kigoma),
Evalist Maembe (Morogoro) na
Steven Wassira (Mara)
Ficha upumbavu wako
 
PISTO LERO,
Sio kweli kluwa viongozi wote wa Chadema wanatokea NCCR-Mageuzi. Kwa sababu hiyo mada yako haikufanyiwa utafiti wa kutosha na inaweza ikawa na upotoshaji wa makusudi!

Asante: ila ndiya sababu nikaomba kujua nini kilitokea.
 
Asante ndugu kwa kuweka majina ya waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na mahali anapotoka kila mmoja wao. Kuna watu wanapenda kutoa tafsiri na tuhuma zisizo za msingi eti CHADEMA ni chama cha kikanda, kikabila, kiukoo, nk. ili mradi tu wakivuruge chama kipenzi cha watanzania walio wengi. Kwa ufafanuzi huo ulioutoa naamini hakutakuwa na ubishi tena, na kama yupo atakayeendelea kuhoji juu ya uanzishwaji wa chama hiki basi tutakuwa na walakini juu ya uelewa wa mtu huyo.
 
Kueneza Demokrasia yenye kumkomboa mtanzania mnyonge kutoka katika wimbi la umaskini uliosababishwa na CCM!
 
Waanzilishi wa CHADEMA ni hawa hapa nani chama cha kisiasa hakikuwahi kubadilishwa.
Edwin Mtei (Arusha),
Makani (Shinyanga),
Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
Edward Barongo (Kagera),
Mary Kabigi (Mbeya),
Menrad Mtungi (Kagera),
Costa Shinganya (Kigoma),
Evalist Maembe (Morogoro) na
Steven Wassira (Mara)
Ficha upumbavu wako
Kumbe Wassira nae ni mmojawapo wa waanzilishi wa CDM?
 
Kilitokana na Wafanyabiashara wa Kichaga. Yaani Chagga Development Manifestor. Lengo lilikuwa kulinda Masilahi ya Wafanyabiashara. Baadaye Mtei na akina Ndesambulo wakaona kiwe chama cha Kisiasa na kubadili jina kuwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, ili kupanua Wigo wa Mapato zaidi.

Mwenye hoja nje na hizi aseme ukuntu wa hiyo hoja.

Upuuzi mtupu.
 
Je? Ni wasira huyu aliyeko ccm kwa sasd au ni wasira baba yake esta.
 
Tatizo lenu ni kukariri badala ya kutafakari kwa kina kabla hujaanza comment chochote afterall sio lazima kuwa kwenye huu uzi..... Soma katiba za vyama hivi CDM na CCM utajua nini unasema.
 
Waanzilishi wa CHADEMA ni hawa hapa nani chama cha kisiasa hakikuwahi kubadilishwa.
Edwin Mtei (Arusha),
Makani (Shinyanga),
Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
Edward Barongo (Kagera),
Mary Kabigi (Mbeya),
Menrad Mtungi (Kagera),
Costa Shinganya (Kigoma),
Evalist Maembe (Morogoro) na
Steven Wassira (Mara)
Ficha upumbavu wako

CC Ritz
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom