Shahidi namba moja kwenye kesi ya ugaidi inayomuhusu Freeman Mbowe na wenzake, RPC Kingai umetuabisha kwa kuchanganya Maelezo yako huku ukiongozwa na wakili wako wa serikali
Je, RPC Kingai hukufahamu kuchanganya Maelezo yako utawafanya mashahidi wanaofuata washindwe wasimamie kitu gani habari za madawa ya kulevya au ugaidi?
Je, RPC Kingai hukufahamu wewe ulitangulizwa mbele ili uonyeshe uwezo wako wa kujenga hoja kama unavyojitanabaisha?
Je, RPC Kingai hukufahamu ushahidi unatolewa kwa kufuata hati ya mashtaka? Kwa uzoefu wako hukujua mahakamani ni moja ya sehemu ngumu sana, Hati ya mashtaka inaelezea ugaidi wewe unaongelea dawa za kulevya?
Je, RPC Kingai hukufahamu kukariri mambo kuna wenyewe, Ni watu wachache wenye uwezo wa kukariri mambo kwa dakika 15 bila kukosea ukiwaambia warudie walichokisema
Je? RPC Kingai hukufahamu kila jambo mahakamani unalotamka linahitaji kifungu cha sheria au maamuzi ya kesi zilizoamuliwa zamani na sio maneno matupu ya kukariri?
Je, RPC Kingai hukujua Sheria ni taaluma sio nguvu na mikwara inayotumika kuhoji watuhumiwa polisi?
Watu wengi wamehoji uwezo wa Polisi hasa wenye vyeo vya juu kusimama mahakamani na kujibu hoja za mawakili wasomi, Mara nyingi Polisi kwa uzoefu wamejiabisha mahakamani aidha kwa kukaa kimya au kujibu Sijui kila kitu
Tunasubiri Maelezo ya RPC Kingai yatakapotumika kumuuliza maswali Yeye mwenyewe, Hakika Itakuwa aibu kubwa sana
We are still waiting