Nina wasiwasi jamaa ataua mtu siku za karibuni

Nina wasiwasi jamaa ataua mtu siku za karibuni

okon

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2008
Posts
305
Reaction score
92
Kuna mshikaji hapa mtaani mkewe kazaa na jirani yake na mtoto ni copyright na babaake. Yaani kila kitu, ni aibu. Katoto chenyewe kanafanana na watoto wa jirani (bana mzazi). Mtaani kila mtu anajua na mshikaji anajua pia ila watu wanasema/wanafikiri kaamua kupotezea, yaani there is no way unaweza usijue kuwa mtoto siyo wake kwa sababu jamaa (jirani) karandisha mbaya.

Sasa ukienda pale kwake ukishika kile kitoto halafu baadae ukakiambie nenda kwa baba jamaa anakuangalia wewe na hicho kitoto yaani kwa jicho kali ile mbaya. Halafu ukimwangalia macho yake yaani yanadisplay evil.

Siwezi elezea lakini naogopa ile mbaya, ni kama yanatangaza death.
 
Mtaa gani huo? Jamaa si ahame tu? Anasubiri aje achinjwe?
 
aiseeee angalia usiwe wa kwanza kuuliwa
 
Katoto kana kama mwaka na nusu hivi.
 
Mtaa gani huo? Jamaa si ahame tu? Anasubiri aje achinjwe?
Kuhama hawezi kwa sababu ndio kwanza kamaliza ujenzi wa nyumba yake ya maana hapa kitaa.
 
Kuhama hawezi kwa sababu ndio kwanza kamaliza ujenzi wa nyumba yake ya maana hapa kitaa.

Apangishe aondoke aisee. Kwa hiyo alipokuwa anakuja kusimamia ujenzi akawa anasimamia na wake za watu?
 
Sasa wewe kwa jirani yako unaenda kufuata nini hadi unaona mwanae kafanana na nani? Usikute jamaa anaona mtoto kafanana na wewe!
 
jirani na wewe mmbea.sasa mpaka umwambie,nenda kwa baba yako ndio nini?unachunguza mpaka anakuangaliaje.mmh na wewe umezidi.waachie wenyewe
 
umbea tu. Mambo ya nyumba za watu yanakuhusu nini? unatuletea umbea JF ili tufanye nao nini????
 
pole yake kwani kapima DNA?

Yaani hata wewe ukionyeshwa hao watu hautahitaji hata DNA. Halafu sasa huyo mwanamke aliezalishwa alimsimulia rafiki yake kipenzi ukweli rafikiye akavujisha kabla hata mtoto hajazaliwa
 
Sasa wewe kwa jirani yako unaenda kufuata nini hadi unaona mwanae kafanana na nani? Usikute jamaa anaona mtoto kafanana na wewe!

Sasa kama hamtembeani kuna ujirani hapo?
 
mambo mengine magumu sana.....sijui watu wanavumilia vipi...?
 
Si jamaa wala mke wake aliyekulalamikia.

Sasa wewe kinachokuuma hasa ni nini?!
 
Watu wengine bwana!

Nyie ndo mnatandikiwa mazulia mlangoni yameandikwa "Umekuja kutembea, usikalie umbea"
 
Ujirani ni kupakana (kushare mipaka) na sio lazma kutembeleana. Yaani kama saa hizi nilivyochoka nawaza tu kitanda afu jitu lije kupoteza muda kwangu. Nampa makavu aisee
Sasa kama hamtembeani kuna ujirani hapo?
 
Back
Top Bottom