Ningekuwa na Mamlaka, ningepiga marufuku uvutaji/uuzaji wa sigara aina zote

Benylin

Member
Feb 9, 2017
44
26
Onyo uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako. Hiyo sentensi ni dhahiri kuwa hupatikana kwenye package ya sigara mbalimbali ikiwa imeandikwa kwa herufu ndogo saana.

Imefikia hatua, katika jitihada za kupambana na madawa ya kulevya, ningependa kuishauri mamlaka husika pia kuliangalia swala LA uvutaji sigara aina zote nchini.

Vijana wengi wanaangamia kwa matumizi ya sigara hizi, kwa kujikuta baada ya utumiaji wq mda mrefu , mapafu(Lungs) hudhoofika na hatimae kushindwa kufanya kazi yake ya Upumuaji vizuri.

Imekua kawaida kukutana na Mtu anavuta sigara barabarani, bila hata kujali uelekeo wa upepo/moshi wa sigara, kiasi cha kuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Pamoja na hayo, imefikia hatua utoaji wa elimu tu ya madhara ya uvutaji wa sigara haitoshi, jitihada za kuzuia uzalishaji na uuzaji wake zinapaswa kufanyika ili kuokoa kizazi kinacho athirika na matumizi ya sigara aina zote, pasipo kujali kodi inayolipwa kutokana na Bidhaa hii.

Kwani kwa kuzuia uzalishaji wake, watumiaji hawatakuwa na fursa ya kuzipata Sehemu yoyote ile, na hivyo watalazimika kuziacha kwa coz of no alternative, na kwa namna hii watakua wamesaidiwa kuepukana na madhara ya kuharibu Mapafu kwa uvutaji wa sigara.

Benylin M.

Nawasilisha hoja
 
Ulisikia wapi kuwa mtu kafa kwa kuvuta sigara ila bado unaendekeza umalaya ambao unaweza kukusababishia ukimwi

Hivi unataka kuniambia hujui madhara ya kuvuta sigara?Baba yangu mzazi baada ya miaka mingi ya kuvuta sigara hatimaye alikufa kwa ugonjwa wa mapafu uliosababishwa na uvutaji wa sigara.Google "The side effects of cigarette smoking" upate taarifa kamili.
 
Very ignorant. Hivi unataka kuniambia hujui madhara ya kuvuta sigara?Baba yangu mzazi baada ya miaka mingi ya kuvuta sigara hatimaye alikufa kwa ugonjwa wa mapafu uliosababishwa na uvutaji wa sigara.Google "The side effects of cigarette smoking" upate taarifa kamili.
Kwahiyo asingevuta sigara asingekufa?
 
Mbona hutaji waliofanya umalaya kama wewe walivokufa kwa ukimwi
 
Ulisikia wapi kuwa mtu kafa kwa kuvuta sigara ila bado unaendekeza umalaya ambao unaweza kukusababishia ukimwi
We pia ni mtumiaji? Watumiaji wa sigara wote huwa nawashangaa sana
Very ignorant. Hivi unataka kuniambia hujui madhara ya kuvuta sigara?Baba yangu mzazi baada ya miaka mingi ya kuvuta sigara hatimaye alikufa kwa ugonjwa wa mapafu uliosababishwa na uvutaji wa sigara.Google "The side effects of cigarette smoking" upate taarifa kamili.
 
New Zealand walianzisha kuprint packet za sigara (plain) na kuweka onyo tu, hazina rangi mbalimbali za kuwavutia watoto.

Nchi nyingi zimeiga lakini walioenda mbali zaidi ni Australia ambao bei ya sigara kwa pack ni ghali duniani ($13) na mwezi wa September 2016 imepita sheria kuwa mwaka 2020 bei itapanda mpaka kufikia $40 kwa packet.

Wavutaji wengi wameacha na kuingiza contraband wamedhibiti sana huko
Nafikiri to damage the pocket is the best option if you know what I mean
 
Onyo uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako. Hiyo sentensi ni dhahiri kuwa hupatikana kwenye package ya sigara mbalimbali ikiwa imeandikwa kwa herufu ndogo saana.

Imefikia hatua, katika jitihada za kupambana na madawa ya kulevya, ningependa kuishauri mamlaka husika pia kuliangalia swala LA uvutaji sigara aina zote nchini.

Vijana wengi wanaangamia kwa matumizi ya sigara hizi, kwa kujikuta baada ya utumiaji wq mda mrefu , mapafu(Lungs) hudhoofika na hatimae kushindwa kufanya kazi yake ya Upumuaji vizuri.

Imekua kawaida kukutana na Mtu anavuta sigara barabarani, bila hata kujali uelekeo wa upepo/moshi wa sigara, kiasi cha kuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Pamoja na hayo, imefikia hatua utoaji wa elimu tu ya madhara ya uvutaji wa sigara haitoshi, jitihada za kuzuia uzalishaji na uuzaji wake zinapaswa kufanyika ili kuokoa kizazi kinacho athirika na matumizi ya sigara aina zote, pasipo kujali kodi inayolipwa kutokana na Bidhaa hii.

Kwani kwa kuzuia uzalishaji wake, watumiaji hawatakuwa na fursa ya kuzipata Sehemu yoyote ile, na hivyo watalazimika kuziacha kwa coz of no alternative, na kwa namna hii watakua wamesaidiwa kuepukana na madhara ya kuharibu Mapafu kwa uvutaji wa sigara.

Benylin M.

Nawasilisha hoja
Nikweli lakini
Kilimo cha tumbaku Tabora hiyo inajulika sana na mpaka viwanda vyake vpo , wasema nimmoja ya zao linalo ingizia Taifa pato kubwa! Kama Rais JPM atasema heeeee! Bunge litalipuka wakat wowote, wafanyabiashara watalia na yeye, kuzuia hiyo haiwezekani kabisa, mwenye kuogopa madhara ataacha asyeogopa hewala
Hataka wengine siku hiz wanachabganya na bang
 
wee piga hiyo 'marufuku yako' ila kama unatufa vita iguse ile sigara nyingine ilee a.k.a 'mmea wa kondeni' ule ulio kuepo tangu enzi ya manabii,
 
Mie naunga mkono ikiwa kweli tunataka nchi iwe sober na tunataka iwe sober, tupambanapo na madawa ya kulevya, shisha, bangi, mirungi na sigareti tukaacha itakuwa fedheha sana eti kwa kuwa serikali ianapata kodi na Tabora inalimwa tumbaku.

Ikiwa kweli hawa walioko mbele wanataka hii idea ya nchi na taifa kuwa sober basi hata sigareti hatutaki eti kwa kuwa wanalipa kodi, hatutaki kodi zinazogharimu mapafu ya watanzania na kuligharimu taifa mabilioni ya fedha kwenye matibabu ya saratani, nguvu kazi, kudhoofisha afya, uchafuzi wa mazingira, nk.

Sigareti iwe miongoni mwa vile vinavyoadhiri afya na akili za watanzania la sivyo hata unga waandike utumiaji wa cocaine ni hatari kwa afya yako tuone kama italeta akili. Ban them all na tusiwe na double standards.

Napongeza sana juhudi za kupambana na madawa ya kulevya na zaidi ikiwa ingejumuisha vita dhidi ya sigareti zote nchini. Tunataka viwanda lakini tupitie tulivyonavyo ikiwa kweli tunavihitaji karne hii na kama tumebaini mathalan sigareti, shisha hatutaki funga viwanda na biashara hizo na tutengeneze vyanzo vya kodi vinavyoleta akili na sio pombe, sigareti etc. zinazogharimu afya za walaji. TBS mpo???
 
Kwahiyo asingevuta sigara asingekufa?
Mkuu ni sawa sawa na mtu kunywa sumu huwa inawahi kumuondoa mtu duniani mapema ndo kma hvyo madhara yatokanayo na sigara ni sawa na kunywa sumu maana unakuwa unajisogeza karibu na kifo..
 
Back
Top Bottom