Ugonjwa wa Kusahau/Kupoteza Kumbukumbu: Dalili, Tiba na Ushauri wa Kukabiliana na Hali Hii

Habari wana jf,

Nina ndugu umri anagika miaka 60, kwenye siku za hivi karibuni amekuwa anapoteza kumbukumbu naomba mnisaidie hospital gani kwa hapa dar naweza mpeleka akafanyiwa vipimo na kupata matibabu.

Natanguliza shukrani
 
Habari za humu ndani madaktari wa Jforums,

Mimi huwa nashindwa kukariri watu ninaokutana nao mara kwa mara, mfano tunaweza tukakutana na wewe kwa mara ya kwanza au mara ya pili tukaongea halafu ikitokea tumekutana sehemu nyingine siku tofaut naweza kukusahau mpaka unikumbushe.

Au mke wa rafiki yangu anaweza akapita nikatambulishwa akipita tena siku nyingine nakuwa nimemsahau, au nikikutana na mtu anahitaji huduma ofisini kwangu akishatoka hata dakika moja tu nikiulizwa alikuwa amevaa nguo za rangi gani nakuwa siwezi au sikumbuki rangi za nguo zake na sura yake pia hadi arudi.

Je, hili ni tatizo au kawaida tu?

Nawasilisha
 
Ilikuwa nina hali kama hiyo kuna mtalaamu kiasi aliniambia kitu kidogo nimekifanyia kazi sasa hivi nipo vizuri. Aliniambia kuwa sio mdadisi na huwa sijali matukio ninayokutana nayo kwa kifupi aliniambia (simakiniki na matukio yanayonijia usoni) yani unaweza akaja mtu ukaongea nae akaondoka bila kudadisi kitu chochote kinacho mhusu mf. nguo na sura.

Sababu kubwa huwa ubize wa kazi au tu ni tabia ya kutofwatilia mambo ya wengine. Mkuu itulize akili yako unapokutana na mtu wa aina yoyote ile mdadisi kuanzia juu mpaka chini ongea nae, kesho ukikutana nae kipo angalau kimoja kitakukumbusha kuhusu huyo mtu,endelea hivyo hivyo mpaka utaona unazoea na akili inakuwa active.

Subiri Wataalamu wa akili watakupa muongozo
 
Ilikuwa nina hali kama hiyo kuna mtalaamu kiasi aliniambia kitu kidogo nimekifanyia kazi sasa hivi nipo vizuri, Aliniambia kuwa sio mdadisi na huwa sijali matukio ninayokutana nayo kwa kifupi aliniambia(simakiniki na matukio yanayonijia usoni) yani unaweza akaja mtu ukaongea nae akaondoka bila kudadisi kitu chochote kinacho mhusu mf.nguo na sura.
Umeniongelea mimi kabisa hapo. Hua sipendi kufatilia wala kuhangaisha akili yangu kwa mambo ya watu yasiyonihusu na hilo tatizo la kusahau pia hua linanitokea mara kadhaa.

Nitajitahidi kufata huo ushauri
 
Umeniongelea mimi kabisa hapo. Hua sipendi kufatilia wala kuhangaisha akili yangu kwa mambo ya watu yasiyonihusu na hilo tatizo la kusahau pia hua linanitokea mara kadhaa.
Nitajitahidi kufata huo ushauri
kuna siku nimewai kupoteza kitu kizembe sana kwa kutomkumbuka mtu sasa hivi nipo makini sana,nikshindwa kukariri sura hata kiatu alichovaa yani angalau chochote kinachomhusu mhusika kiwe kichwani kwa matumizi ya badae.
 
kuna siku nimewai kupoteza kitu kizembe sana kwa kutomkumbuka mtu sasa hivi nipo makini sana,nikshindwa kukariri sura hata kiatu alichovaa yani angalau chochote kinachomhusu mhusika kiwe kichwani kwa matumizi ya badae.
Mimi sura nakumbuka vizuri sana, tatizo maongezi hasa jina na yale atakayoniambia kama hayanihusu direct basi akigeuka nishasahau.
 
Kumbe bora Mimi. Naweza mkumbuka mtu sura yake ila jina sasa ukawa mtihani mkubwa kukumbuka..😅
lkn hili mi si tatizo naona ni kawaida kwangu naweza pia kuwa na kumbukumbu huyu nilishawahi onana nae lkn sikumbuki ilikuwa ni mahali gani.

Mkuu hali yako inatakiwa iwe na wastani usitopee kivile kumkumbuka kila mtu! Kula vyakula natural ndugu kula samaki, maboga, mboga za majani n.k

Huenda itasaidia kuweka kumbukumbu sawa.
 
Nadhani tatizo ni IQ umezaliwa nayo ndogo. Mie nikikutana na mtu na akinitajia jina simsahau labda ipite miaka. IQ yangu kubwa of course
 
Ilikuwa nina hali kama hiyo kuna mtalaamu kiasi aliniambia kitu kidogo nimekifanyia kazi sasa hivi nipo vizuri. Aliniambia kuwa sio mdadisi na huwa sijali matukio ninayokutana nayo kwa kifupi aliniambia (simakiniki na matukio yanayonijia usoni) yani unaweza akaja mtu ukaongea nae akaondoka bila kudadisi kitu chochote kinacho mhusu mf.nguo na sura...
Asante Sana wang shu nimekuelewa
 
Habari za humu ndani madaktari wa Jforums,

Mimi huwa nashindwa kukariri watu ninaokutana nao mara kwa mara, mfano tunaweza tukakutana na wewe kwa mara ya kwanza au mara ya pili tukaongea halafu ikitokea tumekutana sehemu nyingine siku tofaut naweza kukusahau mpaka unikumbushe...
Wewe binafsi huwa unajikumbuka ama kuna wakati pia unajisahau kama ni wewe? Tatizo lako litakuwa la kiufundi zaidi, plug zitakuwa hazichomi vizuri hivyo kusababisha kichwa kiingize miss.
 
Back
Top Bottom