Zabron Hamis
JF-Expert Member
- Dec 19, 2016
- 6,843
- 10,899
Habari wana JF, Heri ya Chritmas&Mwaka mpya. Mwenyezi Mungu atupe ruksa ya kuuona mwaka ujao 2017 ambao utatujia hivi punde.
Najitokeza ikiwa ni mara yangu ya kwanza kuandika thread hapa katika jukwaa la wanajamii wenzangu.
Kilichonifanya kuandika uzi huu ni hatua ya kila unapouguliwa na ndg, jamaa ama rafiki na kumpeleka katika hospitali yoyote iwe ya wilaya au mkoa na kukuta ameishiwa ama ana upungufu wa damu, ni lazima ajitokeze mtu wa kumtolea damu. Maranyingi kuna watu wanaotoka benki ya damu ni wataalamu wa lugha ya kubembeleza (Kushawishi, kusihi) pale wanapopita katika taasisi na sehemu nyinginezo. (Binafsi nilishawahi kutoa damu mara moja baada ya hawa watu kutembelea katika shule niliyokuwa nikisoma, na huenda mpo wengine pia). Watu hupimwa na wale wanaokidhi vigezo na masharti, hutoa damu. Ajabu ni kuwa sikuwahi wala sijawahi kusikia au kuona mtu akiongezwa damu kabla ya ndg yake kujitolea.
Kwanijuavyo mimi (kama sivyo naomba kuelimishwa) ni kua damu inayotolewa hospitali kwaajili ya kumuongezea mtu haiendi moja kwa moja kwa mgonjwa hadi vipimo vya kitabibu vizingatiwe na kuonekana damu iliyotolewa haina dosari ndipo hua tayari kwa matumizi. Hii ikiwa na maana kua anapotokea mtu damu zenu zinamatch hawawezi kutoa damu na kumuongezea mgonjwa papo hapo. Sasa swali langu ni, DAMU AMBAYO INAHIFADHIWA BENKI YA DAMU KARIBU KATIKA KILA HOSPITALI KUBWA NI YA NINI? KAMA HUTUMIKA, HUTUMIKA WAKATI GANI NA KWAKINA NANI? KWANII USIWEPO UTARATIBU WA KUMUONGEZA MGONJWA ILI KUOKOA MAISHA WAKATI TARATIBU NYINGINE ZIKIFUATA? naamini hapa sitatoka kapa hata kidogo