Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 350
1.Kabla sijampata nilimwonyesha kiwanja cha kaka yangu nikamdanganya changu
2.Nilimdanganya mshahara anao upata yeye mimi napokea mara mbili yake ukweli napokea nusu ya mshahara anayelipwa yeye
3.Pesa ambazo nilitumia kwenda Outing na matumizi mbalimbali kumfanya awe happy, kiukweli mimi ni muhasibu wa kikundi fulani hivi kwa sasa nina loss kubwa sana
4.Nilimdanganya sina mtoto, kwa kweli nina mtoto moja
Nimemdanganya mambo mengi sana. Wiki ijayo napeleka posa ili tufunge ndoa. Sasa naombeni ushauri, nimwambie au niache aje akumbane nayo mwenyewe ndani ya ndoa.
Peleka posa kwanza, afu ukishaoa unamwambia ukweli.
Kuna ule wimbo wa 'pendoo eeeh, mimi mumeo ni kibarua wa kuponda kokoto hapa mjini eeh'
Peleka posa kwanza, afu ukishaoa unamwambia ukweli.
Kuna ule wimbo wa 'pendoo eeeh, mimi mumeo ni kibarua wa kuponda kokoto hapa mjini eeh'
dah! kwanini ulimdanganya? nimeumia utafikiri mimi ndio huyo bidada.
Endelea kumdanganya tu hata baada ya kuwa umemuoa, ndivyo walivyo hao viumbe. Ukimwambia ukweli kwake uongo, uongo kwake ukweli.
Mh....!!
Pole kwa maumivu ulopata
mi naona amwambie tu ukweli kabla. hebu jiweke kwenye nafasi ya huyo mwanamke uhisi maumivu utayoyapata.
Aisee! Sa kwanini umenidanganya muda wote huo? Bora hayo mengne na mtoto? Tafadhali peleka posa kwa huyo mzazi mwenzio SIKUTAKII!!
Hata sasa keshaumia, maana kama posa imeshatangazwa na wazazi wa binti wanajua. eti aje aahirishe ndoa kisa bwana kadanganya? Huo usumbufu atakajiletea bora tu aolewe kwa kudanganywa, wataelewana ndoani
Endelea kumdanganya tu hata baada ya kuwa umemuoa, ndivyo walivyo hao viumbe. Ukimwambia ukweli kwake uongo, uongo kwake ukweli.