Ninataka kumwambia mpenzi wangu ukweli, naombeni ushauri.

Msandawe Halisi

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
647
350
1.Kabla sijampata nilimwonyesha kiwanja cha kaka yangu nikamdanganya changu

2.Nilimdanganya mshahara anao upata yeye mimi napokea mara mbili yake ukweli napokea nusu ya mshahara anayelipwa yeye

3.Pesa ambazo nilitumia kwenda Outing na matumizi mbalimbali kumfanya awe happy, kiukweli mimi ni muhasibu wa kikundi fulani hivi kwa sasa nina loss kubwa sana

4.Nilimdanganya sina mtoto, kwa kweli nina mtoto moja

Nimemdanganya mambo mengi sana. Wiki ijayo napeleka posa ili tufunge ndoa. Sasa naombeni ushauri, nimwambie au niache aje akumbane nayo mwenyewe ndani ya ndoa.
 
dah! kwanini ulimdanganya? nimeumia utafikiri mimi ndio huyo bidada.
 
1.Kabla sijampata nilimwonyesha kiwanja cha kaka yangu nikamdanganya changu

2.Nilimdanganya mshahara anao upata yeye mimi napokea mara mbili yake ukweli napokea nusu ya mshahara anayelipwa yeye

3.Pesa ambazo nilitumia kwenda Outing na matumizi mbalimbali kumfanya awe happy, kiukweli mimi ni muhasibu wa kikundi fulani hivi kwa sasa nina loss kubwa sana

4.Nilimdanganya sina mtoto, kwa kweli nina mtoto moja

Nimemdanganya mambo mengi sana. Wiki ijayo napeleka posa ili tufunge ndoa. Sasa naombeni ushauri, nimwambie au niache aje akumbane nayo mwenyewe ndani ya ndoa.

mwambie,ndo utajua kama anakupenda au lah
 
Peleka posa kwanza, afu ukishaoa unamwambia ukweli.
Kuna ule wimbo wa 'pendoo eeeh, mimi mumeo ni kibarua wa kuponda kokoto hapa mjini eeh'
 
Endelea kumdanganya tu hata baada ya kuwa umemuoa, ndivyo walivyo hao viumbe. Ukimwambia ukweli kwake uongo, uongo kwake ukweli.
 
mi naona amwambie tu ukweli kabla. hebu jiweke kwenye nafasi ya huyo mwanamke uhisi maumivu utayoyapata.
 
mambo mengine sio ya kuficha. hivi kwanini mnaficha damu zenu? sio vizuri na mnakeraaaa!
 
Hata sasa keshaumia, maana kama posa imeshatangazwa na wazazi wa binti wanajua. eti aje aahirishe ndoa kisa bwana kadanganya? Huo usumbufu atakajiletea bora tu aolewe kwa kudanganywa, wataelewana ndoani

mi naona amwambie tu ukweli kabla. hebu jiweke kwenye nafasi ya huyo mwanamke uhisi maumivu utayoyapata.
 
Aisee! Sa kwanini umenidanganya muda wote huo? Bora hayo mengne na mtoto? Tafadhali peleka posa kwa huyo mzazi mwenzio SIKUTAKII!!

Looh!!! Utamfanya asimwambie ukweli, maana posa itaweza pigwa teke kule

Hata sasa keshaumia, maana kama posa imeshatangazwa na wazazi wa binti wanajua. eti aje aahirishe ndoa kisa bwana kadanganya? Huo usumbufu atakajiletea bora tu aolewe kwa kudanganywa, wataelewana ndoani

hapana bana, bora mdada ajue mapema akiweza kufanya maamuzi magumu na afanye, kama atahisi kwake ni sawa aendelee. hakuna maana ya kuona halafu ndoa ije kukosa maelewano ndani ya muda mfupi. amwambie tu ukweli.
 
Sasa na wewe kama ulikua na malengo naye ulimdanganya yanini. Mwambie tu ukweli aamue kusuka au kunyoa.Leo unaenda kutoa mahari ukiwa na mauongo kibao kesho mko ndani kikatokea cha kutokea, atakuamini kweli? Umetumia style ya zamani sana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom