Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo

Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo

Wewe ni miongoni mwa wafuasi sugu wa mwanaCCM Lowasa, I Itakuwa ni maajabu wewe kuitakia mema CHADEMA ambao ni maadui wa CCM akiwemo Lowasa, kwa vyovyote vile, utapendekeza kitu ambacho kina madhara kwa CHADEMA! kwa hiyo wewe, kumpendekeza Kitila, ni ushahidi tosha kuwa alikuwa na madhara kwa chama, Period.
Mkuu Kyafulilo, japo mimi sio Chadema, ila kiukweli nimeguswa na andiko lako kiukweli kweli!.
Naamini kama Chadema ina watu kama wewe, then amini usiamini nyinyi ndio mtakuja kuikomboa Chadema na kuifanya ikabidhiwe nchi!.

Umeandika very bonafide and genuine concern kumhusu Dr. Kitila. My opinion ni Dr. Kitila is one of the best brains Chadema has ever had!. Naomba nisieleze machungu yang kwa maamuzi ya mihemiko na double standards za CC ya Chadema!. nimefarijika kujua kumbe Chadema in a some few real people, wise, humble wanamini in humility and forgiveness vs confrontations, hatred, kukomoana na kukomeshana!.

Kiukweli kama mtazamaji wa nje ya box, ule waraka ulikuwa ni kutengeneza a "winning coalition" ningependa wakosaji wote wahukumiwe kwa haki huku wakitendewa haki!.

Baada ya kuwatimua kina Shonza kinyeme cha sheria, taratibu na kanuni, niliwasisitiza Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea haki Watanzania...

Ubarikiwe sana!.

Pasco
 
Chademachaga aka wachaga ukiwa sio wa kwao ww nje. Bwana asifiwe sana.
 
Mkuu pasco kama unajua kuna vichaa kwanini uchangie thread ya kichaa? Soma achana nayo. After all usipende kumuita mtu mwenye mawazo tofauti na yako kichaa bila hoja za msingi! Kichaa hawezi akaandika wala akamilki hata simu! Unaweza ukaona wewe uko sahihi kwa kila uzi unao uandika kumbe hata wewe unaushabiki wa mlengo fulani. Msomi mzuri na bora ni yule anae jadili hoja bila bias yoyote, pia kama anachama huwa tayari kukikosoa pale kinapokwenda ndivyo sivyo, je huwa unayafuata hayo? Napenda sana tuepuke matusi humu jukwaani maana hapa sio baa, ni sehemu ya kuelimishana kama darasa la mtaani.
 
Ni kweli na kuunga mkono inabid tutumie busara kidogo Dr anastahili kusamehewa maana hata mtoto akijisaidia kwenye kiganja huwez kukikata kiganja zaid ya kukiosha mpeni second chance tafadhalini
 
Wewe ni miongoni mwa wafuasi sugu wa mwanaCCM Lowasa, I Itakuwa ni maajabu wewe kuitakia mema CHADEMA ambao ni maadui wa CCM akiwemo Lowasa, kwa vyovyote vile, utapendekeza kitu ambacho kina madhara kwa CHADEMA! kwa hiyo wewe, kumpendekeza Kitila, ni ushahidi tosha kuwa alikuwa na madhara kwa chama, Period.
Mkuu Mjuni, kwenye siasa hakuna permanent friends or enemies, only a common interest!. Leo EL yuko CCM huko ndiko interest yake ilipo kwa Chadema ni adui!, lakini kesho CCM ispipomsimamisha interest ita shift, atahamia Chadema na ndio the one, and only anayeweza kuwaingiza Ikulu?!.

Chadema wasifanye kama Kikwete alivyosamehe wezi wa Epa.... Hilo lisitokee! Msipoweza kuwajibishana leo huko mwendako hata mawaziri mizigo mtashindwa kuwaajibisha! Historia hiyo ipo kwa ccm na isijirudie kwa utawala wa chadema!
 
Ningeweza kuunga mkono hili wazo la kumsamehe Dr.Kitila iwapo tu kwanza angeonyesha ushirikiano wa kutosha kwenye vikao vya CC.Lakini kwa bahati mbaya hakufanya hivyo mfano alikana kutomjua M2.Pili angetulia tu baada ya maamuzi hili nalo hakufanya hivyo .Tatu yeye amekula msimamo anasema hakitenda kosa je? asamehewe kwa lipi?
 
Mkuu Mjuni, kwenye siasa hakuna permanent friends or enemies, only a common interest!. Leo EL yuko CCM huko ndiko interest yake ilipo kwa Chadema ni adui!, lakini kesho CCM ispipomsimamisha interest ita shift, atahamia Chadema na ndio the one, and only anayeweza kuwaingiza Ikulu?!.
Pasco
Ok, kama wewe na CCM ya Lowasa mko after maslahi ni sawa.
Iambieni CCM yenu waache kujiita chama cha Ujamaa, wajiite ni mabepari ambao sera yao kuu ni maslahi ya kudumu, na hakuna rafiki wa kudumu.
 
