Ningependa tanzania ya hivi!

Nenetwa

Member
Jan 16, 2011
14
0
NINGEPENDA TANZANIA YA HIVI: Elimu bora, makazi bora, miundombinu bora, huduma bora za afya, fursa nyingi za ajira za kuajiriwa na kujiajiri, viongozi waadilifu, Uzalishaji viwandani na kuuza nje kwa wingi. Wastani wa miaka mingi ya kuishi (High life expectancy). Je wewe Ndugu yangu Mzalendo Mtanzania unapenda Tanzania ya namna gani? Changia mawazo.
 
Hii Tanzania ninayoitaka, Itafikiwa hivi: FURSA SAWA KWA ELIMU BORA YENYE KUMPATIA MHITIMU MABADILIKO ENDELEVU YA KUDUMU KATIKA NGAZI(DOMAINS) ZOTE ZA MAARIFA, UJUZI, STADI NA MIELEKEO/MAADILI/TABIA ILI AWEZE KUITUMIA ELIMU HIYO KATIKA KUYAMUDU MAISHA NA MAZINGIRA YAKE. KAMA LENGO HILI KUU LA ELIMU LITATEKELEZWA KWA UBORA NA VIWANGO, BASI MENGINE YOTE NILIYOYATAJA YATAKUWA ZAO LA ELIMU. Kumbuka inatubidi kuanza na wazo, kuweka nia, kuwa na matumaini, kuamini kuwa inawezekana, na kujiamini sisi wenyewe kuwa tunaweza! Tuanze sasa,tuanze leo. TUSISAHAU KUWAKEMEA NA KUWAWAJIBISHA MAFISADI NA VIONGOZI WABABAISHAJI. Mabadiliko ya kweli Tanzania, yanawezekana.
 
Back
Top Bottom