Ninashauri 'Mashabiki' Wenzangu wa Simba SC leo tukivaa Jezi tuwe na za Mashati ya Kawaida ya Kubadilishia kwani Upepo si mzuri

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Msidanganyike na asiwadanganye Mtu 85% ya Mechi ( Derbies ) za Simba SC na Yanga SC nchini huwa zinachezwa sana nje ( namaanisha Kishirikina ) 10% Kuhonga Wachezaji au Waamuzi na 5% ni Ufundi pekee kutoka kwa Makocha. Bahati nzuri ninaposema 'Uchawi' ni mwingi ninamaanisha kwani nimeshawahi kuwepo huko miaka ya nyuma kabla sijaamua Kumrudia Mola.

Mara kwa mara GENTAMYCINE katika hizi 'Derbies' nimekuwa nikileta Tabiri ( Nujumu ) zangu na namshukuru Mwenyezi Mungu 90% huwa zinakuwa kweli ( vile vile ) na hizo 10% zinazobaki huwa ni Maamuzi yake tu Mwenyezi Mungu kwani kumbukeni hata Wachawi, Waganga, Majambazi na Mapopoma nao pia humuomba na humtegemea mno huyu huyu Mola / Maulana.

Mechi ya leo tarehe 7 Oktoba 2020 kati ya Yanga SC na Simba SC GENTAMYCINE nakuja na Nujumu ( Tabiri ) yangu ila nakuomba utambue kuwa 'sijakulazimisha' uiamini au baadae kama 'Ukibeti' kwa Mhindi kisha 'ukakosa' ukaniona Mimi nimekuingiza 'Chaka' bali ukikosa hiyo Hela ( Pesa ) tambua tu ya kuwa Wewe ni 'Popoma' uliyetukuka kabisa na Mimi sihusiki na sitohusika kabisa.

Mpaka muda huu naandika huu Uzi Salamu kutoka Kisiwani Pemba, Morogoro na Tanga kwa 'Wataalam / Mafundi' wangu ni kwamba Mechi ya leo 'Kinyota' imekaa vibaya sana kwa Simba SC Kushinda. Pia hata tarehe yenyewe ni 'Nuksi' Kwetu Simba SC na muda uliopangwa wa Saa 11 nao ni mbaya 'Kinyota' kwa Simba SC yetu.

Ninachomaanisha hapa ni kwamba Ushindi wa Simba SC leo ni Sare ( Draw ) ila uwezekano wa 'Kufungwa' na Yanga SC ni mkubwa kutokana na 'Nyota' ya Siku ya leo ambayo ni ya Jumamosi. Hata hivyo mambo ya 'Nyota' na 'Ulozi' huwa yanabadilika kutokana na Nyakati na juhudi za 'Kishirikina / Kindumba' kutoka kwa upande mwingine ( hapa namaanisha Watu wa Simba SC )

Hivyo Ushauri wangu mzuri ( Kuntu ) kabisa kwa Wana Simba SC Wenzangu leo tukienda Uwanjani tukiwa na Jezi zetu tujitahidi pia ama kwa ndani tuwe na Mashati yetu ya Kawaida au tubebe Mifuko tuweke Mashati yetu ya Kawaida ila ikitokea kweli 'tumefungwa' basi haraka sana 'tubadilishe' ili Kupunguza 'Kuzomewa' njiani na Watu wa Yanga SC.

Ikitokea Simba SC yetu 'itashinda' basi itakuwa ni Jambo jema kabisa ambalo hata Mimi GENTAMYCINE 'naliombea' litokee na najua kwa Mwenyezi Mungu hilo linawezekana na lolote laweza kutokea ila kwa Itikadi zetu zile za 'Kishirikina' na hasa 'Kuwahiana' kwa 'Kurogana' na 'Nyota' leo siyo Siku nzuri kwa Simba SC 'Kushinda' hivyo si vibaya tukijiandaa kwa lolote lile.

Yanayoweza kutokea leo Uwanjani hasa katika 'Mechi' hii ambayo nayo pia yatakuwa yamechangiwa au yanachangiwa na 'Ushirikina' ni kwamba kuna uwezekano Wachezaji wa Timu Mbili wakapewa Kadi Nyekundu au wa Timu Moja au Mchezaji 'Tegemeo' wa TImu Moja 'Kuumia' vibaya. Pia kuna 'Penati' itatolewa na 'Vurugu' kubwa kutokea kwa Wachezaji Wote.

GENTAMYCINE namalizia kwa Kuwatakieni Utizamaji mwema wa 'Mtanange' huu muhimu ila tambueni kuwa lolote laweza kutokea Taifa msiogope.
 
Hapo umenena kuumia kwa Lamine kumetutoa Yanga kwenye ushindi kabisa, mkuu umetabiri vema kabisa. Big up
Akhsante na tupo pamoja Mkuu wangu japo najua Watu tena Wapumbavu na Wapuuzi wengi walidhani GENTAMYCINE nilikuwa ninatania tu hapa.
 
iyo nimeikubali aisee ,umelenga mulemule kweli inaonekana umebobea
Nina uhakika ingetokea ndivyo sivyo huu 'Uzi' hadi hivi sasa ungekuwa na Kurasa hata 20 kwa Watu 'Kuuchangia' kwa 'Kunichamba' ila nimeupatia.
 
Back
Top Bottom