kulingana na uzoefu wa kupitia chaguzi mbalimbali zinazofanyika hapa nchini kwetu kuanzia upigaji wa kura, uhesabuji, ujumlishaji na hatimaye utangazwaji wa mshindi ni kazi ambayo huwa inachukua muda. Tukiacha matokeo ya urais, hata matokeo ya ubunge Mara nyingi huchukua mda hadi msimamizi wa uchaguzi wa jimbo kumtangaza mshindi. sasa unaweza kutathimini jinsi kazi hii ilivyokuwa rahisi huko Zanzibar hasa kwenye uchaguzi huu wa marudio tofauti na ilivyokuwa imezoeleka katika chaguzi mbalimbali ambapo tayari mida ya asubuhi tu mshindi wa urais kashapatikana. kila la heri kwa aliyetangazwa mshindi