Ninapata wasiwasi wa kuoa

Ninapata wasiwasi wa kuoa

Kuna options mbili tu duniani KUOA au KUOLEWA!
Maadam umeshaogopa ya kwanza?basi ya pili inakuhusu!kila la kheri
 
Kama una kazi na unaingiza kipato yaani una uhakika wa kupata Tsh. 10000 kila siku tafuta binti mtulivu oa brother japo utumie akili tu broh.
 
Napata wasiwasi ya kuoa kutokana na haya ninayo yaona kila siku kwenye mtandao kuhusu maisha ya wana ndoa
Kila siku lazima nikutane na post ya watu kuachana wengine kufumaniana wengine kulea watoto ambao sio wao
Dah sijui tukimbilie wapi sisi kutafuta wanawake tutakao dumu nao
Tafuta stori nzuri pia usome. Huko ndo utajifunza.
 
Wikiendi iliyopita nimeshuhudia harusi 4. Hii ina maana kuwa watu bado wanaoa.

Usitishwe na utopolo wa mitandaoni humu ambamo kila mtu yuko huru kujiandikia cho chote anachotaka hata kama ni uwongo.

Muombe Mungu sana Akuletee mwanamke mwenye sifa unazozitaka halafu oa ufurahie ndoa yako. Changamoto zitakuwepo lakini kama utakuwa umepata mtu sahihi mmekuwa washikaji sana mengine yote mtayavumilia....

Usiogope!
Umemaliza bro.
 
Napata wasiwasi ya kuoa kutokana na haya ninayo yaona kila siku kwenye mtandao kuhusu maisha ya wana ndoa
Kila siku lazima nikutane na post ya watu kuachana wengine kufumaniana wengine kulea watoto ambao sio wao
Dah sijui tukimbilie wapi sisi kutafuta wanawake tutakao dumu nao
Achana na maisha ya maigizo ya mitandaoni,ishi maisha yako halisi,aishi maisha yake halisi,achana na wafanya maigizo ya maisha.Ukishindwa hilo maisha yalishakushinda🤔
 
Back
Top Bottom