Watanzania wengi bado wapo katika hali ya tahayari kufuatia kufuatia maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA (CC) kuwafukuza wanachama wake watatu ambao walikuwa na majina makubwa ndani ya chama hicho. Ni wazi kuwa CHADEMA haikumuangalia mtu usoni, ikarusha lungu lake bila kujali linamwangukia nani.

Nikiwa kama mwanachama wa CHADEMA, kwanza naunga mkono maamuzi ya CHADEMA kwa ujumla wake kwa kuwa yanajaribu kukitofautisha na vyama vingine vinavyolinda zaidi uenzetu badala ya kusimamia sheria na taratibu za uongozaji wa chama na pia katiba ya vyama vyao. Katika hili, CHADEMA imetuaminisha kwamba hata ikishika dola, itakuwa tayari kumuwajibisha yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na miiko ya uongozi, atakayeisaliti nchi, kuitia aibu na hata kutusababishia hasara au kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa vyenye kuisababishia umaskini nchi yetu na watu wake. Katika hili nakipongeza CHADEMA chama changu.

Pamoja na pongezi hizi, bado naona kwamba maamuzi haya yalikuwa ni ya haraka, na pengine yalitokana na mihemuko ya baadhi ya wanachama. Nasema hivi kwa sababu, katika ushiriki wa MM, M1 na M3 katika uandaaji wa waraka wa siri 2013, mmojawao ambaye ni Kitila Mkumbo alikubali makosa mara moja baada ya waraka huu kugunduliwa, alikuwa tayari kuachia ngazi kama sehemu ya uwajibikaji kwa kosa alilofanya, na hata pale alipotakiwa kwenda mbele ya kamati kujitetea, alifanya hivyo tofauti na wenzake walivyofanya ambao waliamua kutoroka na hata kukimbilia mahakamani. Ni dhahiri kwamba yeye kwa nafasi yake aliyajutia makosa yake na akaonyesha nia ya kutubu na kuendelea kukitumikia chama chake. Tayari Dr. Mkumbo ameshaaminiwa na chama kwa mambo mengi na makubwa, na kwa hakika ameshawekeza vya kutosha kwa ajili ya chama, ilitosha kumsamehe na kumpa onyo.

Nikitazama nyuma, katika utumishi wake ndani ya chama; tofauti na wenzake yeye hajawahi kuwa na kashfa yoyote wala kushiriki kwa namna yoyote kukihujumu chama. Kwa mfano ukimtazama mtu kama Mwigamba, tayari alishawahi kutofautiana na chama kiasi cha kufikia kuondolewa katika nafasi yake ya uhasibu kule makao makuu. Wakati Zitto ameshajihusisha mara kadhaa katika vitendo vyenye kutiliwa shaka ikiwemo kuendesha kikundi cha PM7 ambacho kilifanya kazi ya kuwachafua viongozi kwa nia ya kumjenga Zitto. Lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia kujihusisha na lolote.
Ninawaza ya kwamba kama chama hiki kilikuwa tayari kumsamehe Ben Saanane, ambaye alikuwa ndiye master planner wa mkakati mzima wa kumpindua Mbowe na Slaa kwa faida ya Zitto, hasa baada ya kukosa nafasi BAVICHA, ni kwa vipi kimeshindwa kumsamehe Kitila ambaye alishiriki kuedit tu waraka huu wa kuwaangusha akina Mbowe?

Bado ninaona kwamba Kitila ana mapenzi mema na chama hata kama kwa sasa amekata tamaa na kutamani mbadala wa CCM na CHADEMA. Nafikiri yaanzishwe mazungumzo kati ya chama na Kitila ili kuona ni namna gani anaweza kurudi chamani na ikiwezekana atimize ndoto zake za kuwa mbunge wa Singida kupitia CHADEMA na apewe onyo ili akitumikie chama kwa uaminifu kwa mjibu wa katiba ya chama.

Nina matamanio makubwa ya kuona Kitila anarudi CHADEMA. Kama NCCR mageuzi walimsamehe Kafulila, ni kwa vipi CHADEMA washindwe kumsamehe Kitila na ukizingatia kuwa ni kosa lake la kwanza? Ni lazima tutambue kwamba kama binadamu tuna mapungufu yetu, and we are prone to mistakes. Haitashangaza sana iwapo itatokea kwamba hawa hawa wanaosimama kwenye CC ya CHADEMA na kutoa hukumu kali dhidi ya watu ambao wapo tayari kutubu na kujirekebisha wakafanya madudu makubwa kushinda haya.

