Ninaanza rasmi mgomo wa kulipa kodi

Ninaanza rasmi mgomo wa kulipa kodi

Umenikumbusha niliwahi kufanya manunuzi ya laki9.8 nikapewa risiti ya laki nikacheka sana.
Mimi karibia kila siku nafanya manunuzi yasiyopungua milioni 1, lakini cha ajabu risiti ninazopewa unakuta ni robo tu ya mnunuzi niliyofanya.
Mara nyingi nalazimisha kupewa risiti halali ila kwa mtindo huu hata mimi nitakuwa sidai risiti kabisa.

Haiwezekani tulipe kodi huku viongozi tuliowachagua wazitumie hovyohivyo huku wakitudharau

Zaburi 53.1 MPUMBAVU AMESEMA MOYONI MWAKE HAKUNA MUNGU
 
Tunaimbishwa neno Uzalendo huku watawala na watoto wao ndio wanafaidi nchi. Uzalendo my foot...!
 
Mimi karibia kila siku nafanya manunuzi yasiyopungua milioni 1, lakini cha ajabu risiti ninazopewa unakuta ni robo tu ya mnunuzi niliyofanya.
Mara nyingi nalazimisha kupewa risiti halali ila kwa mtindo huu hata mimi nitakuwa sidai risiti kabisa.

Haiwezekani tulipe kodi huku viongozi tuliowachagua wazitumie hovyohivyo huku wakitudharau

Zaburi 53.1 MPUMBAVU AMESEMA MOYONI MWAKE HAKUNA MUNGU
Kwakweli haina maana.
 
Dah...mleta Uzi naona Kama umezaliwa juzi...Kama ungekuwepo awamu zilizopita...kwa mawazo haya ....ungeishia kujinyonga kwa hasira[emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Umenikumbusha niliwahi kufanya manunuzi ya laki9.8 nikapewa risiti ya laki nikacheka sana.
Kuna siku nilinunua mabati ya mil 4 nikapewa risiti ya 1.5m....zamani nilikua nachukia. Ila kwa haya yanayoendelea namimi silipi. Na siku hizi sina PAYE hata hawanipati shenzi kabisa mapanya buku yamekula 1.5T kimya kimya. Halafu yanaimba ngonjera za uzalendo. To hell.

Sent using my Nokia Torch
 
Umenikumbusha machungu, leo kuna dogo wamemkamata wameenda nae mnaz mmoja kosa halipi kodi ofis yenyewe hata laki mbili za mtaji haifiki ni saloon kiti elf40 vile vya kuunga, mashine ya kunyolea elf30, kioo 40elf na benchi la kukalia wateja wamemwambia kila mwenye frem lazima alipe kodi na kaambiwa alipe 155400,sasa sijui watampeleka polisi manake wameenda nae,swali langu lipo hapa kama wanaotakiwa kulipa kodi wanatakiwa wawe na mitaji ya ml4 hawa wasiofikisha mitaji hiyo hela zao zinaenda wapi?na kwanini wasifanye hivyo kama sheria yao inavyosema? manake pale hivyo vitu vinahesabika hata kwa kukisia tu unajua hapa hakuna hata laki 3 mbona tunaoneana hivyo?mkuu tuko pamoja sitolipa kodi ya aina yoyote na mengine ntakayofanya najua mwenyewe .

tatizo lugha
 
Ndio, Kuna watu watakuja hapa na story zao za uzalendo wakijifanya wanaipenda Sana hii nchi huku wakiwa wamejificha kwenye kivuli Cha kutetea matumbo yao, Binafsi naanza mgomo rasmi wa kulipa Kodi maana sioni namna inavyonifaidisha Mimi na watanzania tulio wengi pamoja na kuwa na rasilimali nyingi hapa nchini.

Kuanzia leo nikikamatwa na traffic natoa pesa tu sitaki risiti, nikipanda mwendo kasi nitataka wanipe ticket used ifanikishe tu kunifikisha ninakoenda, nikienda ubungo nikilipa 300 sitaki ticket na nikinunua kitu chochote sitaki risiti ya aina yeyote ama nikifanya manunuzi kariakoo hata ya mamillion ya pesa nitawaambia wanipe risiti yenye gharama pungufu na niliyonunulia,nikienda shell najaza mafuta kwenye gari siombi risiti( ni bora hii pesa iliwe na wavuja jasho wenzangu, kuliko kuliwa na manyang'au wachache serikalini).

Sijaona Sera na watawala wenye uchungu na nchi hii wa kunifanya niwe mzalendo, hawa wapo kwa ajili ya matumbo yao na familia zao huku wakiimba pambio za uzalendo, Ukiwaona utadhani wanamaanisha wanachokiongea lakini kiuhalisia wanalinda maslahi yao.

KWA NINI NASEMA HIVI?

Nimejaribu kufuatilia maisha ya watanzania walio wengi hayafurahishi hata kidogo, wamechoka, wamekata tamaa hawaijui hata kesho yao.., maisha ni magumu kuzidi maelezo na hamna Sera nzuri za kibiashara na kiuchumi dhidi yao, wakiwa bado wanahangaika kutafta pesa angalau ya kula wanakutana na migambo wa jiji na tume ya mkurugenzi na mkuu inapita kukagua usafi, Hawa jamaa wanachojali ni rushwa tu wao wakikuta hata vikaratasi havijachomwa au majivu umemwaga pembeni wanataka elfu50 papo hapo au uwape rushwa kidogo wakuache na Kama huna wanakupeleka polisi ambapo wanaweza kukuambia uyachome au kuyasogeza na hali ikawa ya kawaida kabisa.

Angalia wakulima wa mahindi, kahawa, mbaazi, na Sasa korosho wameshafungwa mdomo hurusiwi kusema hujalipwa Tena, ukisema hujalipwa unapelekwa ndani.., huko mahospitalini watoto wwtu wa chini ya miaka5 na mababu zetu wanatakiwa watibiwe bure.. kaangalieni kinachoendelea huko.

Shule za serikali zimeshakuwa vituko, watoto wetu wanachokipata humo sio elimu tena na ndo maana hata hawa wanaotutungia mitaala na Sera hizi za elimu hawaruhusu watoto wao wakasoma hizi shule,

Kwa watumishi wa umma huko ndo Hali iko mbaya sana mpka Leo Kuna watumishi wa umma wanalipwa 260,000/= kwa mwezi kabla ya makato, wamewabagua kwa makundi watoto wa masikini utawakuta kwenye taasisi sizizolipa vizuri hizi za 260k, 300k,340k,400k,450k,650k,700k, na 820k na hawana allowance zozote zingine tofauti na mshahara, huku watoto na Hawa vigogo wakiwekwa kwenye taasisi za umma zinazolipa vizuri ambazo utakuta security guard tu anaanzia 1.5m na allowance Kama housing na transport wanapata, kwa Hali hii kwa nini niwe mzalendo?

Ndgu zangu vijijini wanachangia bwawa moja la maji ya kunywa na mifugo na huku budget ya waziri kutembelea zinduzi mbalimbali zisizokuwa na tija zinatosha kujenga visima zaidi ya10 vijijini, mshahara wa mkurungenzi na marupurupu yake kwa mwezi yanatosha kulipa mishahara ya kima chini Cha miaka 30 ya mtumishi wa taasisi hiyohiyo moja huku akiwa analipiwa kila kitu na huyu wa kima Cha chini hana Cha ziada zaidi ya mshahara, kwa nini nilipe Kodi?

Yanayoendelea huko PSSSF/NSSF yananiongezea hasira zaidi ya kutokulipa Kodi... Hapa namba one alicheza mchezo wa kuagiza akijua kabisa alichosema hakitekelezeki, ukienda kwenye hizi ofisi utawahurumia vijana na wazee wanaosubiria mafao Yao, wastaafu wanalipwa kwa kikotoo Cha asilimia 25 na vijana wanaambiwa waje baada ya kufikisha miaka55 kuchukua pesa isiyozidi mill5😀😎, Cha kusikitisha zaidi wengine hawakuwa wanachangia kisheria kwenye mifuko hii, walikuwa wanachangia kwa hiari Cha ajabu nao wanapata usumbufu mkubwa mno kupata pesa zao

Binafsi, sitaki kuwa mnafiki na mzalendo kwa watawala wanaofuja rasilimali zetu, na hata nikikuta mtumishi wa umma anakula rushwa ama anaihujumu serikali kwa vyovyote vile nitamsapoti, nina sababu nyingi za kufanya hivi kuliko kuwa mzalendo.

Angalia bunge la ndugai na CAG, wanamnyonga Assad ili wafisadi vizuri wakijifichicha kwenye koti la uzalendo, wanatetekeza mabillion ya pesa kwa kununua madiwani na wabunge na kugharamia chaguzi zisizo na tija.. kwa nini nilipe Kodi ikatumike namna hii?

Kuanzia leo nawasapoti watumishi Wala rushwa na mafisadi na wasiolipa Kodi kuliko mafisadi mapapa wanaojificha kwenye koti la uzalendo, wanajoiita watetezi wa wanyonge huku wakiwanyonga bila huruma, wanaoimba pambio za maskini huku wao wakiwa matajiri wa kutupwa....

Viongozi wakubwa ambao wanagharimiwa kila kitu na serikali ambao hawajui hata gharama ya kujinunulia chumvi ikoje, wakilipwa mishahara minono isiyokatwa PAYE, anatunga na kupitisha Sera za kukatwa Kodi mwenye mshahara wa 260k per month na asiye na allowance yeyote na akistaafu alipwe kwa kikokotoo Cha asilimia 25, huku yake akichukua kwa mkupuo.... Kwa Hali hii kwa nini nihamasike kulipa Kodi?

Mungu wabariki wakwepa Kodi wote
Kila la kheri katika jukum hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom