Mh! mshiko wa escraw vipi mkuu?
Iv hawa Viongozi N nn??..Mbona tunapigwa changa la Macho!!! Et nitainua uchumi wa Nchi mara nina tiba ya Umaskini Blah blah Buku kidogo..Kwan si walikua na Bado wapo serikalin??...Kwa nini wasinge fanya ayo kabla Wanaboa mno yan Cheo kidogo kimekushinda Iyo Taasisi Utaiweza???...Sasa Siasa sishabikii na kura yangu Simpi mtu..Mxiiiiiiiiiiiiiiuuu...
Jamaa hana mpinzani huyu lazima achukue hii dollla, maana anaonekana ni mwanamapinduzi wa kweli kwa maendeleo ya mtanzania
iTunaijua tiba yako Prof. Muhongo - Watanzania wote tuuze juice
Yeye alikuwa wapi wakati fedhabza Escrow zinabebwa na Lumpesa? Alisaidia vipi Vibaka wasichukue nchi?
Kamuulize wakili fulani ivi aliigeuzaga Tanesco kitega uchumi chake??? Alafu uone kama utarudi na ilo swali lako humu.Amesemaje kuhusu rushwa na ufisadi? Na ambao tayari wameshatuibia na wanajulikana wamezificha uswizi je anacho kiburi cha kuwashughulikia hao watakaokuwa wanamzungusha nchi nzima kumuombea kura ya urais?
Embu fafanua mkuu, ilikuwaje kwanza fedha za escrow zikabebwa??? Na alishiriki vipi either kwa kunufaika au kwa kuzembea?????
Na hadi sasa kuna ripoti yoyote ya uchunguzi iliyomtaja alizembea au aliacha vibaka wachukue nchi??? Tuwekee hapa basi mkuu.
Ila usikimbie tu.
Ondoa shaka, huyu mzee ni jembe.... yupo juu halipingiki. Just imagine kipindi kifupi alichokuwa pale wizarani makubwa aliyoyafanya. Tuombe hao CCM wampitishe, mzee mzuri
Fedha za Escrow zilizomuondosha Mama Tibaijuka zimechukuliwa Muhongo akiwa waziri wa Nishati na Madini.
Zile zilikuwa bado fedha za Tanesco kwa nusu yake. Pia kodi haikulipwa.
Wakili wa Tanesco aliyekuwa akishughulikia hili swala, alifukuzwa kazi kiaina na Muhongo akaja kumtukana Bungeni huku akijua huyo jamaa hawezi kujitetea. Mbowe ndiyo alisimama na kuonyesha barua ambayo jamaa alipewa baraka zote na TANESCO kwenda kuiwakilisha huko Malaysia. Kwa maana hiyo, yeye aliwasaidia vibaka hizo fedha zichotwe.
Mikataba yote ya Mafuta na Gas na madini kwa ujumla, alizuia hata kamati za Bunge zisione. Yaani hata Wabunge hawawezi kuona mikataba hiyo. Halafu bado unadhani CCM kuna msafi wa kuwa Rais wa nchi hii?
Sihitaji kufafanua zaidi kwani ukweli unajulikana kwa miaka mingi. Kama hutaki kuona, basi hata jua utashindwa kuliona saa sita mchana ukiwa umesimama jangwani.
Unazungumzia aliyekuwa wakili wa Tanesco???? Kama hujui fanya utafiti ndugu,mimi pia ni mwanasheria na najua kwa jinsi gani wanasheria wenzangu wanavoifisadi hii nchi kupitia mashirika ya umma. Kwa kukusaidia mtafute mtu yeyote wa Tanesco akuelezee mtandao wa wanasheria ulivokuwa unaifisadi tanesco na jinsi Prof Muhongo alivousambaratisha. Then njoo kwangu kama utakuja na iyo point yako kuhusu huyo mtu.
)Kama wewe ni MwanaSheria basi ni wale Wanasheria wa Kikwete wa Vodafast. Uko mweupe, husomi na hufuatilii kabisa haya mambo. Hebu soma hapa chini nondo za asiye MWANASHERIA kama mimi:
UNAMJUA MWANASHERIA ALIYESULUBIWA NA BODI YA TANESCO BAADA YA KUIKATAZA ISITOE RUHUSA YA KULIPA HELA ZA TEGETA ESCROW KWA IPTL? HUYU HAPA!
![]()
Dar es Salaam. Former Tanesco lawyer Godwin Ngwilimi has opened up about his role in the investigation into the Tegeta Escrow account, saying "time will ultimately prove me truthful."
On Wednesday when presenting a statement by the Parliamentary Public Account Committee (PAC) on the Controller and Auditor General's report on the Tegeta escrow account, PAC chairman Zitto Kabwe claimed that Mr Ngwilimi was sacked for advising the board not to release Tegeta Escrow money to IPTL.
According to Mr Kabwe, the former Tanesco lawyer, who had just visited Malaysia, wrote a letter to the company's managing director warning him against the release of Sh306 billion to IPTL. The reason for the lawyer's move, Mr Kabwe said, was due to controversy surrounding Pan African Power Solution's acquisition of Piper Links shares in IPTL.
Reached for comment yesterday, Mr Ngwilimi preferred not to go into details claiming only time will clear him. "I don't want to get involved in the debate but only time will tell; the truth always comes out when the time is right," he says.
Mr Ngwilimi said he fulfilled his responsibility as Tanesco's lawyer to advise decision makers over the PAP acquisition of Piper Links shares in IPTL.
"My work was simply to advise Tanesco management but whether they worked on my advice or not isn't up to me; but at least they had to consider my advice when making their decisions." .
However, the government dismissed claims that Mr Ngwilimi was sacked. According to the Energy and Minerals minister, Prof Sospeter Muhongo, the lawyer actually resigned on his own volition.
"Mr Ngwilimi wasn't sent to Malaysia by Tanesco to investigate PAP acquisition of Piper Links; in fact he lied to the power utility firm's management that he along with other official from Attorney General office were sent by the AG to Malaysia," said Prof Werema.
From:https://disqus.com/home/discussion/mwananchinew/profesa_muhongo_ajiuzuru_asema_yeye_ni_mtu_safi/
On the other hand, Mr. Mbowe said ex-Tanesco chief legal counsel Godwin Ngwilimi was sent by the government to Malaysia to conduct due diligence on PAP refuting Energy Minister Prof. Sospeter Muhongo earlier statement that Mr. Ngwilimi acted and designed on his own accord.
From: Tanzania - MPs Divided On Escrow Debate - Pesatimes
)
Unajua hapa ndo tofauti yetu inapoonekana, hichi ulicholeta ni taarifa ya gazeti tu(mwananchi) sio ripoti ya CAG au PCCB ambao ndo walichunguza. Sasa ndo uone tofauti yangu mimi na wewe ipo wapi. Alafu kwa hiyo statement Muhongo anasema Mr. Ngwilimi resigned. So kama unachotaka kusema ni ngwilimi alifukuzwa ulitakiwa ulete uthibitisho wa barua aliyoandikiwa ya kufukuzwa and not otherwise ili kumuhusisha Muhongo. Au nianze kukufundisha mbinu za kuwasilisha ushahidi??
Alafu hata kama hoja ni yeye kuresign kwa kuishauri Tanesco ISILIPE still aliyetoa ridhaa kwa zile pesa kulipwa ATTORNEY GENERAL WEREMA and not PROF MUHONGO. Na kimajukumu yeye ndo mshauri NO 1 wa serikali kwenye masuala ya sheria. Sasa kwa nini unamuingiza MUHONGO hapo?????
Alafu ndugu nimekwambia tena jaribu kufuatilia jinsi mtandao wa wanasheria ulivyoifisadi nchi kupitisa TANESCO. uliza hata mfanyakazi yeyote unayemuamini wa TANESCO alafu akwambie Muhongo alifanyaje kudeal na huo mtandao wao.
Acha uvivu wa kusoma, soma kila kitu ndiyo uje kumjibu Ngosha wa ukweli. Hayo maneno ya Mbowe na Muhongo yalisikika Bungeni Live na wengi tuliona. Kama hukuona au hukuelewa basi FUNIKA KIKOMBE.
DK.KIGWANGALA: SIJAWAHI KUONA MSOMI MWENYE UMAHIRI WA KUDANGANYA KAMA PROF. MUHONGO
Sikiliza kuanzia: 6:00 ila kwa maneno ya Muhongo kudanganya ni kuanzia 8:00
Ndugu mbona unazidi kujiaibisha humu???? Hichi ulicholeta ndo nini sasa??? Ndo ushahidi wako??? Nimeshakwambia the only way to prove kuwa Muhongo alidanganya ni kwa kuleta iyo barua aliyoandikiwa Ngwilimi ya kufukuzwa kazi!!! Nothing more Hujaelewa nini sasa hapa ndugu????
Turudi kwa hivyo unavyodai ndo viushahidi vyako, serious ndugu yangu unanipotezea muda tu kumbe!!!!no one anakataa kuwa escrow fedha hazikutakiwa kutoka, kinachosemwa na mimi hapa ni kuwa Muhongo HAKUHUSIKA na huo wizi, uruhusuji wa hizo pesa kutoka au hata HAKUFAIDIKA na ile miamala. Na hiyo ushahidi wake uko wazi kwa sababu hakutajwa kwenye ripoti ya CAG na wala hakuitwa kwenye tume ya maadili.
