Elections 2010 Ningependa Dr Slaa atoe ahadi hizi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Ningependa Dr Slaa atoe ahadi hizi:

1. Akiingia madarakani fedha zote za mapato yote ya serikali zitokanazo na madini ya nchi hii zitumike katika kusomesha watoto wa nchi hii -- kuanzia primary hadi university level. Ni urithi wao kutoka kwa Mungu Mwenyezi, na siyo urithi wa wajanja wachache wakishirikana na watu wa nje.

2. Mali zote zilizochumwa na CCM kutokana na nguvu za wananchi wote wakati wa utawala wa chama kimoja zitaifishwe.

3. Wanaopatikana na hatia ya rushwa kuanzia ile ya Sh milioni 5 na kundelea wafungwe si chini ya miaka 30. Hukumu hii iwe sawasawa na ile ya majambazi watumiao nguvu au wale wanaotuhumiwa kubaka.

4. Mishahara yote ya watumishi wa umma, kuanzia Rais kwenda chini hadi mhudumu ofisi iwekwe wazi kwa wananchi wote kuijua -- kama vile ilivyo Marekani na nchi nyingine zilizoendelea. Kuna siri gani katika hili?

5......

6......

7.....

Ongezeni orodha hiyo wadau.
 
Mafisadi wote walikwapua mapesa yetu warudishe mapesa yetu na wao wanyongwe ama wapigwe risasi.
 
Mkubwa nafikiri suala siyo kutoa ahadi, ila ni jinsi gani atazitekeleza ahadi hizo?????
 
5. Apige marufuku matumizi ya magari ya kifahari na ambayo uendeshaji wake ni gharama kubwa katika ofisi za kawaida (ila tu mawaziri na raisi)
6. Apige marufuku semina na makongamano yote yasiyo ya lazima yanayogharamiwa na ofisi za serikali
7. Aondoe urasimu katika ofisi za umma kama vile uhamiaji, kwa wakurugenzi wa wilaya, kwa wakuu wa wilaya n.k
8. Arekebishe mashirika ya pensheni na kuyafanya yatoe rate sawa na kusiwe na urasimu wala usumbufu wakati wa kufuatilia mafao...
9. Ahakikishe zinatengezwa master plans za maendelezo ya miji yote Tanzania, zikizingatia miundombinu muhimu kama barabara na maji...
10. Aweke ufuatiliaji wa karibu katika taasisi za umma kama vile mahospitalini na kuhakikisha rushwa na urasimu vinapunguzwa au kukomeshwa...
11. Atengeneze mifereji na mabwawa makubwa kutoka mito yetu tuliyo nayo yatakayowezesha kupatikana maji kwa matumizi ya kibinadamu na kilimo
12. Afungue mashamba makubwa ya kisasa ya mazao mbalimbali na kuyakodisha kwa wananchi kwa riba nafuu na condition wazi za kima cha uzalishaji
13.
14.
 
13. Atoe waraka kuwa miradi yeyote ya serikali itakayogharimu zaidi ya tsh mil 100 ipate baraka kutoka ikulu na mchakato wake uwe wazi...
 
Mimi sidhani kama kuna haja ya ahadi kuna vitu vingi vyenye matatizo na vyamuhimu. Hivyo aonyeshe priorities zake ambazo zitatatua matatizo mojakwamoja. Maana we have to solve these problems from the root.
 
Back
Top Bottom