Nina wasiwasi na Dr. Joseph K. Buberwa

ney kush

JF-Expert Member
Feb 16, 2012
1,373
851
Huyu jamaa alikuja na gia ya dawa za kufanya wenye matatizo ya meno yasiwe na matatizo sasa sijui iliishia wapi.

Sasa kaja na program ya kutrack computer, simu sasa kwa upande wangu huyu jamaa namwona kama tapeli tu jihadharini wakuu.
 
nami nilimuona from a to z. walibanwa na swali la mshumbusi wa mtwara - lilijibiwa jujuu. kitu kingine ni kua segment ya watumia simu za china ambazo ni nyingi hapa nchini wataikosa kufuatana na maelezo yao - hivyo kibiashara wenye stationeries na cafe hasa mikoani si busara kukimbilia u agent wa biashara hii. pia nafikiri kuna msemo wa for every action there is a reaction. kadhalika polisi yetu imekuwa na technolojia hii kitambo - nakumbuka mtu alifanya uhalifu mbeya akabadili sim lakini alishikwa tanga kilaini wakiwasiliana nae muda wote kwa simu yake ikiwa na simcard tofauti tofauti.

nawasifu wamejipanga - website yao quite modest
 
nami nilimuona from a to z. walibanwa na swali la mshumbusi wa mtwara - lilijibiwa jujuu. kitu kingine ni kua segment ya watumia simu za china ambazo ni nyingi hapa nchini wataikosa kufuatana na maelezo yao - hivyo kibiashara wenye stationeries na cafe hasa mikoani si busara kukimbilia u agent wa biashara hii. pia nafikiri kuna msemo wa for every action there is a reaction. kadhalika polisi yetu imekuwa na technolojia hii kitambo - nakumbuka mtu alifanya uhalifu mbeya akabadili sim lakini alishikwa tanga kilaini wakiwasiliana nae muda wote kwa simu yake ikiwa na simcard tofauti tofauti.

nawasifu wamejipanga - website yao quite modest

Umeniacha njia panda, unawa-rcommend au, maana unasema, hawakujibu maswali vizuri as if ni wababaishaji, polisi wanayo muda mrefu halafu unasema wamejipanga vizuri! Which is which!
 
Umeniacha njia panda, unawa-rcommend au, maana unasema, hawakujibu maswali vizuri as if ni wababaishaji, polisi wanayo muda mrefu halafu unasema wamejipanga vizuri! Which is which!

Nilidhan me pekeangu ndo cjamuelewa
 
I know the Guy. He is doing fine. And very hard working with great aspiration.
 
Zile dawa za meno nilitumia mara moja tu na siku wahi kung'oa tena jino ingawa lipo lilitoboka lakini sina maumivu.Sijui kama ni ile dawa yake ama imetokea tu maana nilishatoa meno mawili kabla sijatumia.
 
Zile dawa za meno nilitumia mara moja tu na siku wahi kung'oa tena jino ingawa lipo lilitoboka lakini sina maumivu.Sijui kama ni ile dawa yake ama imetokea tu maana nilishatoa meno mawili kabla sijatumia.

Mkuu kama una contact zao hebu niwekee hapa!
 
TV ya taifa ni sehemu ya tunu za taifa. TV ya taifa inapata ruzuku toka serikalini hivyo basi inatakiwa kuonyesha mambo ambayo yana faida kwa taifa zima na siyo kutuonyesha harusi. Wameshindwa hata kuhamasisha usafi wa miji yetu ama hata kilimo wao wapo busy na ekotike! Niliona nikadhani ni chereko lakini lahaula nikaona ni live na inaendelea nikaamua kuangalia New castle v Villa na sasa namsikiliza kichaa wangu Buberwa na mambo yake. Haya mambo ya harusi wawaachie Channel 5.
Kwa kweli ni muda sasa ninawasiwasi na akili na utendaji wa tbc1 hivi kweli tv ya taifa haina vipindi mpaka wanaamua kuonyesha harusi live hii kwa kweli haikubaliki hili nalo ni jipu linahitaji kutumbuliwa mapema sana
Hao jamaa walichobakisha ni kurusha live kipindi cha wanandoa wakifanya tendo la ndoa...........
Kiukweli hili la televisheni ya taifa kurusha vipindi havina mantiki wala maana kwa walipa kodi linatia kichefu chefu kama sio kinyaa kabisa.......serikali kupitia wizara husika hawana budi kulishughulikia hili na kuwakumbusha majukumu yao kwa walipa kodi.......
Unaanzaje kurusha live harusi kupitia televisioni ya taifa ilhali kuna masuala kibao watanzania wanahitaji kuelimishwa kupitia hiyo hiyo TBC......
HERI HATA WANGEWEKA KIPINDI CHA KILIMO NA MAFANIKIO YAKE ILI KUWAVUTIA VIJANA WENGI WAACHE KUZURULA HUKU MIJINI.........

WANGEONYESHA HATA VIVUTIO VYA UTALII ILI KUWAVUTIA WATALII WA NDANI......YAANI KWA KIFUPI KUNA MENGI YA MAANA KWA MLIPA ANATAKIWA KUONYESHWA KULIKO HUO UPUUZI WA HILO LIHARUSI.......
NYAMBAF......
Wadau, kwanza naomba ku declare interest, kuwa sikubahatika kuiona hiyo live ya harusi binafsi ya mtu!. Pili mimi ni mdau wa broadcast jounalism, na niliwahi kufanya kazi TBC enzi zile ikiitwa TVT, ila hapa sichangii kama an authority by as an experience broadcast jounalist!.

  1. Naomba nitofautiane na wengi, kuwa TBC inaweza kuonyesha live ya kipindi chochote ambacho kinaonyeshwaga kikiwa recorded, hii inamaana kama TBC wanarusha kipindi cha Chereko, kikionyesha sherehe binafsi za watu, then mtu akifika bei, Chereko inaweza kwenda live kwenye event yoyote, iwe ni harusi, send off, kitchen party, ubarikio, au hata birthday ya mtu, provided ili live itatumia muda ule ule wa recored program, na kama itabidi ku extend time, isile muda wa more serious na relevant programs simply because mtu ana fedha za kulipia!.
  2. TBC nayo japo ni kituo cha TV kama vilivyo vituo vingine vyote vya TV, nayo inayo haki ya kufanya biashara, kama TV nyingine zote zinazovyofanya biashaa, na ina kipindi cha Chereko kinachoonyesha harusi za watu, then kama mtu ana pesa kulipia, then why TBC ikatae pesa?!, lakini suala la kurusha matangazo ya live, it is not about money on who can pay, but the contents and national interests, nadhani TBC wangeirusha hiyo live muda ule ule wa Chereko na baada ya hapo vipindi vingine vikaendelea kama kawaida, sidhani kama kungekuwa na any basis ya malalamiko, kwa sababu live social events za public figures, prominent people na super stars zinafanyika kwenye tv duniani kote japo not on public TV.
  3. Dr. Buberwa nimefanya naye programs, hana tofauti sana na Renatus Mkinga, au Mchungaji Mtikila (RIP), kuhusiana na soundness of the state of their minds!, hivyo kitendo tuu cha mtu kulipia live ya harusi yake alone, kilitosha ku sound alarm kuhusu tuning a pivate function into a state function, mimi ndio ningekuwa producer, ningekuwa very careful to make sure live inahusisha kuonyesha events tuu na kamwe nisingithubutu kurusha live kitu chochote atakachoongea Buberwa, unless producer huyo alidhani Dr. Buberwa is a normal person of a sound mind!, the truth Dr. Buberwa is insane!.
  4. Dr. Buberwa ni member mwenzetu humu jf, ila alipobainika tuu his state of mind kutokana na mabandiko yake, alifutwa na mabandiko yake yote yakafutwa!. Mtu yoyote mwenye sound mind can tell kwa kusoma mabandiko yake, the best way kuwasaidia watu kama hawa ni kufanya nao recoded programs only where there ae rooms for editing but not live!.
  5. Mwisho, hili la TV ya taifa kufanya biashara linahitaji mjadala wa kujitegemea, BBC World Service, haifanyi biashaa, na haipokei tangozo lolote la mtu yoyote zaidi ya public announcements, lakini iko funded 100% na public, mtu yoyote ukiisha kanyaga tuu ardhi ya UK, unailipia BBC utake usitake!, na sisi tufike mahali, TBC yetu iwe funded 100% ili isihitaji sentano ya mtu, na kugawa majukumu into diferent channels say TBC 1 iwe ni nationa interest, TBC 2 comercial, ifanya biashara, TBC 3, elimu, TBC 4, Afya, TBC 5 kilimo, uvuvi na ufugaji, TBC 6 watoto, TBC 7 michezo, TBC 8 miziki etc, etc.

Wajameni, mtu kuwa kichaa, sio lazima mpaka mtu aokote makopo!.

Pasco
 
Mi naona wa tz wengi ni type za akina buberwa sema wanatofautishwa na mikandamizo tofauti katk mazingira waish?yo.
 
kuna siku alishawahi kuongea hapa kwenye tv kwamba, akiwa mdogo alishawahi kuchanganyikiwa hadi wazazi wake walimpeleka mental institution akakaa huko kwa muda. ni agent mmoja hivi wa shetani, ni kama ana mapepo fulani hivi, ni kama ana mashetani, ukimsikiliza kwa makini na kufuatilia nyendo zake, lazima utajua kuwa hata kama nut moja kichwani haipo, basi unaweza jua kuwa kuna pepo toka kuzimu la uchizi linafanya kazi ndani yake.
 
Mimi sikuangalia hicho kipindi maana nina miaka sijawahi kutune in tbc1. Lakini kwa updates za wana jamii forum kuona tu jina Dr Buberwa nikajua tbc sasa imekufa kabisa maana inarusha matangazo ya vichaa.

Dr Buberwa au jina lingine anajiita Nabii kama nabii musa, kwanza alishatabiri mwisho wa dunia ubgekua mwaka juzi.

Pili amesema yeye ndie nabii pekee anaetegemewa,watu wanamtegemea. Anasema kuazia siku amepewa unabii kama wa musa mwaka 2009 march, miaka 39 badae itakua mwisho wa dunia.

Kama alivyisema pasco hapo dr ni insane.

Tukirudi tbc, nadhani kuna haja ya kufita hiyo tv tuanze upya. Kwa hatua iliyofikia unaweza kulipia kama ukiwa na hela wasitangaze taarifa ya habari kwa mwezi mzima na wakakubali au ukawambia taarifa ya habari itangazwe sa 8 usiku wanakubali.
 
Zile dawa za meno nilitumia mara moja tu na siku wahi kung'oa tena jino ingawa lipo lilitoboka lakini sina maumivu.Sijui kama ni ile dawa yake ama imetokea tu maana nilishatoa meno mawili kabla sijatumia.

Nitaipata wapi na shilingi ngapi, nasumbuliwa na meno mkuu
 
Back
Top Bottom