Ninapata wasiwasi wa kuoa

Ninapata wasiwasi wa kuoa

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,788
Reaction score
5,027
Napata wasiwasi ya kuoa kutokana na haya ninayo yaona kila siku kwenye mtandao kuhusu maisha ya wana ndoa
Kila siku lazima nikutane na post ya watu kuachana wengine kufumaniana wengine kulea watoto ambao sio wao
Dah sijui tukimbilie wapi sisi kutafuta wanawake tutakao dumu nao
 
Napata wasiwasi ya kuoa kutokana na haya ninayo yaona kila siku kwenye mtandao kuhusu maisha ya wana ndoa
Kila siku lazima ni kutane na post ya watu kuachana wengine kufumaniana wengine kulea watoto ambao sio wao
Dah sijui tukimbilie wapi sisi kutafuta wanawake tutakao dumu nao
Kunywa maji mengi kisha muone Dr. Mariposa

Atakusaidia
 
Napata wasiwasi ya kuoa kutokana na haya ninayo yaona kila siku kwenye mtandao kuhusu maisha ya wana ndoa
Kila siku lazima nikutane na post ya watu kuachana wengine kufumaniana wengine kulea watoto ambao sio wao
Dah sijui tukimbilie wapi sisi kutafuta wanawake tutakao dumu nao
Mchumba wako anaandika xaxa badala ya sasa? Kama jibu ni ndio atagongwa sana na wajinga wajinga.
 
Wikiendi iliyopita nimeshuhudia harusi 4. Hii ina maana kuwa watu bado wanaoa.

Usitishwe na utopolo wa mitandaoni humu ambamo kila mtu yuko huru kujiandikia cho chote anachotaka hata kama ni uwongo.

Muombe Mungu sana Akuletee mwanamke mwenye sifa unazozitaka halafu oa ufurahie ndoa yako. Changamoto zitakuwepo lakini kama utakuwa umepata mtu sahihi mmekuwa washikaji sana mengine yote mtayavumilia....

Usiogope!
 
Moja: Omba Mungu akupe mwanamke mwenye utu na utulivu pia awe na hofu ya Mungu

PiLI: Toka nje ukiwa kwenye harakati zako tafuta huyo mwanamke, ukiona ana sifa za mwanzo kama mavazi ya staha, upole usoni nk wewe tongoza. But anaweza kuwa sio sahihi pia ukishakuwa nae ila Kuna % kubwa ukichagua hivyo unaweza pata aliye na Utu na utulivu

Tatu: akiwa na hivyo vigeo mpende, mjari...Care, mpe attention nk...Then achia mapenzi yajieneeshe automatic

Ukifanya hivyo Kuna % kubwa ya kupata mke sahihi, kumbuka mke sahihi ni yule anayeishi na wewe kwenye shida ya kiuchumi, kiafya, kijamii na anayejua kuishi Kutafuta mwisho mwema ukiwa na mwanamke wa hivyo ngumu ngumu Sana kukutana na hizo changamoto ulizotaja

Kupata mwanamke wa hivyo sio rahisi Mimi nahisi sasahivi huyu niliyempata anasifa hizi zote
 
Back
Top Bottom