Ninashuhudia mambo mazito kwenye ndoa ya dada yangu. Natamani kumshtua jamaa asiendelee kuibiwa ila nashindwa

Wakubwa shikamoni, Wadogo hamjambo?

Dadaangu ameolewa mwezi wa 10 mwaka jana alikua mjamzito mimba kubwa tu. Wamehamia mkoa wa mbali anaishi na Bwana wake. Sister alijifungua mwezi wa 3 mwaka huu. Juzi juzi nimeenda kikazi nikafika kumtembelea kwenye mji wake.

Nilishaangaa sana aisee.

Mtoto wa sister sasahiv anasimamia vitu, aisee hafanani na shemeji kwa lolote. Nilipomkagua nikagundua anaufanano mkubwa na njemba flani niliwah kutambulishwa na sister kwenye party flani kwamba ndo angekua bwana wake wa kuona. Yani dogo ile rangi, utege, kisogo na mapepe ya macho purely ni yule njemba aisee.

Kama mwanaume ninaumizwa sana ninaona shemeji kabambikwa ila sina la kufanya.

Niliona sister anajistukia na kama anakua anatabasam nikimshika mwanae na kumrusharusha...amegutuka kwamba sikubaliani nae kuhusu baba wa mtoto.

Hii imekaaje wakuu?
Jitahidi utafute kazi ufanye, anayofanyiwa chumbani dada yako na shemeji kwa kosa hilo usipende kuyajua
 
Una hamu dada ako awe single mama wewe.

Mshtue tuu mwana kisha uondoke na sister ako kurudi home kwenu.
 
Kijana unaonekana una element za ukikekike, ndio maana dada ako akawa na guts za kukuonesha anayemgegeda wakati hajaolewa.

Na hili linathibitishwa na wewe kutokuwa na kifua mpaka umeamua kuleta hii siri ya dada ako kwenye social media.

Man up mtoto wa kiume.
 
We fanya kazi iliyokupeleka upite iv. Dada ako mwache na ndoa yake. Nyumba zinaficha mengi. Labda shemeji yako anajua kuwa analea mtt ambae c wake. Unaenda kumwambia unashangaa unaaibika ww. Mwachie dada ako msala wake.
 
Kwa mwafrika c ajabu ni kawaida sana kufanya huo ukatiri, but co wote wako ivyo.
sio Africa tu duniani kote.hakuna anayeweza kuvumilia kulea mtoto wa mwenzie.yaani hapo huyo dada afanye mpango ambebee mimba mumewe kupunguza makali.
Ila inauma sanaa.mimi nilibambikwa mimba bandia . nashukuru mungu baaadae nikajua.nikaachana nae.
Hapo nishahudumia vya kutosha.
Je ningebambikiwa mtoto sio wangu si mpaka leo ningeendelea kumuhudumia.?
 
Back
Top Bottom