Ninaomba MDAHALO wa kisiasa na Nape Nnauye

Nimeona janja ya CHADEMA kumkimbiza Nape mitandaoni hasa JF.......Nape plz hilo ni tego la mwizi, kula kona au kuwa tayari kunasa, huyu Yerico ni hatari sana........weka mbali na siasa za kizee

Hehee mkuu mimi sio mtu hatari kama unavyofikiri, bali ni mimi ni mjenzi imara wa siasa za kisasa!
 
Nape aruhusiwe kuwa na mamluki ili wamsaidie so that at least huo mpambano ufike raundi ya 4. Yericko usimnock out mapema waajiriwa wake hawataona weupe wake. Ila kamanda all the best man!
 
kwani hujasoma hapo juu??
Inasemekana bwana Nnauye Jr atagawa id kwa
mwingine ha ha yericko anaweza akawa anafanya mdahalo na watu 12.aisee
Invisible na Fanga
saidieni hii makitu mchezo mchafu usifanyike hapa.
Na vile kuna uwezekano wa kuwa na group la vijana kawakodisha na
kuwalipa kwa kazi hii.
Bravo Yericko Nyerere

This is serious, Honestly tutahitaji justfications who is behind the PARTICULAR ID ... Kabla ya take off!
 
Last edited by a moderator:
Napendekeza huu
mtanange ufanyike jumatano 26/12/2012, siku ya kufungua vifurushi ili
wote kwa pamoja, waliopata vifurushi jana yake na wasiopata tujumuike
siku hiyo kuvifungua kwa mdahalo.

Pia nampendekeza AshaDii aongoze mdahalo huu,
nadhani anaweza kuumudu huu mpambano.

... have the same opinion!
 
Last edited by a moderator:
Nape aruhusiwe kuwa na mamluki ili wamsaidie so that at least huo mpambano ufike raundi ya 4. Yericko usimnock out mapema waajiriwa wake hawataona weupe wake. Ila kamanda all the best man!

Hehehee naamini Nape anauelewa mkubwa wa siasa za nchi hii, ukiondoa cheo cha kipropaganda alichonacho, Nape ni mwanasiasa zaidi ya watu wanavyomfikiria!
 
Nashukuru Yericko,
Kwanza nipo nje ya Tanzania mpaka January tukipanga muda tukubaliane kwa
kuzingatia tofauti ya masaa...tunatofautiana masaa nane na nyumbani
Tanzania.
La pili nakubaliana tupate mtu ambaye anafahamika hapa kwa jina lake na
is kivuli kama wengi wanavyofanya.

La tatu tuje kuzungumza hoja za nchi/vyama na si hoja binafsi(personal
attack)... Baada ya hapo karibu kwa mapendekezo

...Cant believe this NAPE hongera sana kwa kuwa serious na hii mechi/ngoma ...
nafikiri Jf kuna uzoefu juu ya conditions unazozitaka. just reffere
MDAHALO WA ZZK! WAS REAL NOBLE AND CREDIBLE .... !
 
Boss Nape sikujua kama uko nje ya nchi, nilipendekeza mdahalo ufanyikie Clouds FM kwenye kipindi cha Jahazi sababu ndio uwanja wako wa nyumbani na pia ingeepusha kuwa na too many typing errors, lakini kama unadai uko conforable kufanya mdahalo hapa naomba ututhibitishie kwamba hautagawa ID kwa mtu mwingine.

Nilikua napitia reply zpte za Post hii...nikiangalia kama kunamtu ameliona hilo...nimekuna ndugu..pigia mstari.


Yeriko nyerere, jiandae mdahalo na jopo la CCM sio nape watapangwa watu maalamu..na sio Nape..huyu hawezi ku debate na wewe Mkuu.

Thanks siku hiyo nasikiliza hoja lkn sifikirii kama una dahalo na nape bali CCM special team.
 
Kwa Sababu Marope hayupo tenaa, ndo maana kakubali, Looks like Jangili Mmogadishu katoa a go ahead
 
Ili kuimarisha siasa Tanzania tena siasa za kisasa na zenye mafaa, Kwaheshima na taadhima ninaomba KESHO siku ya JUMAPILI au siku yoyote itakayipendekezwa tufanye mdahalo wawazi hapa jf na ndugu Nape Mnauye katibu Mwenezi wa CCM!

Ningependekeza mdahalo huo uhusu mambo makuu matatu!

1) Katiba za Chadema na CCM,

2) Katiba ya Tanzania (maeneo yahusuyo vyama vya siasa)

3) Sera za vyama hivi,

Ninafanya hivyo nikiwa kama muambata wa Chadema na mhafidhina wa siasa za machipuko!

Joto la kisiasa lililopo sasa hasa likiongozwa na siasa za ccm za kale na za kipropaganda zaidi, sisi tuendeshao siasa za mitandaoni na wanamikakati ya kisasa, tunapaswa kuilisha jamii siasa zenye mafaa!


Msimamizi wa mdahalo mnaweza kumpendekeza nyinyi wadau,


Ninaomba athibitishe hapa jukwaani kama yupo tayari kushiriki ama laa!

UPDATES:

Nimefurahi kuona ndugu Nape Nauye amekubali kushiriki mdahalo huu, na kulingana na maoni yenu wadau hapa, tumepanga jumatano tarehe 26/12/2012 saa tatu asubuhi kwa Tz na saa kumi kamili za jioni kwa eneo alilopo bwana Nape, mdahalo utaanza hapa JF ukisimamiwa na Maxence Mello.

Nape??? Huyu hawezi kujibu lolote, ni muoga wa hoja, huwa hajibu au kuchangia mijadala anayoanzisha. Sidhani kama atajibu hoja bila matusi. Ngoja tuone
 
Nipo, nasubiri

nape aliwaambia yupo nje ya nchi na tunatofautiana masaa nane. so mkisema muanze saa hizi mtakua mnamuonea sababu yeye bado ni usiku labda saa hizi kwake ni saa saba za usiku. mungemtaarifu kwa pm kuangalia kama yupo hewani. mia
 
Back
Top Bottom