Ninadhani nina ugonjwa wa kisukari

ChidyB

Member
May 3, 2012
13
1
Mimi nina umri wa miaka 19 nipo form 5. Ila inaniwia vigumu kuendelea vizuri na masomo kwa sababu za kiafya, ninahisi nina kisukari japo sijapima ila dalili zote ninazo kama miguu na mikono kufa ganzi, sometimes kuishiwa nguvu na jicho la kulia hushindwa kutazama jua kali.

Ninaomba mnisaidie ushauri jinsi gani ya kulihandle gonjwa hili hali nipo boarding ambapo chakula kikuu ni ugali maharage sometimes wali ambavyo vyakula vyote ni wanga na ninavyojua mgonjwa wa kisukari hatakiwi kula vyakula vya wanga kwa wingi.

Naombeni pia mnijuze gharama ya vipimo vya kisukari pia hospitali ipi niende kwa uhakika zaidi, nipo Dar. Naombeni mnisaidie ndugu zangu ili niweze kufanya vizuri katika masomo na ikizingatia nipo PCM ambopo masomo yanahitaji muda mwingi wa kusoma ilhali mimi muda mwingi huwa nakosa raha ya kusoma hasa pale ninapohisi ganzi imenishika, kwani hunitokea kila siku.

Nisaidieni jamani.
 
Unahisi kisukari.................. japo hujapima. Jibu ni rahisi, nenda kapime.

dalili zote zipo cdhani kama kuna tatzo linaloweza kusababisha ganzi na macho kushndwa kuona vizur zaid ya kisukari, ila kupima ndio lengo ndio maana nikaulizia bei ya vipimo ili nijipange.
 
kwani ulikua unakula sukari(joke) mbona upo mdogo mana kisukari kinawapata wazee.Alafu usisahau kufanya Check up ya Blood pressure mana hayo magonjwa huwa ni baba na mwana mida mwingne.
 
Dah, i can feel ur pain..pole sana chidy,utapata tu ushauri mzuri,vuta subra akina dk Riwa watakuja
 
kwani ulikua unakula sukari(joke) mbona upo mdogo mana kisukari kinawapata wazee.Alafu usisahau kufanya Check up ya Blood pressure mana hayo magonjwa huwa ni baba na mwana mida mwingne.

Mdogo!!! si kweli kabisa. nimeshashuhudia mtoto wa 8years ana chronic kisuksri,yaani mpaka kanajua kujifanyia test home na kujichoma sindano. its so painful jamani ukikaona. ikipanda yaani mpaka anapauka mwili.

mi naona aende hosp kwanza.
 
Kapime upate uhakika.......acha kuhisi na kuanza kuogopa........yawezekana wala huna kisukari!
 
My sista Kiukweli nina uhakika ni kisukari kwani kila dalili zinazotajwa mimi ninazo of coz ntapima ila nawaza jinsi gani ntaishi na hali hii shule na ntamudu vp masomo i need advice plz

Pole ila nenda kapime afu upate uhakika then ukihakikisha mie ntakwambia nini cha kufanya serious tena wala usiwe na woga!
 
Dogo acha uoga. kapime kama unavyoshauriwa . wapo wataalamu humu JF wa kukusaidia . kupima ni pesa ndogo tu Tshs 3000/=
 
Niambie umetofautishaje na hyperthyroidism coz symptoms zinafanana, ukisoma kidogo tu unaona kila ugonjwa unao, hujasoma ukimwi nao utahisi pia unao. Ungekuwa unasoma medical school ningesema una medical students syndrome
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom