Nina uhakika kuna nchi moja kubwa tu katika Jumuiya ya Maziwa Makuu haijafurahishwa na Ushindi wa Felix Tshishekedi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Sasa ni wakati muafaka kabisa wa hiyo nchi Kuwarudisha Wanajeshi wake kwani aliokuwa akiwaunganisha na kuwapa ' mchongo ' wa Kupiga ' Dili ' za ' Dhahabu ' Rais Kabila kupitia ' Gogo ' lake Emanuel Ramazan Shadary wameangukia pua na sasa Wakongo ( Bandeko Nangai ) watapenda Kujiongoza wenyewe na siyo kwa ' Janja Janja ' ya kujifanya mnawalinda kumbe mnawaibia rasilimali zao.

Akhsanteni sana ' Bana Kongo ' kwa hayo Maamuzi yenu hivyo ni matumaini yangu makubwa tu sasa kwamba Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila sasa atarudi na pengine hata Kuishi katika hiyo nchi ambayo ' Mstaafu ' wake mmoja ' alineemeka ' vilivyo na ' Mali ' za Kongo kupitia Kamanda wake mmoja Kijeshi ambaye nae pia kwa sasa ameshastaafu.

Nitoe RAI tu kwa hiyo nchi moja kubwa katika Jumuiya ya Maziwa Makuu kwamba huu ni wakati sasa wa Kuonyesha Upendo wenu kwa Kabila kwa Kumuhifadhi ili awe anaangalia vyema sasa Vitega Uchumi vyake vingi tu alivyoviwekeza hapo kwani msitegemee tena Rais aliyeshinda Tshilombe Felix Tshishekedi akawa ' Popoma ' kama Kabila na mumtumie na kuzinyonya ' Rasilimali ' za Congo DR kwa Kigezo cha kuwa mnawalinda.

Sijui na Rais wa hiyo nchi Siku ambayo Rais Tshishekedi ataapishwa nae ataenda Kinshasa au kama kawaida atamtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje au Namba Mbili wake kama siyo namba Tatu wake.

Kazi ipo na Kumekucha!

Nawasilisha.
 
Sio ile nchi unayojitapa nayo sana humu kuisifia + Rais wake


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hahahahaa,Rafiki yake mtu fulani atakuwa kamuambukiza mwenzake kutofurahia jambo hilo!
 
Back
Top Bottom