Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,135
- 282,834
JajiJoseph Sinde Warioba, waziri mkuu mstaafu amesema maisha yake yako hatarini. Anatishiwa kuuawa, lakini hana cha kuogopa.
"Kuna watu wengi sana wanaoniletea ujumbe, kwamba mzee angalia. Ukiendelea hivi. ama utatekwa au utapewa sumu," anaeleza.
Anaongeza mini nawajibu tu hainipi matatizo, maisha yangu yapo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Siwezi kutishwa, siogopi. Wala kutengwa hakunitishi.
Anasema, kwa ajili ya umri wake na afya yake, mara nyingi anakuwa nyumbani na hivyo, hana anachohofia.
Anasema, vitisho hivyo anavipata kutokana na msimamo wake wa kukosoa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Jaji Warioba ametoa kauli hiyo, katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari hivi karibuni, ambapo MwanaHALISI limekuwa likichapisha mahojiano hayo kwa wiki ya tatu sasa.
Katika mahojiano hayo, pamoja na mengine, Jaji Warioba, ameonesha masikitiko na kilichotokea tarehe 29 Oktoba mwaka jana, kufuatia ghasia za maandamano yaliyolenga kupinga kuwapo kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
Waandamaji wakiongozwa na vijana na wanawake, walijitosa mitaani, kushinikiza serikali kufanyia mabadiliko mifumo ya uchaguzi na ujio wa Katiba mpya.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, maelfu ya watu waliuawa na vyombo vya dola wakati wa maandamano hayo.
Hakutaja idadi, lakini alisisitiza. "...watu waliouawa kwa risasi, wakati wa maandamano ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi wa 29 Oktoba, ni wengi kuliko wale waliokufa kwenye vita vya Kagera.
Alisema, "Waliokufa siyo makumi. Siyo mamia. Ni maelfu. Ni wengi kuliko wale waliokufa kwenye vita vya Kagera.
Akifafanua madhila anayopitia, Jaji Warioba alisema, kuna wakati anapokea ujumbe, kupitia simu yake ya mkononi, wenye harufu ya vitisho.
Bali yeye anasema, "Nimelelewa kusema ukweli. Nitaendelea kusema ukweli." Anasema, hiyo ndio ahadi ya TANU (Tanganyika African National Union), kwamba "tumelelewa hivyo
Anasema, "Kule TANU, siku hizi tunazungumza Katiba ya CCM, lakini mengi yalitoka kwenye Katiba ya TANU, maana wakati ule uliluwa ukijiunga na TANU, lazima ukubali ahadi zake
"Ahadi moja ya nane inasema nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko Hii ni ahadi anafafanua, kwa kuwa yeye ni muumini wa TANU na CCM, hatayumbishwa Ataendelea kusimamia ukweli.
Anaongeza, "Mimi nasema jambo ambalo naliona ni kweli. sitegemei watu waniletee fitina Kama nimekosea watakuja nione kosa langu.
Anasema, kuna watu wengi wananitakia mema, kwa sababu ya hali ilivyo nchini na anafurahi kuona kuna watu wanaunga mkono msimamo wake huo.
"Wakati mwingine kwa kuwa nayasema haya, unaonekana kama hutakiwi. Wakati mwingine unatoa hoja, unapata lugha ya kubezabeza.
"Kuna wakati napigwa vijembe baada ya kutoa maoni yangu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana (mwaka 2024), anasimulia.
Anasema, "Wakati tunamuaga mwenzetu (Cleopa Msuya, allyewahi kuwa waziri mkuu) walisema kuwa yeye hakuwa na tabia ya kuongea na vyombo vya habari kuisema serikali."
Anasema maneno yaliyosemws kuhusu ukimya wa Msuya yalimlenga yeye. Hakumtaja aliyetamka.
Hata hivyo, rekodi zinaonesha kuwa aliyetamka maneno hayo alikuwa Jakaya Mrisho Kikwete, rais mstaafu wa Tanzania, kwa kile kinachoitwa na baadhi ya watu, "kulinda maslahi yake Wanasema, Kikwete ni mmoja wa wanufaika wakubwa wa serikali iliyopo madarakani.