Sijamsemea Zitto na Mwigamba kwa kuwa tayari walishakuwa na kashfa za utovu wa nidhamu ndani ya chama kiasi cha kustahili adhabu, lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia katika hayo.

Nawaombeni viongozi wa CHADEMA mpunguze hasira, na kutoa nafasi ya mazungumzo na mwanazuoni huyu, na ninamwomba sana Dr. Kitila apunguze hasira, ajirudi na kukubali mazungumzo na viongozi wa CHADEMA. Waswahili husema kosa moja haliachi mke, nami nasema kosa moja la Kitila lisitufanye tukose mchango wake mhimu kwa chama.

Mungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki CHADEMA!

Mawazo yako ni mazuri na binafsi nayapenda. Ila kukubali tu kosa kama alivyofanya Dr. Kitila hakumaanishi kuwa Chadema imsamehe. Nadhani yeye alitakiwa kuandika barua ya kukiri kosa na kuomba msamaha. Ilivyoonekana Dr. kitila hakufanya hivyo sasa angesamehewa kwa lipi?
 
Mkumbo asamehewe wadau!cdm wamuweke chini na aonywe yaishe.ila zito asisamehewe.
 
Well thought idea. Japo there are times walionyesha hali ya ukaidi, lakini nafikiri haya yaliyojiri lazima yamewafundisha. Tuwasamehe tusonge mbele.
 
Dr.Kitila akili zake saw na wakina Mboe elfu moja.ila kilichotokea ni akili ndogo kutawala akili kubwa.
 
Dr.Kitila akili zake saw na wakina Mboe elfu moja.ila kilichotokea ni akili ndogo kutawala akili kubwa.
Sina shaka na uwezo wa Kitila. He is smart enough. I would say tumpe last chance.
 
Kitila akikubali kumtosa Zitto naunga mkono asamehewe coz nimemfuatilia toka mwanzo ameonyesha uungwana sana na nidham toka sekeseke hili lianze sema hapa mwishoni aliteleza akaharibu kidogo kwenye media,Ukisoma hata ule waraka alikuwa anasisitiza mambo yaende kwa umakini yasiharibu image ya Taasisi kuonyesha hakuwa na dhamira mbaya na CHADEMA,ila huyu anayepambana na Chama na yule Mwenzake wanaotumia mitandao kuchafua Viongozi NO!Hata wasisikilizwe.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Siyo kila anayekuja na mawazo tofauti au mtizamo tofauti ni mwanaCCM. Acheni utoto huo. Ni kwa lipi baya nililomsema Ben Saanane? Sijawahi kutofautiana na Ben Saanane, ila nimemtolea mfano tu, focus ya mjadala hapa ni Kitila, kama una la kuchangia kuhusu Kitila fanya hivyo.
Ulipomsema Saanane, nakulinganisha na Kitila aliyemwita MIDAEIGHT wakati wakiandaa waraka wa uasi ambao wewe umeupenda!
 
Dr.Kitila akili zake saw na wakina Mboe elfu moja.ila kilichotokea ni akili ndogo kutawala akili kubwa.
Kwa maneno ya "kitila" - nyuma ya pazia kama haya nasema "ALAANIWE KWA UASI!"..
 
Nina matamanio makubwa ya kuona Kitila anarudi CHADEMA. Kama NCCR mageuzi walimsamehe Kafulila, ni kwa vipi CHADEMA washindwe kumsamehe Kitila na ukizingatia kuwa ni kosa lake la kwanza? Ni lazima tutambue kwamba kama binadamu tuna mapungufu yetu, and we are prone to mistakes. Haitashangaza sana iwapo itatokea kwamba hawa hawa wanaosimama kwenye CC ya CHADEMA na kutoa hukumu kali dhidi ya watu ambao wapo tayari kutubu na kujirekebisha wakafanya madudu makubwa kushinda haya.
Mkumbo hatukuwahi kumsikia katika hayo.
Kipofu anapomshauri aonaye kuwa anachoona si kweli ni MAJANGA!!!!. Hakuna ujinga aliofanya ZITTO ambao nyuma yake hakuwepo KITILA!.
 
Ok, kama wewe na CCM ya Lowasa mko after maslahi ni sawa.
Iambieni CCM yenu waache kujiita chama cha Ujamaa, wajiite ni mabepari ambao sera yao kuu ni maslahi ya kudumu, na hakuna rafiki wa kudumu.
Mkuu Mujuni, kwanza mimi sio CCM, bali namkubali sana Lowassa!. CCM kilikuwa chama cha kijamaa enzi za Nyerere, azimio la Zanzibar liliuzika ujamaa ila ukabaki kwenye maandishi!. Tena maandishi hayo yako hadi kwenye katiba ya nchi!.
Pasco
 
Back
Top Bottom