Ninachokiona kwa Wanaowania Ubunge wa EALA sasa ni ushindani na madoido ya kuongea Kiingereza tu, vichwani hakuna kitu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,721
109,155
Naomba miaka ya baadae (mbeleni) huko nje ya kuwataka Wagombea wawe na Elimu Kubwa ila pia wawe Wanapimwa kama ni Werevu Kiuhalisia kwani kuna tofauti Kubwa mno kati ya kuwa Msomi (Intellectual) na kuwa Mwerevu (Intelligent) lakini bahati mbaya kwa Tanzania yetu Msomi anajumlishwa kuwa nae ni Mwerevu.

GENTAMYCINE nawatizama hawa Wateuliwa wa CCM ambao wanataka Kugombea Ubunge wa EALA wakijinadi mbele ya Wabunge na ninachokiona hasa ni Kushindana tu kwa Uhodari wa Kuzungumza Kiingereza kwa Mikogo (Madoido) mengi lakini Mipango, Dira na Mikakati ya Kimantiki ya Kutekelezeka siioni Vichwani (Mibichwani) mwao.

Tunakwenda Kuaibika tu huko EALA!
 
Hilo mpaka kwenye Bunge la JMT

Asilimia kubwa ya wabunge ni vilaza kabisaaa

Yaan mule kupata Mbunge asimame uone anatoa mchango wa kutukuka, mchango chanya wenye Kusaidia Taifa, na SHERIA BORAA

Ni WA kutafuta, ndo unawakuta Akina Luhaga Mpina, Gwajima, na wachache sana .

Nadhan Mfumo Wetu wa Elimu una shida sanaaa na wanaosoma pia Wana shida sana.

Sishangai Vijana kabla ya Intavyuu utasikia "Jamaan naomba msaada wa Maswali yanayoulizwa kwenye Uswahili wa Taasisi XYZ".

Unajiuliza, hivi huyu kijana kama amesoma, na alichosoma kipo kichwan, inakuaje anataka kuingia Kwa Intavyuu kichwan akiwa na Maswali na majibu yake ???

Yaan kwann mtu asiache Kichwa na akili yake kumfikiria na kuja na suluhisho .

Sasa Vichwa vya aina hii, unategemea vitakuja na mawazo gani ya kukomboa Jamii???

Hamna!

UKWELI NI KWAMBA, WAZUNGU WAMETUZIDI AKILI MBALI MNOOO, HATA MATUMIZI YA HIYO AKILI, WAMETUZIDI MBALIIIII MNOO
 
Shida iko hasa kwa wabunge

Nyetere aliwahi hojiwa kwa nini anateua mawaziri vilaza ambao kabisa wanaonyesha akili hawana

Akasema Tatizo liko.kwa wapiga kura

Ukiweka Proffessor na mwingine darasa la saba kura za maoni wananchi wanampa kura darasa la saba wanamuacha Proffessor!!
Ndio.maana wengi wanaojua mambo hawagombei sababu wanajua watatemwa

Kwa mawaziri Nadhani katiba ibadilishwe Iwe kama Kenya Raisi ateue mawaziri toka mitaani sio bungeni

Mitaani atalanta watu sahihi wenye uwezo sana kuliko.hawa wabunge hopeless
 
BUNGE LA WAHUNI WATUPU WANAPIGA KELELE UTADHANI MITOTO YA CHEKECHEA.

MBUNGE ANAJIELEZA WAO WANAPIGA STORI TU HATA HAWAWASIKILIZI WAGOMBEA.

WANACHEZEA TU KODI ZETU, NATAMANI HAMZA AFUFUKE AWAFYEKELEE MBALI AU BIBI TOZO AVUNJE TU HILI BUNGE.
 
Naomba miaka ya baadae (mbeleni) huko nje ya kuwataka Wagombea wawe na Elimu Kubwa ila pia wawe Wanapimwa kama ni Werevu Kiuhalisia kwani kuna tofauti Kubwa mno kati ya kuwa Msomi (Intellectual) na kuwa Mwerevu (Intelligent) lakini bahati mbaya kwa Tanzania yetu Msomi anajumlishwa kuwa nae ni Mwerevu.

GENTAMYCINE nawatizama hawa Wateuliwa wa CCM ambao wanataka Kugombea Ubunge wa EALA wakijinadi mbele ya Wabunge na ninachokiona hasa ni Kushindana tu kwa Uhodari wa Kuzungumza Kiingereza kwa Mikogo (Madoido) mengi lakini Mipango, Dira na Mikakati ya Kimantiki ya Kutekelezeka siioni Vichwani (Mibichwani) mwao.

Tunakwenda Kuaibika tu huko EALA!
Sio tu kuaibika, ni kusindikiza! unakuwa tu msindikizaji wa chochote kilichopo unakubali na kuwa msindikizaji! Nimeliona hili pia
 
Back
Top Bottom