muafi
JF-Expert Member
- Oct 6, 2015
- 2,115
- 4,801
Kitu kinachopelekea Tanzania tunakuwa nyuma kiteknolojia na kimaendeleo ni kuvipa vyeti kipaumbele kuliko ujuzi binafsi.
Mitaani kuna njemba zina fani na akili vibaya mno, kuna mtu nilimshuhudia katengeneza redio mtaani kwake yaani ilikuwa inasikika maeneo ya mtaani kwake na mitaa ya jirani, jamaa alibuni tu kwa kutumia vifaa vyake vya kawaida tu wala sio vile vya kutoka kwa mabeberu, lakini jamaa alipoanza kupata umaarufu hakuchukua raundi serikali wakamvaa na huo ukawa mwisho wake.
Nilimsikia jamaa mwingine nahisi kati ya Shinyanga au Singida yeye alikuwa ni mtaalamu wa kutengeneza mabomu, jamaa alikuwa anatengeneza mabomu yeye mwenyewe na yanalipiua kweli kweli baada ya kugundulika jamaa hakuchukua raundi baada ya kuendelezwa au hata kuajiriwa kwenye majeshi yetu alipewa zawadi ya kuwekwa ndani nadhani mpaka leo ananyea debe.
Kuna watu mitaani wanajua vitu vingi sana, wapo wanaozalisha umeme. Wapo wenye teknolojia mbalimbali lakini kwakuwa hawana vyeti wameishia kubaki hivyo hivyo walivyo.
Kwa tulipofikia hivi sasa tunapaswa hata silaha za jeshi tutengeneze wenyewe mimi ninaamini inawezekana, kuna njemba ziko mtaani zikiwezeshwa zinaweza kufanya hivyo vitu.
Matokeo yake watu wanaenda kuuza teknolojia nchi za nje, kuna jamaa wa Kigoma aliuza teknolojia ya majiko yanayotumia betri kwa wachina.
Mwingine naye kauza teknolojia ya kulipia gesi kwa UK.
Kuna watu wana Degree na Masters lakini hawana impact yoyote serikalini zaidi ya kula na kunywa tu.
Kuna watu wana uwezo mkubwa sana lakini hawaangaliwi, majeshi yetu pia yanahitaji watu wenye teknolojia kuna watu mtaani wanateknolojia za hali ya juu ni wadukuzi waliobobea, wapo watu wana uwezo wa kutengeneza silaha kiasi kwamba wakipewa sapoti tu wataikuza teknolojia kwenda viwango vingine lakini ndio hivyo wakikamatwa mwisho wao ni kunyea debe.
Mimi nafikiri sasa hivi tuangalie na wale wenye vipaji tuwasapoti kuliko kuangalia vyeti tu visivyo na tija.
Magenius tunao tuwape sapoti!
Unadegree nne tukikuuliza taifa umeshalifanyia nini huna cha kujibu, kwanini nisitafute la saba anayeweza kuniletea teknolojia mpya nikamuendeleza kwa faida ya taifa?
Waafrika tuache ushamba hata mabeberu huwa wanawathamini sana watu wenye vipaji binafsi!