Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 40,022
- 51,164
Ningeshituka na kufarijika na kuona kweli demokrasia imekua hapa nchini kama nyomi kama wanavyodai, lililoletwa na Bw. lowasa Lingekua limeletwa na Mbowe ama Slaa.
Lakini Kwakua wingi wa watu kama tunavyoona, umeletwa na aliyekuwapo katika siasa za CCM kwa miaka zaidi ya 30, sina shaka kusema kwamba, Siasa za Tanzania bado ni ya viwango vya chini mno, na demokrasia bado haijakua kabisa.
Anayejaza mikutano ya CHADEMA ni aliyejiondoa CCM, hivyo basi wanakwenda kumwangalia kwa mantiki moja tu ya kuhakikisha kama kweli kahama. Lakini haina maana kuwa watampigia kura, hilo ni swala lingine ambalo linahitaji mjadala wakati mwingine.
Nahitimisha kwa kusema kwamba, bado Tanzania inayo mengi ya kuyafanya na kujifunza kabla ya kufikia siasa safi yenye viwango vya daraja la juu vinavyokubalika kidemokrasia.
Uliopo ni ushabiki ambao kimtazamo una madhara yake tusipokua makini. Mabadiliko yanayokubalika ni yale yanayofuata kanuni na miiko, sio katika dhana ya kulazimisha na ushabiki.