Ninachokitabiri kwa huyu muuza madawa ya kulevya

Ninachokitabiri kwa huyu muuza madawa ya kulevya

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,662
Ni miaka minane sasa huyu bwana mdogo tangu nianze kumfahamu kipindi hicho akifanya biashara ya mbao na bangi kwa wakati mmoja.

Siku nilipofika kwake kwa mara ya kwanza kununua mbao nilikuta vijana wengi wapole na wastaarabu wakinikaribisha utafikri ndio wenye mji. Chini kidogo ya nyumba yake lilikuwepo shimo huku likiwa na mti mkubwa wenye kivuli nako pia niliona vijana wamejilaza baada ya kutumia bangi kadiri ya dozi yao.

Nilipata nafasi ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa kijiji pia mwenyekiti wa kijiji akanichagua kuwa mmoja wa washauri zake. Siku moja palitokea wizi wa kuvunja milango na familia sita zikaibiwa mali zote hadi magodoro,tulipofanya utafiti tuliona chanzo ni vijana wale wapole kwa yule jamaa.

Tulimuita ofisini na kwa kauli moja tulimtaka afunge hiyo biashara na aangalie kazi nyingine tofauti na uuzaji bangi. Katka hali iliyotuacha hoi wajumbe ni pale kwa ujasiri alituuliza;sawa mimi niko tayari kuacha sasa nifanye biashara gani?

Mwenyekiti,hii biashara yangu nimeifanya kwa miaka yote na nikilipia ushuru wa kila mwezi ofisini hata kituo cha polisi napo napeleka kwa mkuu leo hii kwa sababu ya chuki tu mnataka nifunge biashara yangu!? Haiwezekani.

Baada ya vuta nikuvute tulimuamuru ahame kijijini na atafute kijiji kinachoruhusu hiyo biashara. (nilifahamu hilo ni jambo lisilowezekana).

Baada ya miezi kama tisa huyu kijana alianza kuuza unga na bangi huku akipata wateja wenye hadhi za juu tena wakipaki magari yao pasipo woga wowote.

Baadae tulimuita tena kumuonya lakini sasa ameshajitanua na hadi sasa ana kikosi ambacho kikitaka kukuchomoa roho wanagusa tu unapotea. Katika hilo kundi kuna wanaokodiwa kuua iwe una bifu na mtu,unatuhumiwa uchawi n.k kwa malipo makubwa.

Jamaa yangu wa karibu ameniambia hivi sasa wameanzisha mfuko wa dharura(pesa) endapo mmoja wao akikamatwa basi hizo pesa itatumika kumtoa jela.

Mimi mwenyewe nimeamua kuulinda moyo wangu kwa kuufyata na namtabiria baada ya miaka mitano mbele atakuwa muuzaji wa madawa mkubwa sana ukizigatia umri mdogo alionao na amekamatwa mara kibao mwaka huu hadi anapelekwa mkoani lakini hata wiki haiishi unamuona mtaani akitamba tu.

Kwa sasa naamini atakuja kuwa Elchapo Guzzman wa Shinyanga.
 
Tupia picha yake tumblacklist, au kama VP mpigie Kamanda Nzowa amzoweke!!
 
Kijijini chenu cha kishua sana.
Hadi unga unapatikana!
Tena magari mengi yanakuja kununua hapo!!
 
Huyu mtumbua majibu vijitu kama hivo havitamsumbua ila hofu yangu kwa wale wakina WASTAAFU NA WATOTO WAO JE ATAWEZA KUWATUMBUA ?????
 
Mmh Kama N Shinyanga Sawa Mi Nilijua Kahama Kwa Guzman Wa Kijijn Kama Huyo Unaye Muongelea Ambaye Anauza Kipimo Cha Kucha Ya Mwisho Wa Kidole Elfu 7,
 
Huo ni mzizi wa mtu aliekuepo juu sana haung'oki kirahisi ispokuwa chukua tahadhari usije kupewa wewe kesi ukapotezwa jumla.
 
wewe lazima utakuwa mchawi tu! sasa baada ya kijiji chenu kutokea tukio la wizi ni sababu ipi ilipelekea ukahisi walioiba ni wavuta bangi na sio walevi au watu wengine?
 
ajira zenyewe hakuna acha watu watajirike kwa kuuza unga #NO WRATH#.
 
Huyo ni mmoja tu mdogo wako wengi saana wameshashindikana ili uokoe maisha yako kaa tu kimya mwaya
 
Mmh Kama N Shinyanga Sawa Mi Nilijua Kahama Kwa Guzman Wa Kijijn Kama Huyo Unaye Muongelea Ambaye Anauza Kipimo Cha Kucha Ya Mwisho Wa Kidole Elfu 7,


Mkuu unajua kabisa jinsi anavyopima na bei yake!!!!
 
Kuna ndugu yangu "Babangu mdogo" alikuwa teja,alijihusisha na utumiaji wa unga huko Dodoma, kuna siku mwaka 2002 polisi walivamia mahali ambapo ndipo walipokuwa wakinunua huo unga na kuvuta,It means mateja wanaenda kwa jamaa wananunua ngada na kuvuta hapohapo. Siku hiyo polisi walienda na media kabisa,jamaa akakamatwa (yaani muuza unga) na wale vijana "mateja" kama saba hivi.
Kesi inaendaenda,yule muuza unga akawa amepata dhamana while wateja wake "mateja" walishindwa kukamilisha mashart ya dhamana.

Siku ya hukumu nikaenda mahakamani,mmoja wa mashahidi waliokuwa wakitoa ushahidi ni "MJUMBE/MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA" nilimskia akimwambia mheshimiwa hakimu kuwa "SIku ya tukio huyu bwana (muuza unga) hakuwepo kwake,polisi waliwakamata hawa hapa (mateja)". Ilhali siku ya tukio walikamatwa watu wote (mateja na mzungu wao). Kweli hukumu ikasomwa yule bwana "muuza unga" akaachiwa ikaonekana hatia hana,wale "mateja" waliokutwa kwa muuza unga wakahukumiwa miaka saba jela kila mmoja.

Mimi nikawa na jukumu la kwenda jela kumuona ndugu yangu kila weekend,kwa ajili ya kupeleka sabuni na mahitaji mengine. Ikatokea jamaa (ndugu yangu) akaanza kuumwa kule jela,nikaleta taarifa nyumbani,hali ikawa mbaya sana,akapelekwa hospitali chini ya uangalizi wa magereza, bahati mbaya jamaa alifariki,kumbe walikuwa wakishare mabomba ya sindano so wakaambukizana UKIMWI kwani kati yao watu wawili walifia gerezani by then.

Baada ya muda nikajaribu kufatilia mwenendo wa huyo "Mzungu" ukweli amejitanua sana kwa sasa sio kwamba anatambulika mtaani bali mji mzima na ameongeza wadau wanaomsaidia biashara hiyo.
Kiufupi nimetoa mfano wa ndugu yangu mmoja tu aloathirika kwa UNGA.Kwa lugha nyingine nami ni MUATHIRIKA WA UNGA maana I lost my relatives.
 
Mkuu unajua kabisa jinsi anavyopima na bei yake!!!!
Kwa muda nimekua nikifatilia juu ya biashara hii,maana uzuri inafanyika uswahilini na ushuani. Nimekua nikiwahoji wadau na hata mateja,wanakueleza jinsi mzigo unavyoingia aidha kwa bahari au kwa ndege pale AIRPORT, haiishii hapo, hata namna ya kuficha,jinsi wanawake wanavyoficha, mwanamke ana uwezo wa kuingiza mzigo mkubwa sana kupitia PAPUCHI YAKE,lakini huwa najiuliza kama raia wa kawaida najua mamlaka husika hazijui?

Bagamoyo inasemekana ni moja ya chaka ambalo mzigo huingilia sana,let say mzigo ukipakiwa kwenye landcruiser nani atakauejua?
 
waanza na yule kijana wa kiranja mkuu ambaye ameacha kazi majuzi..hivi vidagaa vitapotea
 
Ngoja tuanze kuwashushia non do kama zamani kuhusu hii biashara ya ngada naona kuna watu hawajui kiundani kuhusu hii biashara!
Na ugumu na vikwazo vyake wanavyopata wale wanaotaka kudhibiti hii biashara
 
Back
Top Bottom