Ndugu wana wa TANZANIA HABARI, Huwa mara nyingi nimekuwa Mbishi sana Kuamini Mambo ya Kishirikina Lakini kwa Hili MHh! nalazimika Kuamini Kuwa ‘sio bure sisi Tumelogwa na Tunahitaji Mganga Haraka inavyo wezekana kupata tiba'. TAZAMA Kinyanambo‘C', Itimbo, Ihalimba, Nundwe, Vikula, Ugesa, Usokame, Kibengu, Mapanda, Mtili, Ifwagi, Ludilo, Ilasa, Ifupila, Itona, Mdabulo, Ikansa, Ihanu, Kilosa Mfindi, Ibwanzi, Lulanda, ECP, Iyegela, Ikaning'ombe, Luhunga, Igoda, Mkonge, Sawala, Mlevelwa, Mtwango, Ngalanga, Matanana, Kibidula, Sao Hill Village , Nzivi, Nyololo, Ngwazi, Igowole, Mninga, Kibao, Kitasengwa, Mwitikilwa, Kihansi.
Ilundi na Wami ni robo tatu ya vijiji vyote hapa Wilaya ya Mufindi ambavyo MITI hustawi na kushamiri kwa kiwango kikubwa sana na kufanya vijiji hivi kuwa muhimu sana kwa biashara ya Mbao hapa Wilaya ya Mufindi lakini cha kushangaza Wahehe wanao ishi katika vijiji hivi ni Masikini!, Masikini!, Masikini! kupindukia kitu kinacho nifanya kuhisi huenda wakawa wamelogwa hawa kwa kuwa uchumi wanao na wameukalia Kwa mujibu wa tafiti zilizo fanywa na chama cha Wafanya biashara wa Mbao Wilaya ya Mufindi ‘SAFIA' ni kwamba kama uwekezaji wa kutosha ungefanyika katika Mashamba haya ya Miti ,Wilaya ya Mufindi ingekuwa Kiongozi wa soko ‘Market leader' wa soko la Mbao Afrika Mashariki na Kati lakini kwa sasa soko hili linatoshelezwa kwa asilimia kumi na moja tu, na
Serekali haijali juu ya Fursa hii ya Uwekezaji na imekaa kimya ‘Sio Bure sisi tumelogwa' Inakadiriwa kuwa kwa sasa Biashara ya mbao hapa Wilaya ya Mufindi inaajiri watu zaidi ya 1,500,000 ikijumuisha wafanyakazi wa serekali, wafanyabiashara na Vibarua na kama Uwekezaji utaongezeka kwa angalau mara mbili ya sasa basi Biashara hii ya mbao hapa wilaya ya Mufindi itaajiri zaidi ya watu 5,000,000. Lakini serekali hailioni hili na hapo ndipo ninapo hisi ‘Sisi tumelogwa'. Katika taarifa yake ya mwaka 2012 Shamba la miti la GREEN RESOURCES inaeleza kuwa ni Maajabu kusikia Tanzania inanunua Nguzo za Umeme Afrika ya Kusini wakati nguzo hizi zinapatikana Wilaya ya Mufindi kwa wingi! kwangu mimi haya si tu maajabu ila ninahisi ‘sio bure sisi tumelogwa'
Maono yangu ni kuwa Serekali inalazimika kutafuta kiasi cha Shilingi Bilioni 500 zinazo hitajika kuwekezwa na SHAMBA LA MITI LA SAO HILL Kupitia wizara ya Mali asili na Utalii ili nusu ya Maeneo yote yanayofaa kwa uwekezaji wa miti hapa Wilaya ya Mufindi yamilikiwe na Serekali, Lakini tangu Mradi huu ulipo anzishwa serekali imeshindwa kuwekeza fedha za kutosha na hapa ndipo ninapo hisi sio bure sisi tumelogwa kwani sio rahisi kuamini eti serekali imeshindwa kutafuta shilingi bilioni 500 hata kwa kukopa! Pia nilitegemea Serekali ingewekeza katika Mazoa ya Miti hapa Wilaya ya Mufindi kupitia Kikosi cha Jeshi cha JKT MAFINGA lakini maeneo mengi yanayo Milikiwa na Kikosi hiki yameachwa bure yakingoja ‘Miujiza ya Mwenyezi Mungu' na kwa mujibu wa kanali Mstaafu MLAI na Kanali MMARI ambao walikuwa wakuu wa kikosi hiki kwa nyakati tofauti ni kwamba Kikosi kinahitaji Shilingi Billioni 100 ili kuwekeza katika mashamba yote yanayo milikiwa na kikosi na wanadai kama hizo fedha zingepatikana basi kikosi kingekuwa na uwezo wa kusambaza Nguzo za Umeme Afrika nzima lakini serekali imeshindwa kupata hizo fedha ‘Kwa kweli sisi Tumelogwa!'
Na nilidhani ni sahihi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Kuongeza uwekezaji wake katika Mashamba ya Miti Halmashauri hii imewekeza kwa asilimia 2.5 tu katika Miti, Ninachoka kusikia Eti kuna Shule nyingi za kata hapa wilaya ya Mufindi hazina madawati ‘Kweli kwenye miti hakuna wajenzi!' na kweli sisi tumelogwa na sielewi madiwani wetu wanawakilisha nini kwenye Baraza la madiwani kama wameshindwa kuwekeza hata kwenye miti japo kwa asilimia 10 tu na ikizingatiwa rasilimali hii inapatikana MUFINDI kwa kiwango kikubwa! Ni kwamba inasadikika kuwa iwapo Uwekezaji wa kutosha ukifanyika katika Mashamba ya Miti hapa Wilaya ya Mufindi kupitia SAO HILL, JKT MAFINGA, GREEN RESOURSES, HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI NA ZAIDI WAWEKEZAJI WADOGO WADOGO ,Tanzania inauwezo wa kuzalisha Shilingi Trilion 15 kwa miaka nane kwa kuuza Mazao ya Miti kama Magogo,Mbao na Hewa ya Ukaa.Pia Mazao haya yanaweza kuajiri hadi watu Milioni 7 kwa miaka 8 lakini serekali hailioni hili na hapa naamini SISI TUMELOGWA!
' Am Signing Out'