Mbali ya kulipwa mabilioni ya shilingi kama stahiki za kuwa rais mstaafu. Kikwete bado anaendelea kufanya kazi kadhaa za serikali, ikiwamo kuwakilisha nchi kwenye mikutano ya kimataifa.
Aidha, mke wa Kikwete, Salma Kikwete, anapokea mamilioni ya shilingi anayolipwa kwa wadhifa wa ubunge na mafao yanayotokana na kuwa mwenza wa rais mstaafu.
Akizidi kufafanua hoja yake. Jaji Warioba ambaye alipata kuwa makamu wa rais alisema, "Na katika kipindi hiki, mimi nilikuwa nazungumzia yanayoendelea nchini."
Anasema, alikuwa anaambiwa asiendelee kuzungumzia mambo yanayoendelea nchini, ikiwamo kuvurugwa kwa chaguzi za serikali za mitaa kwa kuwa heshima yake itashuka.
Anasema, "Lakini nikawajibu, kushuka huko, ni kwa watu wa Juu".
Anasema, kuna wakati aliambiwa anayosema hayasaidil, bali yanasaidia upinzani.
Nikawaambia, niliyoyasema mwaka 2024, kukosoa uchaguzi, maana nilisema kuingilia mawakala ni dosari kubwa, kutumia kura bandia ni dosari kubwa, hivi hapa nimekosea wapi, anaeleza kwa njia ya kuhoji.
"Mnipe kwa hoja. Mnieleze kwamba kuengua wagombea ni kuzuri, kwa sababu hizi na hizi. Lakini mnasema haya ninayosema haya hayasaidi siwaelewi, anasisitiza.
Anasema, kuna wakati yeye na Joseph Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu ya Mwalimu Nyerere, walipokea ujumbe kwamba wanataka kulipeleka taifa pahala pabaya.
Anasema, "Lakini mimi nililelewa katika misingi ya kusema kweli na bila kuwa na kinyongo.
Akizungumzia shinikizo la mabadiliko, Jaji Warioba amesisitiza kuwa mabadiliko nchini yataletwa na vijana licha ya wazee kutengeneza njia na misingi imara ya taifa.
"Misingi ile ambayo tumeikuta Itabaki kuwa misingi, lakini mabadiliko yataletwa na vijana, ameeleza
Akizungumzia nguvu iliyotumika kukabiliana na waandamanaji, Jaji Warioba anasema, kwa miaka miwili vyombo vya ulinzi na usalama viliambiwa vijiandae kuja kusimamia mchakato wa uchaguzi, ili uwe huru, haki na amani.
"Kwa hiyo, watu waliamini kuwa vyombo hivi vimejiandaa, kama kitatokea chochote. Sasa tunajiuliza, walijiandaa vipi? Walijiandaa kwa bunduki na risasi? Kwa sababu ndizo walizotumia zaidi. Nini waliandaa na hiyo ndio inayoweza kutusaidia kufahamu kama ngua iliyotumika ilikuwa inafanana na mazingira.
Anaongeza, "...unakabiliana na vijana ambao hawana bunduki za kisasa. Wewe unazo, sasa watangaze, ndio tunaweza kuamua kama inastahill. sama nguvu iliyotumika
Anasema, "Mimi nadhani kwamba hali ni tofauti. Maana unaona waliouawa, ukiangalia vita ya Kagera, vijana wetu waliouawa na adul ukilinganisha na idadi ya hawa wanaozungumziwa hapa, ni wengi kuliko wale. Kule tuliusa na adul, hapa tumejiua sisi wenyewe.
Anahoji, "Hivi hawa polisi, hakuna hata mmoja ndugu yake ameuawa? Hawa wa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, hakuna hata mmoja ambaye ndugu yake ameuawa? Ama hawa viongozi hakuna hata mmoja ndugu yake ameuawa.
Anasema, tusimtafute mchawi kutoka nje, matatizo ya tumesababisha sisi wenyewe Tusiwasingizie wengine. Haya tumeyafanya hapa.