Ninawasiwasi mkubwa na ujenzi huu

Ndetirima

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
1,008
784
Ninawasiwasi na ujenzi kama huu wa gorofa ya matofali ya kuchoma na udongo endapo kutatokea tetemeko kidogo tu la ardhi, madhara yanaweza kuwa makubwa sana. Jamani inabidi tuangalie uimara kwanza badala ya kujenga gorofa kutafuta sifa wakati uimara hakuna. Bora ujenge hata vyumba viwili imara kuliko hivi. Ni maoni yangu tu sio kashfa.
 
Attachments

  • Nyumba.jpg
    Nyumba.jpg
    56.9 KB · Views: 225
Acha ushamba!!
Maghorofa mengi yanayojengwa sasa watu wanaimarisha nguzo tu, labda na "slide beam"
Baada ya hapo unaweza kuweka hata maboksi pembeni,
Sembuse hayo matofali ya kichoma???
 
mhh ukitazama nguzo zinatia mashaka hata kwa macho
labda mtoa mada ameshaichunguza.
wabongo huwa wabishi kuambiwa ila linapotokea la kutokea tunakuwa wa kwanza kulaumu pia.
 
Acha ushamba!!
Maghorofa mengi yanayojengwa sasa watu wanaimarisha nguzo tu, labda na "slide beam"
Baada ya hapo unaweza kuweka hata maboksi pembeni,
Sembuse hayo matofali ya kichoma???

Hivi umeangalia vizuri hizo nguzo au unaropoka tu?
 
Acha ushamba!!
Maghorofa mengi yanayojengwa sasa watu wanaimarisha nguzo tu, labda na "slide beam"
Baada ya hapo unaweza kuweka hata maboksi pembeni,
Sembuse hayo matofali ya kichoma???

Hakuna sababu ya kutokwa mapovu,kama unauelewa tufahamishe kwa ustaarabu kwani sie tunaona kama ni tatizo
 
Barriers hakuna, hatari sana kwa binadam hao hapo juu...Otherwise maeneo mengine ni ya kiufundi zaidi. Huenda nikarudi.
 
Hakuna sababu ya kutokwa mapovu,kama unauelewa tufahamishe kwa ustaarabu kwani sie tunaona kama ni tatizo

Ok,
Ujenzi kama huu wa ghorofa moja una aina mbili,
Waweza kulaza matofali (ya umeme) kisha nguzo zisiwe imara sana na maisha yakaenda!!
AU
Unaweza ukasimamisha matofali (au usiweke kabisa) but nguzo ziwe imara sana na maisha yakaenda vilevile!!
Ujenzi huu wa aina ya pili wa kutegemea uimara wa nguzo na slide beam (roof/floor) unatumika hata kwa majengo ya zaidi ya ghorofa marefu zaidi!!
Ukiwa hujui tumia lugha nzuri ueleweshwe!!
 
Acha ushamba!!
Maghorofa mengi yanayojengwa sasa watu wanaimarisha nguzo tu, labda na "slide beam"
Baada ya hapo unaweza kuweka hata maboksi pembeni,
Sembuse hayo matofali ya kichoma???

Ninakubaliana na wewe kabisa Mkuu. Uimara wa nyumba si matofali bali vitu vifuatavyo:
- Uimara wa msingi. Ni bora na pengine lazima kupata wataalamu kupima uimara wa ardhi unapojenga na kukushauri utumie nyenzo za aina gani na kwa kiwango gani. Sio tu kumimina mifuko ya zege (hapa tusidhani kuwa kadri suruji inavyokuwa nyingi ndivyo uimara wa msingi, ni zaidi ya hivyo. Tafuta watalaamu wafanye utaalamu wao)
- Vivyo hivyo kwa nguzo (side beams). Usishitushwe na unene wa beams, uimara wake umo katika nyenzo zilizotumika). Tumeona nguzo nene zinakatika pamoja na nondo zake ikiwa ardhi haiko imara na havikutumika viwango sahihi.

Kwa umasikini upande mmoja, tunachukua mafundi wa vichochoroni ili kupunguza/kuepuka gharama. Kwa upande wa pili, tunaka mijisifa ya kuwa "na mimi nimejenga ghorofa) bila ya kuzingatiambo muhimu ya kitaalamu. Tukumbuke kuwa lengo hasa sio kuwaonesha watu tumefanya nini, bali suala la nyumba linapohusika tuzingatie usalama wa watakao ishi na kwamba jengo hilo linatakiwa lidumu milele (kwa karne nyingi).
 
Ninawasiwasi na ujenzi kama huu wa gorofa ya matofali ya kuchoma na udongo endapo kutatokea tetemeko kidogo tu la ardhi, madhara yanaweza kuwa makubwa sana. Jamani inabidi tuangalie uimara kwanza badala ya kujenga gorofa kutafuta sifa wakati uimara hakuna. Bora ujenge hata vyumba viwili imara kuliko hivi. Ni maoni yangu tu sio kashfa.

Kama sijakosea huyo mwenye gorofa hiyo ni jirani yako au mtu unayejilinganisha naye na sasa wivu unakusumbua hulali,unaona akikaa juu atakutemea mate kwenye kamsonge kako. Jaribu kuwa na wivu wa maendeleleo, mfuate umshauri au jenga gorofa yako umuonyeshe mfano ni vipi gorofa inatakiwa kujengwa.Masikini hatauona ufalme wa mbinguni kwa vile ndani ya umasikini kuna chuki, wivu na husuda.
 
Back
Top Bottom