Ningependa kufahamu, hivi damu ambayo watu huchangia inatumiwaje?

Zabron Hamis

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
6,510
10,415
Habari wana JF, Heri ya Chritmas&Mwaka mpya. Mwenyezi Mungu atupe ruksa ya kuuona mwaka ujao 2017 ambao utatujia hivi punde.

Najitokeza ikiwa ni mara yangu ya kwanza kuandika thread hapa katika jukwaa la wanajamii wenzangu.

Kilichonifanya kuandika uzi huu ni hatua ya kila unapouguliwa na ndg, jamaa ama rafiki na kumpeleka katika hospitali yoyote iwe ya wilaya au mkoa na kukuta ameishiwa ama ana upungufu wa damu, ni lazima ajitokeze mtu wa kumtolea damu. Maranyingi kuna watu wanaotoka benki ya damu ni wataalamu wa lugha ya kubembeleza (Kushawishi, kusihi) pale wanapopita katika taasisi na sehemu nyinginezo. (Binafsi nilishawahi kutoa damu mara moja baada ya hawa watu kutembelea katika shule niliyokuwa nikisoma, na huenda mpo wengine pia). Watu hupimwa na wale wanaokidhi vigezo na masharti, hutoa damu. Ajabu ni kuwa sikuwahi wala sijawahi kusikia au kuona mtu akiongezwa damu kabla ya ndg yake kujitolea.

Kwanijuavyo mimi (kama sivyo naomba kuelimishwa) ni kua damu inayotolewa hospitali kwaajili ya kumuongezea mtu haiendi moja kwa moja kwa mgonjwa hadi vipimo vya kitabibu vizingatiwe na kuonekana damu iliyotolewa haina dosari ndipo hua tayari kwa matumizi. Hii ikiwa na maana kua anapotokea mtu damu zenu zinamatch hawawezi kutoa damu na kumuongezea mgonjwa papo hapo. Sasa swali langu ni, DAMU AMBAYO INAHIFADHIWA BENKI YA DAMU KARIBU KATIKA KILA HOSPITALI KUBWA NI YA NINI? KAMA HUTUMIKA, HUTUMIKA WAKATI GANI NA KWAKINA NANI? KWANII USIWEPO UTARATIBU WA KUMUONGEZA MGONJWA ILI KUOKOA MAISHA WAKATI TARATIBU NYINGINE ZIKIFUATA? naamini hapa sitatoka kapa hata kidogo
 
Kwa utaratibu wa sasa kila hospital ya Wilaya,mkoa rufaa na zingine lazima zichukue damu kutoka Benki ya damu salama kwa matumizi ya hospital husika lakini kwa masharti kuwa ndugu lazima wareplace damu iliyotumika.

Na mahitaji ya damu ktk hospital zote Tanzania ni makubwa kupita stock ya damu iliyopo Benki ya damu.

Kwa dharura na kama damu IPO mgonjwa lazima awekewe tu ila kama hakuna damu ndipo ndugu mtaambiwa mtoe damu.
 
Sasa kwanini inakua kama PF3, lazima itolewe kwanza ndipo mgonjwa atibiwe, kwanini isitolewe wakati matibabu yanaendelea. (Hapa ni kwazile hospitali zenye stock ya damu)
 
Kuna mambo hayaelezeki.yaani hata aliyeshauri lifanyike hivyo pia hajui ni kwanini aliona iwe hivyo.
 
Swali zuri sana.!!
Majibu.
Damu tunayo ikusanya kwenye mashule ama mahali popote pale ni kwa ajili ya kusaidia makundi kama wanaojifungua,majeruh,watoto, na watu mbalimbali wenye magonjwa yenye kuhitaj damu au operation. Tukija kwenye hoja yako ya "kwa nin mgonjwa hapew damu mpaka ndugu waje kufanya replacement..? Jibu ni kwamba tuna pendekeza kufanya hivyo ili kuhakikisha kuwa bank za damu hazipungukiw na damu hata kidog. Ingawa hoja ni kuwa endapo ndugu wakikosekana au ndugu group lake likionekana haliendani na mgonjwa bas huwa wajibu wetu tutampa mgonjwa damu ili tuokoe maisha yake. Kwa hiyo ndug yang hayo ndo majib na majawabu. Naomba kuwasilisha
 
Sasa kwanini inakua kama PF3, lazima itolewe kwanza ndipo mgonjwa atibiwe, kwanini isitolewe wakati matibabu yanaendelea. (Hapa ni kwazile hospitali zenye stock ya damu)
Damu ni dharura haitaji kutolewa kwanza ndiyo iwekwe.Kulazimishwa kutoa ni ili replacement ifanyike
 
Swali zuri sana.!!
Majibu.
Damu tunayo ikusanya kwenye mashule ama mahali popote pale ni kwa ajili ya kusaidia makundi kama wanaojifungua,majeruh,watoto, na watu mbalimbali wenye magonjwa yenye kuhitaj damu au operation. Tukija kwenye hoja yako ya "kwa nin mgonjwa hapew damu mpaka ndugu waje kufanya replacement..? Jibu ni kwamba tuna pendekeza kufanya hivyo ili kuhakikisha kuwa bank za damu hazipungukiw na damu hata kidog. Ingawa hoja ni kuwa endapo ndugu wakikosekana au ndugu group lake likionekana haliendani na mgonjwa bas huwa wajibu wetu tutampa mgonjwa damu ili tuokoe maisha yake. Kwa hiyo ndug yang hayo ndo majib na majawabu. Naomba kuwasilisha
bado kidogo. mbona kuna watu wanakufa kwasababu hakuna damu
 
Kwa utaratibu wa sasa kila hospital ya Wilaya,mkoa rufaa na zingine lazima zichukue damu kutoka Benki ya damu salama kwa matumizi ya hospital husika lakini kwa masharti kuwa ndugu lazima wareplace damu iliyotumika.

Na mahitaji ya damu ktk hospital zote Tanzania ni makubwa kupita stock ya damu iliyopo Benki ya damu.

Kwa dharura na kama damu IPO mgonjwa lazima awekewe tu ila kama hakuna damu ndipo ndugu mtaambiwa mtoe damu.
Kwahiyo benki ya damu Kuna muda inafilisika?
 
Back
Top Bottom