Ninakulaumu RPC Ramadhani Kingai kwa ushahidi unaoleta utata kwa Taifa

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
184
1,000
Shahidi namba moja kwenye kesi ya ugaidi inayomuhusu Freeman Mbowe na wenzake, RPC Kingai umetuabisha kwa kuchanganya Maelezo yako huku ukiongozwa na wakili wako wa serikali

Je, RPC Kingai hukufahamu kuchanganya Maelezo yako utawafanya mashahidi wanaofuata washindwe wasimamie kitu gani habari za madawa ya kulevya au ugaidi?

Je, RPC Kingai hukufahamu wewe ulitangulizwa mbele ili uonyeshe uwezo wako wa kujenga hoja kama unavyojitanabaisha?

Je, RPC Kingai hukufahamu ushahidi unatolewa kwa kufuata hati ya mashtaka? Kwa uzoefu wako hukujua mahakamani ni moja ya sehemu ngumu sana, Hati ya mashtaka inaelezea ugaidi wewe unaongelea dawa za kulevya?

Je, RPC Kingai hukufahamu kukariri mambo kuna wenyewe, Ni watu wachache wenye uwezo wa kukariri mambo kwa dakika 15 bila kukosea ukiwaambia warudie walichokisema


Je? RPC Kingai hukufahamu kila jambo mahakamani unalotamka linahitaji kifungu cha sheria au maamuzi ya kesi zilizoamuliwa zamani na sio maneno matupu ya kukariri?

Je, RPC Kingai hukujua Sheria ni taaluma sio nguvu na mikwara inayotumika kuhoji watuhumiwa polisi?

Watu wengi wamehoji uwezo wa Polisi hasa wenye vyeo vya juu kusimama mahakamani na kujibu hoja za mawakili wasomi, Mara nyingi Polisi kwa uzoefu wamejiabisha mahakamani aidha kwa kukaa kimya au kujibu Sijui kila kitu

Tunasubiri Maelezo ya RPC Kingai yatakapotumika kumuuliza maswali Yeye mwenyewe, Hakika Itakuwa aibu kubwa sana

We are still waiting
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,672
2,000
Matumizi makubwa ya nguvu kwa jeshi la polisi yanatokana na uwwezo wao mdogo. Sasa kama RPC ndio anaongea ule utoto, hao anaowaongoza ni wajinga kiasi gani?

Ndio maana watawala inakuwa rahisi kuwaagiza polisi kutenda nje ya sheria, kwani wengi ni wajinga na hawana uwezo wa kuhoji, bali kutii kila kitu ili wapate upendeleo wa kupanda vyeo wajitajirishe kwa rushwa.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,765
2,000
Matumizi makubwa ya nguvu kwa jeshi la polisi yanatokana na uwwezo wao mdogo. Sasa kama RPC ndio anaongea ule utoto, hao anaowaongoza ni wajinga kiasi gani? Ndio maana watawala inakuwa rahisi kuwaagiza polisi kutenda nje ya sheria, kwani wengi ni wajinga na hawana uwezo wa kuhoji, bali kutii kila kitu ili wapate upendeleo wa kupanda vyeo wajitajirishe kwa rushwa.
Aibu kubwa sana !
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom