Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 47. Nina watoto watatu. Ninaishi Dar es Salaam.

Ninahitaji kumpata mwanamume ambaye ana mapenzi ya dhati hasa uaminifu. Sihitaji kuolewa au niseme kuishi na mwanamume kwa haraka ila ninataka company tu. Na kupitia kampani nitaweza kujifunza kwa undani kama kweli mwanaume yuko siriazi au la. Ninachohitaji kwa sasa ni upendo wa dhati, Nimerudia hapo.

Sitaki wabahishaji wa mahusiano na hapa atakayejitokeza awe mtu wa uhakika ambaye:

- Ni mgani i.e aliyefiwa na mkewe kwa misingi hii kama una baba yako hapa alifiwa na mama niunganishe tu. Au kaka yako ambaye amefiwa na mke niunganishe tu. Au awe Mtalaka na si kutengana.

- Akubali kupima HIV

- Asiwe mume wa mtu au mwanaume ambaye hajaoa ila ana wanawake ambao ana connect nao. Hii imenigusa sana baada ya kukutana na mwanaume ambaye alizaa na several women kumbe ni mtu ambaye hana future kabisa kimaisha ya familia. Nilimpenda sana ila changamoto za wanaume kama hawa ni kubwa sana. Ni kujitakia presha.

- Anipe uhuru wa kufanya mambo yangu ya kiuchumi kwa kuwa nina watoto na ninahitaji wasiishi maisha ya tabu . Sitaki kuwa tegemezi hapa. Nimejifunza sana.

- Awe ananithamini mimi kama mpenzi wake na asinilazimishe ndoa mpaka pale nitapona kuwa kweli ni mtu wa kuzeeka naye.

- Awe ni mtu anayejituma katika kuzalisha mali, either ameajiriwa/kujiajiri au anafanya biashara zake.

- Awe ni mtu anayependa familia kwa kuanzia na watoto wake mwenyewe iwe ni priority kwake kabla hajawapenda wanangu mimi.

- Awe tayari kuandikiana pre-nuptial agreement kama itafikia mahali tuamue kuishi pamoja. Ninasema hivi kwa kuwa atakuwa na mali zake na wanawe ambao atataka kuwapa urithi na mimi nina wanangu na chochote kidogo nilichoweza kuhangaikia kwa miaka yangu hivyo sitaki ugomvi wa mali hata kidogo.

- Asiwe Mlevi au Mvuta sigara.

- Awe mkristu. Sibagui ila mimi ni mkristu na wanangu pia hivyo itakuwa shida kidogo hapa. Nimekuwa mkweli msinielewe vibaya.

- Awe na miaka kati aya 47-52.

- Akiwa DSM ni vizuri. Nje ya DSM tutakubaliana workable situations.

- Vigezo visikutishe kama una vingi kati ya hivyo hasa umri na kutokuwa na mke tuwasiliane PM na ninaamini tutafikia muafaka wa pamoja.

Ninasema sasa kwa mwanaume ambaye anaona anaweza kujaribu kuanzisha mahusiano na mimi karibu PM. Ukiona utatoa lugha mbovu isiyo na staha ninaomba upite taratibu.

Angalizo.
Nipo serious, ninaomba sitaki lugha za matusi au mitaani mimi ni mtu mzima. Wanaume serious tu na wenye umri niliotaja wani Meseji (PM].
mie umri huo sijafikia ila napenda wanawake wa umri wako,ninaamini nina uwezo wa kukukojoza,maana umri unaouhitaji wengi visukari tu,nguvu hamna,hasa hao wanaume wa dar,anyway kila la kheri mamangu!
 
Kwa umri wako, 47 ni ngumu kidogo maana wigo ni mdogo. Wengi wameshaoa na wanaendesha familia zao. Lakini Mungu akiwa upanxe wako, hakuna gumu lolote.

* Jaribu kuwa flexible, huwezi kupata 100% match. Katika maisha sio vizuri kuweka "mimi" wakati wote. Ni lazima uangalie na yule unayetaka kuishi nae anaweka nini mezani ili mkijadili na kupata muafaka(compromising is very important in relationships)

* Sio lazima awe 47-50yrs, katika huo umri unaweza kuishi na mtu mwenye 44+yrs bila tatizo lolote kwa sababu tayari naye amejiweka vizuri, ana watoto(hasa kama wameachana au kufiwa) maisha yake yapo solely kwa ajili ya watoto.

