nInGeKuWa MiMi (TRAFKI) niNgEjInYoNgA mBeLe Ya KoVA

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,687
4,071
Jamaa kasimamishwa na
trafiki yuko hai spidi
mwanawani. Sasa ona
maongezi: Trafiki: Unajua kuendesha
kasi kiasi hicho ni kosa la
jinai? Jamaa: Najua lakini wala
sijali, kwani we unatakaje? Trafiki: Khaa, hebu nipe
kadi yako ya gari. Jamaa: Kadi sina, kwanza
hili gari nimeliiba muda is
mrefu. Trafiki: Unasema?! Kwa
hiyo wewe ni jambazi na
inaelekea unatumia silaha! Jamaa: Sio silaha nyingi,
Shoti Gani, AK47, risasi mia
300 na mabomu machache
ya kutupa kwa mkono. Pia
nina kiroba cha bangi. Trafiki: Leo umekwenda na
maji mwanaharamu wewe.
Fungua buti la gari nikague. Jamaa: Sitaki, kuna vichwa
20 ya watu kwenye buti
kwa ajili ya kutoa sadaka.
Na kuna watu wawili
nimewaua naenda
kuwatupa, pia wako humo kwenye buti. Trafiki: Mungu wangu!!!!!!
Hai spidi, gari umeiba,
unamiliki silaha, muuaji, leo
ndo mwisho wako. Afande kakamata simu
kampigia Ze Bigi Bosi Kova
mwanawane. Ngrriiiiiiiiiiiiiii.
Afande nimekamata
jambazi sugu ana vichwa 20
vya binadamu, kaiba gari, kaua, ana silaha na madawa
ya kulevya. Mwanawane madifenda
hayo na Kova ndani
vyuuuuuupu eneo la tukio. Kova: Fungua buti
usachiwe. Jamaa akafungua. Kova:
Mbona hamna vichwa wala
hamna hao watu, wala
madawa? Jamaa: Afande Kova, mimi
hata nashindwa kuelewa
askari wetu siku hizi
wamekuwaje. Hapo nahisi
atakuwa pia
amekudanganya kwamba nina silaha na nilikuwa hai
spidi. Ndo kawaida
kutubambikia.! Mwanawane, jamaa
huyooooooo akaachiwa
asepe zake!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom