Mkuu Kyafulili, tangu mwanzo nimekuunga mkono bandiko lako kwa humility ulioonyesha, ila kuna jambo moja muhimu sana nimeligiundua kwako hapo mwanzo nililiover look!.
Unakubaliana na maamuzi ya CC ya Chadema, they did the right thing, Kitila ni mkosaji aliyestahili adhabu ile!. Huu nao mimi nauita ni upofu uliosababishwa na mahaba makubwa kwa Chadema!.
Kitila ni an academician, ule waraka ni an academic paper ya regime change through "a winning coalition" through the normal electoral process ya ndani ya chana!, hakuna uhaini wowote pale wall hakuna mapinduzi yoyote pale!, it was a regime change only!.
Masikini CC ya Chadema imejaa vilaza wengi zaidi kuliko wasomi!, na baadhi ya wasomi wenu ni wasomi wa divinity, kwao mawazo yoyote tofauti yanatafsiriwa kama uasi, hivyo nao hawakuweza kuona "the motive behind" waraka ule, wakaishia kuuita uhaini na kutoa hukumu iliyopaswakwa wahaini!.
Kitendo cha Kitila kuomba msamaha, ni kukubaliana na upuuzi wa CC ya Chadema!. Nilisema watu wenye sense kama wewe ndio wangeweza kuokoa Chadema kwa CC kujitathmini, na kurudi kumomba msamaha Kitila kwa kumsingizia uhaini!. Kwa vile ni vigumu sana baba kumuomba msamaha mtoto aliyemuadhibu kwa makosa, baba atajisikia kuwa mdogo kama piriton, the African way ni baba kwenda kwa babu, (baraza Kuu), na kumueleza babu, nimemkosea mtoto!, Babu ndie atamuita mtoto, na kumweleza shetani alimpitia baba na kufanya yasiyo paswa, yule ni baba yako, anakupenda ndio maana alikudhibu kwa makosa, amejuta, msamehe, muheshimu, mtashikana mikono na baba, mtasameheana, mtakumbatiana na maisha yatasonga mbele!.
Sijawahi kuipitia CV ya Kitila, ila ukimsoma, utajiridhisha jamaa ana very high IQ, ni level ya kina Beregu, Safari, Mnyika etc. Akifuatilia arguments za wengi wa viongozi wenu wana ordinary IQ na wengine low IQ, hivyo kitendo cha kumpoteza kitila, hawa ordinary na low IQ wanaona poa, kwa sababu kwao Kitila was just a person tuu kama alivyo Sugu au kiongozi mwingine yoyote!, wale wenye high IQ wanaumia kwa sababu kumpoteza Kitila kwao sio issue, kwao issue ni kuipoteza ile "the best brain", hivyo Chadema ku suffer "brain drain", naamini hapa unanielewa!. Kwa Chadema kumfukuza Kitila, it has everthing to loose and nothing to gain!", kwa Kitila kufukuzwa Chadema, he has nothing to loose, (except time and efforts alizotumia na kupoteza), kwa sababu amefukuzwa na brain yake anayo!, and has everything to gain kwa kuivest anywhere else!. Hivyo the loosers ni Chadema na sio Kitila!, aombe msamaha kwa kosa gani?!.
Pasco.
Kaka,
Pasco, kwanza nimefarijika kusoma story yako ambayo imechimbua hadi ndani kabisa na kueleza hisia zako zote kuhusu sekeseke linaloendelea. Ninaomba nijibu kama ifuatavyo:
Kwanza bado nabaki kwenye msimamo ule ule wa kuunga mkono maamuzi ya CHADEMA ya kuamua kuwaadhibu kwa kile kilichokuwa kinaendelea. Ninaunga mkono maamuzi haya kwa sababu mtindo na utaratibu wa kutafuta madaraka uliotumiwa na kikosi hiki, haukuwa na mstakabali mzuri kwa chama. Utakumbuka kuwa kama sehemu ya utekelezaji wa mikakati ya waraka ule, Samsoni Mwigamba alitengeneza ID iliyoitwa mkulima masikini na akaitumia hiyo kuwananga viongozi wa chadema humu JF, huku akiwatuhumu kwa mengi yakiwemo ya kubadilisha vipengele vya katiba, tuhuma ambazo alishindwa kuzidhibitisha. Unakumbuka vema namna ambavyo makala za mwigamba humu jamvini ziliharibu taswira ya CHADEMA, nakuonekana ni chama ambacho viongozi wake wanakula ruzuku/wanatumia ruzuku kwa mambo yao binafsi na kujinufaisha bila kukisaidia chama. Unakumbuka kwamba skendo za Mbowe kutembea na Mbunge wake na kujenga nyumba huko Dubai ziliibuliwa katika kipindi kile?
Nataka tu kukuuliza Pasco, na kwa kutumia busara ya kawaida tu, CCM inachukiwa na wananchi kwa kuwa ina sera mbaya au kwa kuwa ina viongozi wabaya? Nataka niseme, hakuna namna yoyote unayoweza kuwachafua viongozi wakuu wa chama pasipo kukichafua chama? Kwa kuwachafua viongozi wa juu wa chama ni kukimaliza chama na si kukijenga. Katika hilo hawa ndugu zetu wakubali kuwa walifanya kosa.
Pili, Zitto alishakuwa na mienendo yenye kutilia mashaka tangu zamani, akianza na kukalia report ya uchunguzi wa mkataba wa madini wa Buzwagi, kupewa nafasi ya kuongozana na JK kwenda Sudan kusini kumwapisha Rais mpya wa huko bila kuwa na sababu zozote - jambo lililotafsiriwa kama ni rushwa, kuwasaliti wenzake wakati wa mpango wa kutoka bungeni ili kumpinga JK, kuanzisha na kufadhili kikundi cha masalia, nk. Katika mlolongo wa sintofahamu hizi ambazo zimejitokeza huko nyuma, ilikuwa ni aghalabu sana kwa CHADEMA kumsamehe mtu kama Zitto ambaye tangu mwanzo alionyesha kutafuta umaarufu wa yeye peke yake na si wa chama. Ikumbukwe pia Zitto alitiliwa shaka kwenye sakata la Lwakatare, ambapo yeye pekee aliandika barua kutaka chama kimtose Lwakatare, huku akijua kwamba Lwakatare angetoswa asingekuwa na uwezo wa kulipia gharama za kesi na hivyo angeshindwa kesi na pengine angewekewa maneno yenye kukifanya CHADEMA kifutwe. Mlolongo wa matukio ya Zitto yalimfanya ashindwe kuvumiliwa katika hili. Likewise, Mwigamba ambaye hakufanya vema alipokuwa mhasibu wa chadema makao makuu.
Katika hayo, naona ya kwamba akina Kitila walifanya kosa, ambalo kiujumla hata Kitila mwenyewe alilikubali na akawa radhi kuachia ngazi. Na hapo ndipo ninaposema kwa ustaarabu na uungwana aliouonyesha Kitila kwa CHADEMA wakati wa sakata hili, tofauti na walivyofanya wenzake, kwa hakika anastahili msamaha. Lakini pia kwa kuwa alikubali kosa na akawa tayari kujiuzuru, si vibaya pia akubali kuomba msamaha kwa faida ya chama na kwa faida yake.
Najua kwamba inawezekana kutokana na hasira au vinginevyo amefikia mahali pa kukata tamaa na kukiona CHADEMA si mbadala mzuri wa CCM, lakini naamini kama atapewa nafasi nyingine anaweza kuwa msaada mkubwa sana kwetu na akakisaidia chama chetu kuwa mbadala halisi wa CCM. Daima kama binadamu tunajifunza kutokana na makosa. Hakuna msafi hata mmoja kati yetu. Tofauti na akina Zitto na Mwigamba ambao walishakuwa wanakosea na kuonywa several times na hawakubadilika, Kitila hili ni kosa lake la kwanza. Apewe onyo, bila shaka ameshajifunza na amejua ni wapi alipoharibu. Yafaa asamehewe aendelee kusaidiana na wapambanaji wengine ndani ya CHADEMA.
Kitila ni mtu wangu wa karibu, namfahamu kwamba ni mpambanaji, ana rekodi nzuri ya kazi kila alipowahi kwenda, amekuwa mkuu wa kitivo pale DUCE kwa miaka isiyozidi miwili kafanya mambo ambayo hayalinganishwi na yaliyofanya na watangulizi wake waliokaa kwa muda mrefu. Ni mbunifu, mwenye IQ kubwa. Lakini zaidi ya yote, kwa asili yake
Kitila Mkumbo ni mwanasiasa. Yeye na siasa hawatenganishiki, lakini kwa uwezo wake na upenda mageuzi wake, sioni pengine panapomfaa zaidi ya CHADEMA. Kitila hawezi kuwa mwanaCCM kwa kuwa hataweza kabisa kuendena na sera za ndiyo mzee, sioni chama kingine chochote cha siasa nje ya CHADEMA ambako Kitila ataweza kudemonstrate uwezo wake halisi wa kufanya mambo. Itapendeza kwa hakika wakubwa wetu hawa ndani ya CHADEMA wafikirie upya kuhusu huyu bwana, tunaweza kuwa na hasira nyingi sana dhidi yake lakini haitasaidia chochote. Mtoto akinyea mkono hatuukati, bali tunauosha na kumkanya mtoto asijisaidie mikononi tena.
Pasco umeongea kuhusu suala la nani aombe msamaha, na umekosoa wazo langu la kwamba
Kitila Mkumbo aombe msamaha, lakini mimi napenda niwe mkweli katika hili. Hakuna namna yoyote ambayo CHADEMA watafikiria kumtafuta Kitila na kuomba msamaha. Hivyo ndivyo wakubwa walivyo, hata siku moja hawapendi kuonekana kwamba wamewapigia magoti walio wadogo kwao. Lakini kwa kuwa sisi tunamhitaji Kitila ndani ya chama, tunayo nafasi ya kumwombea msamaha, na ikiwezekana tunayo nafasi ya kumsindikiza kwenda kuomba msamaha. Wazo la kuomba msamaha ni lazima liwe initiated na Kitila mwenyewe akisaidiana na sisi. Hawa walio juu hawawezi hata siku moja kukubali kula matapishi yao wenyewe. Alifanya hivyo Kafulila na mambo yametulia sasa. Wakati mwingine ni vizuri kuwa mpole kwa ajili ya kuokoa mambo mengine mengi na makubwa kwa faida yako binafsi na ya taifa.
Bado naona Kitila ana msaada mkubwa kwa taifa letu kupitia chadema. Tukishika madaraka ya nchi hii kitila ni potential Minister of Education. Kuna ubaya gani akipiga magoti na akalifaa taifa letu katika nafasi ya waziri wa elimu huko mbeleni? Watu wanadhani akitubu atakuwa amedhalilika, lakini wanasahau impact yake kwa taifa baada ya kukubali hicho tunachodhani ni kujidhalilisha. Bado naona kuna haja ya kitila kukubali kupiga magoti ili yaishe. Yamewezekana kwa Kafulila why not Mkumbo. CHADEMA kinaongozwa na binadamu ambao pia wana mapungufu yao mengi tu, tunaamini hawataliangalia sana hili kosa moja la Kitila na kusahau mambo makubwa mengi aliyokifanyia chama na nchi. Na ni imani yangu kwamba hawa watu wanaoongoza CHADEMA, wanayatazama pia mapungufu yao na kutambua kwamba Kitila kateleza kama ambavyo hata wao waliwahi kuteleza hapo awali au wanavyoteleza kila siku. Tusameheane tusonge mbele.