Nina tatizo la swinging mood

Nina tatizo la swinging mood

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,872
Reaction score
2,741
Mwenzenu kuna mambo huwa yananitokea nikiyawaza najihisi nina tatizo ila suluhu yake ndo shida kwangu. Naombeni ushauri nifanyeje niwe na positive mind kila wakati.

  • Nikikosana na shemeji yenu, na/au ikitokea nimekaa muda mrefu bila kupata huduma ninakuwa na hasira za ajabu ajabu. Siku hiyo ofisini ninaofanya nao kazi inabidi wawe careful au akija mteja nimhudumie basi nakuwa na majibu ya mkato na ghadhabu mpaka watu wananiogopa. Mtu akichemsha kidogo tu naweza mtoa baru. Baadaye nikija kuongea na mtu in a very polite way, au nikimtokea mtu nimempenda, jambo la kwanza ananiambia mbona wewe mkali sana. Hii kitu inaniumiza.
  • Kuna wakati nakuwa mpole sana kuliko maelezo. Ninakuwa very charming, very positive and you can really enjoy kuwa na mimi. Hapo nikianza kupigisha story siishiwi iwe siasa, dini, elimu, mapenzi, biashara au chochote.
  • Kuna wakati ninakuwa na hali ya kupenda sana yaani inakuwa tabu kweli. Nikimtokea mtu nimempenda hapo i can do anything.
  • Kuna wakati nawachukia wanawake wote kasoro mama yangu. Najikuta sina hamu ya mapenzi, alafu nikikumbuka michepuko niliyowahi kutoka nayo najiona ----- kweli. Sasa wakati huo ikitokea kuna mchepuko ananitaka nitoke naye anaweza akajuta kunifahamu. Hapo nawaza maisha yangu tuu, na sitaki mtu anisemeshe. Ila baadaye hii hali ikipita nakuja kumuomba msamaha.
  • Kuna wakati narudia mambo ya Mungu, nakwenda kanisani nafanya kila niwezalo, natubu dhambi zangu zote, naimba kwaya, natoa michango, yaani mpka naona raha.
  • Kuna wakati huko kanisani nako kunaanza kuboa, najikuta narudi mawazo ya mwanzo, especially nikiona huko kanisani yanayofanyika ndivyo sivyo. Hapo ni rahisi sana kurudia kule kwa michepuko.
Kwa leo naishia hapa
 
Aisee!!! Pole sana,but you just need somebody to take care of you and your feelings.
 
Unaelekea kupata depression...jitahidi kufanya vitu vinavyo kuintertain na kukupa furaha kama michezo,musics,games,kusoma novels etc na hilo suala la kwenda kanisani uendelee nalo huku ukimwomba Mungu akupe furaha ya kweli inayopatikana kwake. Hizi furaha zingine zote ni za kimwili zaidi na ni za muda mfupi tu.
 
'mood swing '

baadhi ya unayo yafanya ni kawaida tu
part of growing...

hujasema umri wako na afya yako ikoje..

unaweza kuwa huna tatizo.....
 
kimwili hakuna tatizo hapo ni hali ya kawaida.

kiroho mrudie Muumba wako, acha michepuko, tubu dhambi na usikubali lolote likutenge na upendo wa Mungu...

mda wa mapumziko soma Biblia... kaa na watoto kama unao.

au kaana marafiki ukiwa na mkeo mbadilishane mawazo.
 
Mwenzenu kuna mambo huwa yananitokea nikiyawaza najihisi nina tatizo ila suluhu yake ndo shida kwangu. Naombeni ushauri nifanyeje niwe na positive mind kila wakati.

  • Nikikosana na shemeji yenu, na/au ikitokea nimekaa muda mrefu bila kupata huduma ninakuwa na hasira za ajabu ajabu. Siku hiyo ofisini ninaofanya nao kazi inabidi wawe careful au akija mteja nimhudumie basi nakuwa na majibu ya mkato na ghadhabu mpaka watu wananiogopa. Mtu akichemsha kidogo tu naweza mtoa baru. Baadaye nikija kuongea na mtu in a very polite way, au nikimtokea mtu nimempenda, jambo la kwanza ananiambia mbona wewe mkali sana. Hii kitu inaniumiza.
  • Kuna wakati nakuwa mpole sana kuliko maelezo. Ninakuwa very charming, very positive and you can really enjoy kuwa na mimi. Hapo nikianza kupigisha story siishiwi iwe siasa, dini, elimu, mapenzi, biashara au chochote.
  • Kuna wakati ninakuwa na hali ya kupenda sana yaani inakuwa tabu kweli. Nikimtokea mtu nimempenda hapo i can do anything.
  • Kuna wakati nawachukia wanawake wote kasoro mama yangu. Najikuta sina hamu ya mapenzi, alafu nikikumbuka michepuko niliyowahi kutoka nayo najiona ----- kweli. Sasa wakati huo ikitokea kuna mchepuko ananitaka nitoke naye anaweza akajuta kunifahamu. Hapo nawaza maisha yangu tuu, na sitaki mtu anisemeshe. Ila baadaye hii hali ikipita nakuja kumuomba msamaha.
  • Kuna wakati narudia mambo ya Mungu, nakwenda kanisani nafanya kila niwezalo, natubu dhambi zangu zote, naimba kwaya, natoa michango, yaani mpka naona raha.
  • Kuna wakati huko kanisani nako kunaanza kuboa, najikuta narudi mawazo ya mwanzo, especially nikiona huko kanisani yanayofanyika ndivyo sivyo. Hapo ni rahisi sana kurudia kule kwa michepuko.
Kwa leo naishia hapa

uache bange za kuvutia chooni
 
Matatizo ya Bangi na viroba haya,,,acha kuvuta bangi mdogo wangu
 
Mkuu wewe ni mgonjwa wa akili wahi hospital mapema upate msaada wa kitaalam. Kuna siku utatembea bila nguo
 
Nafikiri upo katika umri wa kukua, naamini unakaribia Kumaliza adolescents
 
Back
Top Bottom