Mimi sio mdini lakini huwa nikiona mtu anatafuta mchumba/mke halafu anasema dini yoyote???? Mi sijui namchukulia je?? Manake Imani kwa Mungu, jinsi ya kuabudu, na utamaduni wa kidini kwangu mimi ni moja ya mambo yakuangalia kwa mtu ninayefikiria anaweza kuwa mke/mume.
Ni mawazo yangu tu!! Yawezekana nikielimika zaidi naweza kubadilika, lakini nahisi nina kamsimamo fulani juu ya hilo.