* Una watoto watatu, je uliwahusisha wakati wa kufanya maamuzi? Au una mpango huo baada ya kukutana na Mr? Ni vizuri wakajua, wakaridhia na kukupa baraka. Nina close relative ambaye watoto walikataa kabisa, akafosi na leo hii mtoto mmoja hataki kushirikiana na mama yake, ameondoka nyumbani.

* Mtu akikuomba uende PM au akituma namba ya simu, sio vizuri kukataa. Wengine humu hawajui PM ni kitu gani, unaweza kuanzisha chats huko PM. I'm writing from experience.
 
Hongera mama natumai utampata mzee, nilikua sijui na kama mlio na umri mkubwa mnawashwa hivi duu kweli age is just a number, genye ziko pale pale.
Hiyo avatar yako kama sikosei naona kama ni shada la maua la ile nyumba yetu ya milele. pole sana i hope utapata chaguo lako maisha yasonge yadi Mungu atakapokuita
 
Kwani Hadija Kopa siyo binadamu? Age lies on a positive side of number line in ascending order. You will soon or later be there.
mama nikuishauri kitu ungeweka namba ya simu au email adress maana pm ni kwa members wa jf tu.wanaosoma ambao sio member hawataweza kukupata
halafu humu waongooo kuwa makini mama
 
mama nikuishauri kitu ungeweka namba ya simu au email adress maana pm ni kwa members wa jf tu.wanaosoma ambao sio member hawataweza kukupata
halafu humu waongooo kuwa makini mama
Amina sana. Asante mno kwa ushauri hasa kwa waongo. Hawakosekani na ndiyo wengi. So far kwa miezi minne sijafanikiwa kabisa. Sijaona serious kwa vigezo ila hata japo kuwa mkweli wa kumaanisha. Niko busy na mambo Yangu sasa ila ninaamini yupo atakuja kwa Majira yake Mungu. Mungu hujibu Maombi na asipojibu haraka ana sababu na hakuna kukata tamaa.
 
mie umri huo sijafikia ila napenda wanawake wa umri wako,ninaamini nina uwezo wa kukukojoza,maana umri unaouhitaji wengi visukari tu,nguvu hamna,hasa hao wanaume wa dar,anyway kila la kheri mamangu!
Uwe na adabu. Kamkojoze mama yako. Nilitoa angalizo toka awali kuwa sitaki lugha za kipuuzi. Mimi ni MTU mzima na nimelelewa. Hiyo sentensi ya mama yako nimeitoa kukuonyesha point ya kutovumilia ujinga na ukilaaaaza.
 
Kwa umri wako, 47 ni ngumu kidogo maana wigo ni mdogo. Wengi wameshaoa na wanaendesha familia zao. Lakini Mungu akiwa upanxe wako, hakuna gumu lolote.

* Jaribu kuwa flexible, huwezi kupata 100% match. Katika maisha sio vizuri kuweka "mimi" wakati wote. Ni lazima uangalie na yule unayetaka kuishi nae anaweka nini mezani ili mkijadili na kupata muafaka(compromising is very important in relationships)

* Sio lazima awe 47-50yrs, katika huo umri unaweza kuishi na mtu mwenye 44+yrs bila tatizo lolote kwa sababu tayari naye amejiweka vizuri, ana watoto(hasa kama wameachana au kufiwa) maisha yake yapo solely kwa ajili ya watoto.

* Una watoto watatu, je uliwahusisha wakati wa kufanya maamuzi? Au una mpango huo baada ya kukutana na Mr? Ni vizuri wakajua, wakaridhia na kukupa baraka. Nina close relative ambaye watoto walikataa kabisa, akafosi na leo hii mtoto mmoja hataki kushirikiana na mama yake, ameondoka nyumbani.

* Mtu akikuomba uende PM au akituma namba ya simu, sio vizuri kukataa. Wengine humu hawajui PM ni kitu gani, unaweza kuanzisha chats huko PM. I'm writing from experience.
Asante mno kwa ushauri wako ndugu. Nitazingatia yote. Ukweli. Nimekataa kuwasiliana na waliotoa namba straight. I am sorry kama nimewakwaza. Nikitaka japo tufahamiane kwanza kiasi na ikifika kupeana namba inakuwa tayari na Matumaini Fulani. Wengi walitaka namba sasa huwezi kumpa kila MTU nao ni usumbufu. Mungu atabgulie yote.
 
Hata mimi siafiki kutoa namba mapema, especially kwa sasa ambapo matapeli wa kifijitali wamejaa. Lakini akiikupa namba, we mzukie pm, kama yupo serious kweli mtaongea.
 
Back
Top Bottom