Ninachokiona, watu wengi wanachukulia mapenzi seriously

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,480
Wasalaam

Katika harakati za maisha nimejikuta nikienda sehemu nyingi na kukutana na watu wengi sana. Sehemu kubwa ya watu ninaokutana nao wana matatizo makubwa ya ki-mahusiano; wanaume kwa wanawake.

Hadithi ni nyingi sana, na heka heka ni nyingi sana pia. Kimsingi, watu wamevurugwa, wanachukulia mapenzi seriously. Kila kukicha ni visa na mikasa tu, mara huku fumanizi, mara kule mauji kama siyo kunywa sumu. Mapenzi yana wasumbua sana watu, yanapoteza sehemu kubwa ya uwezo wa binadamu wa kufikiri sahihi na kuchakata namna sahihi ya kusongesha maisha.

Ngoswe (penzi kitovu cha uzembe) ni riwaya yangu ya kwanza kunifikirisha hatari ya mapenzi kama hauna uwezo wa kujiratibu. Kimsingi, mapenzi siyo kwa kila mtu, ni kwa wale wenye ukomavu wa akili tu. Tafiti za mchongo zinaonesha, watu wengi makini walikwisha achana na mambo ya mapenzi wako busy ku-pursue ndoto zao.

Leo nataka nichochee tafakari yako juu ya mambo yafuatayo:

Kwanini una penda? je kuna ulazima wa kufanya hivyo?

Ukiachilia wadangaji na marioo, mapenzi yana faida gani kiuchumi?

sipokua kwa habari ya nyege, je kuna ulazima wa kumfuga mtu (mke au mume) na kushi nae?

Kwani huyo mpenzi wako anayekuchetua, ulizaliwa nae au utakufa nae?

je unajua huyo mpenzi wako alikua ni mpenzi wa mtu mwingine na aliachwa?

Unapaswa kujua pia, kama alikupenda wewe, nafasi iko akampenda mtu mwingine mwenye quality za juu zaidi yako;

Twendeni taratibu, msichukulie mapenzi seriously, fanya unachoweza kufanya, kila mtu ana objectives zake kwenye mahusiano, timiza zako angalia ustaarabu wako.

Nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom