Ninachokichukia ndani ya Mabasi ya Safari

jay311

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
2,932
2,715
Rejea kichwa cha habari hapo juu...

Kwa bahati mbaya wakati wa kusafiri kwenda mikoani( mkoa to mkoa) huwa sifanikiwi kupata usingizi ndani ya basi,hivyo nalazimika kuwa macho/awake muda wote.

Mara nyingi huwa kwenye basi wanaweka entertainment kama muzic video na movie na hata bongo movie....

Guess what? kwa bahati mbaya tena mm sio mshabiki kabisa wa bongo movie,na pia huwa sipendi kutumia headphones kwa hiyo kwa njia yeyote ile ni lazima nitasikia tuh kelele za akina nani sijui wa bongo movie basi nachanganyikiwa tu nabakia kuangalia miti inavyorudi nyuma.

Isitoshe wale wahudumu wa mle ndani wanaweka music video za zaman kweli miaka ya 2000's na pia wanarudia miziki ile ile yani kwenye basi lao ,,,yaani flashdisk zao hawabadilishi mziki wala nn...kwa hiyo ukisafiri kwa express mwaka huu ukisikiliza nyimbo ya Mo music ujue kuwa mwaka 2017 pia ukipanda basi lile na mabasi mengine pia utasikiliza cd/flashdisk ile ile....

Yaani kusafiri inakuwa kama jela fulani hivi with no freedom....nachukia sana wanavyorudia movie zile zile za comedy mfano zulu au za jackie chan sometimes ni ile ile,hivi wanadhani kila safari wasafiri ni WAPYA?
 
mi mwenyewe nachukiaga hayo mamuvi,ya ajabu ajabu.bora waache kwasababu sio kila mtu anapenda muvi
 
Muombe mungu wako, akupe nguvu ufanye kazi kwa bidii ili uweze kununua kilimo kwanza ili iwe unasafiri privet, hakuna mtu atakupangia kumuangalia Mzee majuto
 
kunywa dawa za usingizi pia kumbuka kumwambia konda unashukia wapi. kero zote za bongo muvi, watu kutapika hovyo, watoto kulialia, dereva kukata kona ki ajabu ajabu na zile breki za ghafla utasimuliwa tu. ni kama time travelling
 
kunywa dawa za usingizi pia kumbuka kumwambia konda unashukia wapi. kero zote za bongo muvi, watu kutapika hovyo, watoto kulialia, dereva kukata kona ki ajabu ajabu na zile breki za ghafla utasimuliwa tu. ni kama time travelling
dawa za usingizi ni addictive sana
 
Muombe mungu wako, akupe nguvu ufanye kazi kwa bidii ili uweze kununua kilimo kwanza ili iwe unasafiri privet, hakuna mtu atakupangia kumuangalia Mzee majuto
hehe haya ,,,namuomba sana mungu, ila hata nikiwa na pesa kiaje,i still prefer bus to plane
 
Nadhani kulala sio hobby yako.

Ingekuwa ni hobby yako hata disco ungelala.
 
Kama ni mpenzi kusoma vitabu, jaribu kuwa navyo angalau
Kitabu kimoja unakisoma safarini, kukaa kwenye gari Masaa mawili hadi matatu inatosha kuongeza maarifa ya kutosha, kuliko kukaa Bure tu. Ukishindwa kitabu angalau basi gazeti.
 
Kwel kunywa dawa ya usingizi!!hata gari ikidumbukia mto wami huna habari,ukishtuka unajikuta mamba kashakula mguu kakuweka kiporo,pembeni ya mto!!

hahah kweli hamnitakii mema,,je nikinywa dawa ya usingizi halafu nione kichaka cha kukojolea nikiwa usingizin?
 
Back
Top Bottom