Asanteni wote.
Lengo langu kuu ni kuwapa vijana taaluma za kuwa wapasha-habari/watoa-taarifa (communicators). Kama mnavyoelewa, hivi sasa, ili ujumbe wako umfikie mlengwa, unahitaji kuwekwa kwenye mfumo unaoeleweka. Kwa mfano, kuna masuala ya "branding", ambapo kampuni hupenda ujumbe wake uwe kwenye mfumo usiobadilika.
Kuna artistic na technical skills, kama vile produduction (digital videography, editing, motion effects, special visual effects, sound effects, etc.), graphic arts (the full spectrum), na mengi mengine.
Hizi ni highly skilled professions. Kampuni kama vile Tigo, Vodacom, Airtel, hutumia pesa nyingi sana kutengeneza hizo branded advertising campaigns zao, NJE YA NCHI, kwa kuwa hatuna wataalam wa kutosha wenye uwezo wa kufanya kazi hizo KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA. Sisi tumezoea ulipuaji. Angalieni matangazo (graphic ads) ya TBC1, ITV, Channel TEN, na wengineo. CloudsTV wanajitahidi kwenye upande wao wa Graphic Identity.
Mimi nimejifunza kufanya mambo haya kwa kuwa nina kipaji cha asili. Lakini, cha msingi ni kwamba, nataka kuwapa vijana hizi skills, ili waweze kujiajiri wenyewe, ama kwa kushirikiana au kwa namna yoyote ile. Na atakayependa kuajiriwa, basi atakuwa na uwezo wa kufanya kazi yake vizuri.
Nadhani nimeeleweka.