Sasa wewe unayedai alihusika ndo nakwambia weka ushahidi wako hapa kila mtu auone. Acha porojo na kurukia kuleta viclip vya mtu tu anaongea. And by the way who is kingwalala ambaye hata hapo kwenye clip anadai tu Muhongo muongo lakini asemi uongo wake ni upi. Alafu kwa aibu yako nawe hata huyo kingwalala hapo amejichanganya amesema Muhongo hakuhusika na huo wizi sasa hukuipitia nini kabla ya kuiweka humu????? Kwa sababu inapingana na hoja yako kuu ya kumuhusisha Muhongo na escrow.
Listen ndugu,kizazi cha Tanzania kimebadirika na watu tunahoji kila kitu hadi mwisho. Sasa kama kuna watu unawajua walimfix Muhongo ili tu kumkomoa na kumuondoa pale ili wanufaike na vitalu vya gesi waambie mbona hatuoni uhusika wa huyu mtu????? Au hawakujipanga vizuri?????
Cha zaidi waambie tu waaanze kujiandaa kuweka mapato yao wazi ili walipe kodi stahiki maana hiyo ni moja ya sera ya Muhongo akiingia madarakani.
Ndiyo maana nakuita KICHWA MAJI. Nani anaongelea barua ya KUFUKUZWA KAZI huyo Mwana Sheria wa Tanesco?
Hapa ugomvi ni safari ya Mwanasheria wa Tanesco kwenda Malaysia ambayo huyo MJOMBA wako Muhongo alikataa bungeni kuwa hakutumwa na Tanesco. Hili ndiyo lilimuamsha Mbowe aje apinge kudhalilishwa kwa Mwanasheria huyo.
Vithibitisho kuwa Wakili alitumwa na TANESCO na akaja kutoa ushauri ambao wao Muhongo, Werema na serikali kwa ujumla ukiongeza na Tanesco waliukataa maana ulikuwa unazuia fedha za Escrow kuchukuliwa upo chini kwenye link. Wewe heri ukubali yaishe vinginevyo Prof. Muhongo nondo zake zitazidi kuanikwa hapa.
Ni heri hata useme alilazimishwa ila haikuwa nia yake (hili hata mimi naamini ndivyo ilivyokuwa) ila kusema Muhongo hakusema hivyo, unajitia AIBU. Alichemsha sana kumshambulia na tena anajitapa "...tulifanya makosa tukakubali barua yake ya kujiuzulu peke yake, ilitakiwa tumshtaki mahakamani...." Too sad.
Barua hizi hapa: MTWARA KUMEKUCHA: SINEMA YA ESCROW INAENDELEA...............
Amezidi majisifu na majigambo....kamwe hatufai
Hivi wewe ni mzima kweli ndugu yangu???? hujioni unavogeuka vitu unavovileta mwenyewe????? Unajua watu wanakusoma humu.
Haya ngoja nimalizane na wewe ile ujue mimi ni mtu wa facts na sio porojo,hichi ndo ulichokiweka ona sasa,
However, the government dismissed claims that Mr Ngwilimi was sacked. According to the Energy and Minerals minister, Prof Sospeter Muhongo, the lawyer actually resigned on his own volition."Mr Ngwilimi wasn't sent to Malaysia by Tanesco to investigate PAP acquisition of Piper Links; in fact he lied to the power utility firm's management that he along with other official from Attorney General office were sent by the AG to Malaysia," said Prof Werema.
Au labda hujui kiingereza nikutafsirie, icho ulichoweka kinamaanisha ivi kwa kifupi, aliyesema ngwilimi alijiuzuru nafasi yake na hakufukuzwa ndo Muhongo na aliyesema Ngwilimi hakutumwa kwenda Malyasia kuchunguza ni Werema.
Sasa ndo mana ninakwambia kama Muhongo alidanganya kuwa Ngwilimi hakufukuzwa bali alijiuzuru, wewe ndo wa kuweka huo ushahidi wa iyo barua aliyoandikiwa na Tanesco ya kufukuzwa kazi ili kurove Muhongo alidanganya
Alafu mbona hata hizo barua zako nyingine kwenye iyo link yako mpya hamna barua inayoonyesha ngwilimi alifukuzwa kazi?????
Mkuu nimwekwambia mimi ni mwanasheria. PLEASE huwezi nidanganya. Take that in your mind.